Pate : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
(Hakuna tofauti)

Pitio la 16:06, 21 Mei 2006

Pate ni kisiwa kikubwa cha funguvisiwa vya Lamu mbele ya pwani la Kenya katika Bahari Hindi. Pate ni kisiwa ambacho ni karibu na Somalia.

Pate ilikuwa kati ya mahali pa kwanza pa kutembelewa na wafanyabiashara Waarabu, labda kuanzia karne ya 7 BK. Inawezekana ilikuwa tayari kati ya mahali palipotajwa katika taarifa za kale kuhusu Azania kama vile Periplus ya Bahari ya Eritrea.

Kisiwa cha Pate kilikuwa mahali pa miji muhimu ya Waswahili Pate, Siyu na Faza iliyoshindana na mji wa Lamu juu ya kipaumbele katika funguvisiwa. Katika karne ya 19 BK umuhimu wa miji hii ilirudi nyuma.

Kisiwa kilikuwa sehemu ya dola la Usultani ya Zanzibar katika karne ya 19.

Hakuna barabara wala magari kisiwani.