Fonolojia : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
+sawazisho dogo tu
No edit summary
Mstari 1: Mstari 1:
'''Fonolojia''' (hasa huitwa '''Sarufi Matamshi''') ni tawi la sayansi ya [[isimu]]. Inashughulikia uchunguzi wa mfumo wa sauti katika lugha fulani, kwa mfano ugawanyaji wa [[irabu]] na [[konsonanti]]. Ala za sauti (vipashio vya utamkaji) zinatumika katika utamkaji wa fonimu (vitamkwa) za lugha husika. Mkondo wa hewa wakati wa utamkaji. Kuwepo na kutokuwepo kwa mguno wakati wa utamkaji (guna/siguna). Utanzu huu hushughulikia kanuni zinazotawala uchambuzi wa mfumo wa sauti, yaani, sauti kutamkwaje na wapi katika kinywa cha mwanadamu.
'''Fonolojia''' (hasa huitwa '''Sarufi Matamshi''') ni [[tawi]] la [[sayansi]] ya [[isimu]]. Inashughulikia [[uchunguzi]] wa [[mfumo wa sauti]] katika [[lugha]] fulani, kwa mfano ugawanyaji wa [[irabu]] na [[konsonanti]].


Ala za [[sauti]] ([[vipashio]] vya utamkaji) zinatumika katika utamkaji wa [[fonimu]] (vitamkwa) za lugha husika. Mkondo wa hewa wakati wa utamkaji. Kuwepo na kutokuwepo kwa mguno wakati wa utamkaji (guna/siguna).
Matokeo ya uchunguzi wa kifonolojia yana umuhimu katika kubuni [[alfabeti]]. Dhana ya fonolojia inajipambanua vizuri zaidi ikifasiliwa kwa kutofautishwa na fonetiki. Wakati fonetiki ni taaluma inayochunguza sauti zitamkwazo na binadamu bila kuzihusisha na lugha yoyote, fonolojia huchunguza mfumo wa sauti wa lugha mahususi kama vile sauti za Kiswahili, Kiingereza, Kimwera, na Kinyaturu. ZINGATIA: Fonetiki huchunguza sauti zote zitamkwazo na binadamu; fonolojia huchunguza MFUMO WA SAUTI wa lugha mahususi.


[[Utanzu]] huu hushughulikia kanuni zinazotawala uchambuzi wa mfumo wa sauti, yaani, sauti kutamkwaje na wapi katika [[kinywa]] cha [[mwanadamu]].
Hivyo, fonetiki huchunguza sauti nyingi kadri iwezekanavyo, lakini fonolojia huchunguza sauti chache tu zilizomo katika mfumo wa sauti wa lugha husika. Mathalani, mfumo wa sauti wa lugha ya Kiswahili una sauti thelathini tu (irabu tano na konsonanti ishirini na tano).


Matokeo ya uchunguzi wa kifonolojia yana umuhimu katika kubuni [[alfabeti]].
Jambo lingine la kuzingatia ni vipashio vya kiuchambuzi vya matawi haya mawili. Wakati fonetiki kipashio chake cha msingi ni FONI, fonolojia kipashio chake cha msingi ni FONIMU. Kwa kuzingatia maelezo ya hapo awali, ni wazi kuwa FONI ni nyingi zaidi kuliko FONIMU, kwakuwa FONI ni kila sauti itamkwayo na binadamu, wakati FONIMU ni sauti zile tu zilizomo katika mfumo wa sauti wa lugha mahususi. Hivyo, kuna FONIMU za Kiswahili, za Kiingereza, za Kichina, n.k., lakini FONI si za lugha yoyote na wala uwezi sema kwa uhakika kuna FONI ngapi, kwakuwa bado kuna lugha nyingi duniani ambazo bado hazijatafitiwa.


[[Dhana]] ya fonolojia inajipambanua vizuri zaidi ikifasiliwa kwa kutofautishwa na [[fonetiki]]. Wakati fonetiki ni [[taaluma]] inayochunguza sauti zitamkwazo na binadamu bila kuzihusisha na lugha yoyote, fonolojia huchunguza mfumo wa sauti wa lugha mahususi kama vile sauti za [[Kiswahili]], [[Kiingereza]], [[Kimwera]] na [[Kinyaturu]]. Kwa ufupi, fonetiki huchunguza sauti zote zitamkwazo na binadamu; fonolojia huchunguza mfumo wa sauti wa lugha mahususi.

