Kipindupindu : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1: Mstari 1:
'''Kipindupindu''' (kwa [[Kilatini]] na [[Kiingereza]] ''cholera'' kutoka neno la [[Kigiriki]] χολέρα, kholera, lililotokana na χολή, kholē, [[nyongo]]) ni [[ugonjwa]] hatari unaosababishwa na [[bakteria]] hasa katika [[utumbo mwembamba].Bakteria hao huitwa [(vibriocholerae)]ambao huweza kusababisha [[kuhara]] sana na [[kutapika]] sana pamoja na [[homa]] kali. Kuambukizwa hutokea hasa kupitia [[maji]] au vyakula vilivyochafuliwa na wadudu kama vile nzi. Wadudu kama vile nzi huweza kuchafua vyakula hivyo endapo vyakula hivyo vitaachwa wazi bila kufunikwa na chombo chochote na kusababisha nzi hao kutua juu ya vyakula hivyo na kuacha bakteria watakao sababisha ugonjwa wa kipindupindu kwa mtu yule atakaye kula chakula kile. Kiwango cha kuhara na kutapika kinaleta upungufu wa maji na uwiano wa [[chumvi]] mwilini. Baada ya dalili hizo kutokea kuna hatari ya [[kifo]] kwa [[asilimia]] 20 - 70 ya wagonjwa kama hawana [[tiba]].
'''Kipindupindu''' (kwa [[Kilatini]] na [[Kiingereza]] ''cholera'' kutoka neno la [[Kigiriki]] χολέρα, kholera, lililotokana na χολή, kholē, [[nyongo]]) ni [[ugonjwa]] hatari unaosababishwa na [[bakteria]] hasa katika [[utumbo mwembamba]]. Bakteria hizo ambazo huitwa ''vibriocholerae'' huweza kusababisha [[kuhara]] sana na [[kutapika]] sana pamoja na [[homa]] kali.
Maambukizi hutokea hasa kupitia [[maji]] au [[vyakula]] vilivyochafuliwa na [[wadudu]] kama vile [[nzi]]. Wadudu hao huweza kuchafua vyakula endapo vyakula hivyo vitaachwa wazi bila kufunikwa na chombo chochote na kuvutia nzi hao kutua juu ya vyakula hivyo na kuacha bakteria zitakazosababisha ugonjwa wa kipindupindu kwa [[mtu]] atakayekula chakula kile.
Kiwango cha kuhara na kutapika kinaleta upungufu wa maji na uwiano wa [[chumvi]] [[Mwili|mwilini]]. Baada ya [[dalili]] hizo kutokea kuna hatari ya [[kifo]] kwa [[asilimia]] 20 - 70 ya wagonjwa kama hawana [[tiba]].

Tanzania tunaweza kujilinda na kipindupindu endapo tukajilinda na vitu vifuatavyo ambavyo ni kunywa maji safi na salama na kula chakula kisicho poa. Bila kusahau kusafisha maeneo yote yanayo mzunguka kiumbe hai hasa binadamu. Nchini TANZANIA yatupasa kufanya usafi katika mikoa yetu yote hasa mkoani Dar es alaam ambako kunashutumiwa sana kuwa ni mkoa mchafu.
Tunaweza kujilinda na kipindupindu endapo tukajilinda na vitu vifuatavyo ambavyo ni kunywa [[Maji salama|maji safi na salama]] na kula chakula kisichopoa. Bila kusahau kusafisha maeneo yote yanayomzunguka [[kiumbe hai]], hasa [[binadamu]]. Yatupasa kufanya [[usafi]] katika mikoa yetu yote, hasa [[Jiji|majijini]] ambako kunashutumiwa sana kuwa machafu.
[[Picha:Cholera bacteria SEM.jpg|thumb|right|Bakteria wa ''Vibrio cholerae'']]<ref name=Sherris>
[[Picha:Cholera bacteria SEM.jpg|thumb|right|Bakteria wa ''Vibrio cholerae'']]<ref name=Sherris>
Mstari 19: Mstari 24:
| isbn = 978-1-904455-33-2
| isbn = 978-1-904455-33-2
}}</ref>
}}</ref>
[[Picha:Distribution of the cholera.PNG|thumbnail|250px|Kutokea kwa kipindupindu duniani; Nyekundu: kinatokea mara kwa mara; Njano: kinatokea mara kadhaa; Nyeupe: kinatokea mara chache ]]
[[Picha:Distribution of the cholera.PNG|thumbnail|250px|Kutokea kwa kipindupindu duniani. Nyekundu: kinatokea mara kwa mara; Njano: kinatokea mara kadhaa; Nyeupe: kinatokea mara chache.]]
==Ambukizo==
==Ambukizo==
Kipindupindu husababishwa na bakteria aina ya [[Vibrio cholerae]] zinazosababisha kuhara majimaji yenye rangi kama maji ya kupikia [[mchele]]. Bakteria hiyo ilitambuliwa mwaka [[1854]] na [[Filippo Pacini]]. [[Robert Koch]] alifaulu mwaka [[1883]] kufuga bakteria kutokana na [[utumbo]] wa wagonjwa waliokufa kwa kipindupindu huko [[Misri]].
Kipindupindu husababishwa na bakteria aina ya [[Vibrio cholerae]] zinazosababisha kuhara majimaji yenye rangi kama maji ya kupikia [[mchele]]. Bakteria hiyo ilitambuliwa mwaka [[1854]] na [[Filippo Pacini]].