Hivyo, fonetiki huchunguza sauti nyingi kadiri iwezekanavyo, lakini fonolojia huchunguza sauti chache tu zilizomo katika mfumo wa sauti wa lugha husika. Mathalani, mfumo wa sauti wa lugha ya Kiswahili una sauti [[thelathini]] tu (irabu [[tano]] na konsonanti [[ishirini na tano]]).

Jambo lingine la kuzingatia ni vipashio vya kiuchambuzi vya matawi haya mawili. Wakati fonetiki kipashio chake cha msingi ni FONI, fonolojia kipashio chake cha msingi ni FONIMU. Kwa kuzingatia maelezo ya hapo awali, ni wazi kuwa FONI ni nyingi zaidi kuliko FONIMU, kwa kuwa FONI ni kila sauti itamkwayo na binadamu, wakati FONIMU ni sauti zile tu zilizomo katika mfumo wa sauti wa lugha mahususi. Hivyo, kuna FONIMU za Kiswahili, za Kiingereza, za [[Kichina]], n.k., lakini FONI si za lugha yoyote, wala huwezi kusema kwa uhakika kuna FONI ngapi, kwa kuwa bado kuna lugha nyingi [[duniani]] ambazo hazijatafitiwa.
== Marejeo ==
== Marejeo ==

Pitio la 13:13, 7 Novemba 2016

Fonolojia (hasa huitwa Sarufi Matamshi) ni tawi la sayansi ya isimu. Inashughulikia uchunguzi wa mfumo wa sauti katika lugha fulani, kwa mfano ugawanyaji wa irabu na konsonanti.

Ala za sauti (vipashio vya utamkaji) zinatumika katika utamkaji wa fonimu (vitamkwa) za lugha husika. Mkondo wa hewa wakati wa utamkaji. Kuwepo na kutokuwepo kwa mguno wakati wa utamkaji (guna/siguna).

Utanzu huu hushughulikia kanuni zinazotawala uchambuzi wa mfumo wa sauti, yaani, sauti kutamkwaje na wapi katika kinywa cha mwanadamu.

Matokeo ya uchunguzi wa kifonolojia yana umuhimu katika kubuni alfabeti.

Dhana ya fonolojia inajipambanua vizuri zaidi ikifasiliwa kwa kutofautishwa na fonetiki. Wakati fonetiki ni taaluma inayochunguza sauti zitamkwazo na binadamu bila kuzihusisha na lugha yoyote, fonolojia huchunguza mfumo wa sauti wa lugha mahususi kama vile sauti za Kiswahili, Kiingereza, Kimwera na Kinyaturu. Kwa ufupi, fonetiki huchunguza sauti zote zitamkwazo na binadamu; fonolojia huchunguza mfumo wa sauti wa lugha mahususi.

Hivyo, fonetiki huchunguza sauti nyingi kadiri iwezekanavyo, lakini fonolojia huchunguza sauti chache tu zilizomo katika mfumo wa sauti wa lugha husika. Mathalani, mfumo wa sauti wa lugha ya Kiswahili una sauti thelathini tu (irabu tano na konsonanti ishirini na tano).

Jambo lingine la kuzingatia ni vipashio vya kiuchambuzi vya matawi haya mawili. Wakati fonetiki kipashio chake cha msingi ni FONI, fonolojia kipashio chake cha msingi ni FONIMU. Kwa kuzingatia maelezo ya hapo awali, ni wazi kuwa FONI ni nyingi zaidi kuliko FONIMU, kwa kuwa FONI ni kila sauti itamkwayo na binadamu, wakati FONIMU ni sauti zile tu zilizomo katika mfumo wa sauti wa lugha mahususi. Hivyo, kuna FONIMU za Kiswahili, za Kiingereza, za Kichina, n.k., lakini FONI si za lugha yoyote, wala huwezi kusema kwa uhakika kuna FONI ngapi, kwa kuwa bado kuna lugha nyingi duniani ambazo hazijatafitiwa.

Marejeo

  • TUKI 1990, "Kamusi Sanifu ya Isimu na Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
  • Massamba, David 2004, "Kamusi ya Isimu na Falsafa ya Lugha", Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fonolojia kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.