[[Robert Koch]] alifaulu mwaka [[1883]] kufuga bakteria kutokana na [[utumbo]] wa watu waliokufa kwa kipindupindu huko [[Misri]].
Kipindupindu hutokea hasa katika nchi pasipo maji safi hasa ambako maji ya kunywa na majimaji ya [[choo]] yanaweza kuchanganyikana. Bakteria ya vibrio cholerae hupatikana hasa katika [[mavi]] na maji ya choo na pia katika maji ya [[bahari]], ma[[ziwa]] na mito kama maji machafu huingizwa katika ma[[gimba]] ya maji bila kusafishwa kwanza.

Kipindupindu hutokea hasa katika nchi pasipo maji safi, hasa ambako maji ya kunywa na majimaji ya [[choo]] yanaweza kuchanganyikana. Bakteria ya vibrio cholerae hupatikana hasa katika [[mavi]] na maji ya [[choo]] na pia katika maji ya [[bahari]], ma[[ziwa]] na [[mito]] kama maji machafu huingizwa katika ma[[gimba]] ya maji bila kusafishwa kwanza.


Vilevile [[samaki]] na vyakula vingine kutoka maji yenye bakteria vinachafuliwa na vinaweza kusababisha [[ambukizo]]. Vilevile vyakula vinavyooshwa kwa maji yaliyochafuliwa na bakteria ya kipindupindu.
Vilevile [[samaki]] na vyakula vingine kutoka maji yenye bakteria vinachafuliwa na vinaweza kusababisha [[ambukizo]]. Vilevile vyakula vinavyooshwa kwa maji yaliyochafuliwa na bakteria ya kipindupindu.


Katika [[mazingira]] yenye maji ya [[bomba]], yaliyosafishwa na [[karakana]] ya kusafisha maji machafu, kipindupindu hutokea mara chache tu. Kujulikana kwa njia za kuambukizwa kulikuwa sababu ya kuanzishwa na kugharamiwa kwa [[teknolojia]] hizo katika nchi nyingi.
Katika [[mazingira]] yenye maji ya [[bomba]], yaliyopitia [[karakana]] ya kusafisha maji machafu, kipindupindu hutokea mara chache tu. Kujulikana kwa njia za kuambukizwa kulikuwa sababu ya kuanzishwa na kugharamiwa kwa [[teknolojia]] hizo katika nchi nyingi.


== Matibabu ==
== Matibabu ==
Mstari 50: Mstari 57:


== Kuepukana na Kipindupindu ==
== Kuepukana na Kipindupindu ==

Kinga ni kama ifuatavyo:
Kinga ni kama ifuatavyo:
* wakati wowote kunawa mikono kabla ya kutayarisha au kula chakula, kusafisha vyombo kama [[sahani]], [[vikombe]] n.k.
* wakati wowote kunawa mikono kabla ya kutayarisha au kula chakula, kusafisha vyombo kama [[sahani]], [[vikombe]] n.k.
* Nawa mikono kabisa kwa sabuni – kiganja, upande wa nyuma wa mkono, katikati ya vidole na kucha kwa sekunde. Baada ya haja na kabla ya kula.
* kunawa mikono kabisa kwa sabuni – kiganja, upande wa nyuma wa mkono, katikati ya vidole na kucha kwa sekunde. Baada ya haja na kabla ya kula.
* kuwa na [[akiba]] ya maji yaliyochemshwa pasipo na maji safi ya bomba
* kuwa na [[akiba]] ya maji yaliyochemshwa pasipo na maji safi ya bomba
* kupika [[chakula]] vizuri maana [[halijoto]] juu ya 75 °C (hadi 85 mlimani) inaua bakteria;
* kupika [[chakula]] vizuri maana [[halijoto]] juu ya 75 °C (hadi 85 mlimani) inaua bakteria;
Mstari 62: Mstari 68:
* mikono inayoshika wagonjwa au [[nguo]] zao inapaswa kunaniwa kwa [[sabuni]]
* mikono inayoshika wagonjwa au [[nguo]] zao inapaswa kunaniwa kwa [[sabuni]]
* mashimo ya choo yanapaswa kutiwa dawa za kuua bakteria kwa kutumia [[klorini]]
* mashimo ya choo yanapaswa kutiwa dawa za kuua bakteria kwa kutumia [[klorini]]
* Tumia maji yaliyotibiwa pekee hasa ikiwa ni ya kunywa; yachemshe au utie matone 5 ya [[klorini]] kwa kila galoni 1 au utumie dawa ya kutakasa maji. Yaache maji yatulie kwa dakika 30 kabla ya kunywa.
* Tumia maji yaliyotibiwa pekee hasa ikiwa ya kunywa; yachemshe au utie matone 5 ya [[klorini]] kwa kila [[galoni]] 1 au utumie dawa ya kutakasa maji. Yaache maji yatulie kwa [[dakika]] 30 kabla ya kunywa.
* Tumia choo kila mara – usiende haja karibu au ndani ya chanzo cha maji.
* Tumia choo kila mara – usiende haja karibu au ndani ya chanzo cha maji.


Mstari 68: Mstari 74:
Mnamo miaka [[1816]]-[[1826]] kulikuwa na '''[[janga]] la kwanza la kipindupindu''' mkoani [[Bengal]], nchini [[India]]. [[Waingereza]] 10,000 na [[Wahindi]] walikufa.<ref>[http://www.earlyamerica.com/review/2000_fall/1832_cholera_part1.html The 1832 Cholera Epidemic in New York State], By G. William Beardslee.</ref>
Mnamo miaka [[1816]]-[[1826]] kulikuwa na '''[[janga]] la kwanza la kipindupindu''' mkoani [[Bengal]], nchini [[India]]. [[Waingereza]] 10,000 na [[Wahindi]] walikufa.<ref>[http://www.earlyamerica.com/review/2000_fall/1832_cholera_part1.html The 1832 Cholera Epidemic in New York State], By G. William Beardslee.</ref>


Janga la '''pili la kipindupindu''' lilikuwa mnamo [[1829]]-[[1851]] kilipoenea nchini [[Urusi]], [[Hungaria]], [[Ujerumani]] na [[Uingereza]]. Zaidi ya watu 55,000 walikufa kutoka Uingereza pekee.<ref>[http://www.ph.ucla.edu/EPI/snow/pandemic1826-37.html Asiatic Cholera Pandemic of 1826-37].</ref> Mwaka [[1831]], watu 150,000 walikufa kutokana na janga hili nchini [[Misri]].<ref>[http://whqlibdoc.who.int/bulletin/1947-1948/Vol1-No2/bulletin_1948_1(2)_353-381.pdf Cholera Epidemic in Egypt (1947)].</ref>
'''Janga la pili la kipindupindu''' lilikuwa mnamo [[1829]]-[[1851]] kilipoenea nchini [[Urusi]], [[Hungaria]], [[Ujerumani]] na [[Uingereza]]. Zaidi ya watu 55,000 walikufa katika Uingereza pekee.<ref>[http://www.ph.ucla.edu/EPI/snow/pandemic1826-37.html Asiatic Cholera Pandemic of 1826-37].</ref> Mwaka [[1831]], watu 150,000 walikufa kutokana na janga hili nchini [[Misri]].<ref>[http://whqlibdoc.who.int/bulletin/1947-1948/Vol1-No2/bulletin_1948_1(2)_353-381.pdf Cholera Epidemic in Egypt (1947)].</ref>


Mwaka [[1849]], kipindupindu kilizuka tena kwa mara ya pili mjini [[Paris]].<ref>[http://www.oocities.com/CapitolHill/Congress/2807/irishfamine.html The Irish Famine].</ref> Mjini [[London]] watu 14,137 walikufa.
Mwaka [[1849]], kipindupindu kilizuka tena kwa mara ya pili mjini [[Paris]].<ref>[http://www.oocities.com/CapitolHill/Congress/2807/irishfamine.html The Irish Famine].</ref> Mjini [[London]] watu 14,137 walikufa.
Mstari 76: Mstari 82:
Mnamo [[1991]]-[[1994]] kulikuwa na janga lingine huko [[Amerika Kusini]], lililosababishwa na [[meli]] iliyomwaga maji machafu. Nchini [[Peru]] watu takriban 10,000 waliuawa.
Mnamo [[1991]]-[[1994]] kulikuwa na janga lingine huko [[Amerika Kusini]], lililosababishwa na [[meli]] iliyomwaga maji machafu. Nchini [[Peru]] watu takriban 10,000 waliuawa.


Mwaka [[2000]], wagonjwa 14,000 waliripotiwa kuugua kutokana na kipindupindu. Takriban 87% waliripotiwa kutoka bara la [[Afrika]].<ref>[http://www.worldwaterday.org/wwday/2001/disease/cholera.html Disease fact sheet: Cholera]. IRC International Water and Sanitation Centre.</ref>
Mwaka [[2000]], wagonjwa 14,000 waliripotiwa kuugua kipindupindu. Takriban 87[[%]] waliripotiwa kutoka [[bara]] la [[Afrika]].<ref>[http://www.worldwaterday.org/wwday/2001/disease/cholera.html Disease fact sheet: Cholera]. IRC International Water and Sanitation Centre.</ref>


Julai - Desemba [[2007]]: [[ukame]] wa [[maji salama]] kwa ajili ya kunywa nchini [[Irak]] ulisababisha tena janga la kipindupindu.<ref>{{cite news |first= |last= |authorlink= |author= |coauthors= |title=U.N. reports cholera outbreak in northern Iraq |url=http://www.cnn.com/2007/WORLD/meast/08/29/iraq.cholera/index.html |work= |publisher=CNN |id= |pages= |page= |date= |accessdate=2007-08-30 |quote= }}</ref> Watu 22 walifariki.<ref>[http://www.guardian.co.uk/world/2007/dec/02/iraq.davidsmith Cholera crisis hits Baghdad], The Observer, 2 Desemba 2007.</ref>
Julai - Desemba [[2007]]: [[ukame]] wa [[maji salama]] kwa ajili ya kunywa nchini [[Irak]] ulisababisha tena janga la kipindupindu.<ref>{{cite news |first= |last= |authorlink= |author= |coauthors= |title=U.N. reports cholera outbreak in northern Iraq |url=http://www.cnn.com/2007/WORLD/meast/08/29/iraq.cholera/index.html |work= |publisher=CNN |id= |pages= |page= |date= |accessdate=2007-08-30 |quote= }}</ref> Watu 22 walifariki.<ref>[http://www.guardian.co.uk/world/2007/dec/02/iraq.davidsmith Cholera crisis hits Baghdad], The Observer, 2 Desemba 2007.</ref>


Mnamo Agosti [[2007]] jimboni [[Orissa]], [[India]], zaidi ya watu 2,000 walilazwa hospitalini.<ref>[http://news.bbc.co.uk/2/hi/south_asia/6968281.stm Cholera death toll in India rises], BBC News.</ref>
Mnamo Agosti [[2007]] jimboni [[Orissa]], [[India]], zaidi ya watu 2,000 walilazwa [[Hospitali|hospitalini]].<ref>[http://news.bbc.co.uk/2/hi/south_asia/6968281.stm Cholera death toll in India rises], BBC News.</ref>


Machi - Aprili [[2008]]: watu 2,490 walilazwa hospitalini nchini [[Vietnam]] kutokana na janga la kipindupindu.<ref>[http://www.who.int/cholera/countries/VietNamCountryProfile2008.pdf Cholera Country Profile: Vietnam]. WHO.</ref>
Machi - Aprili [[2008]]: watu 2,490 walilazwa hospitalini nchini [[Vietnam]] kutokana na janga la kipindupindu.<ref>[http://www.who.int/cholera/countries/VietNamCountryProfile2008.pdf Cholera Country Profile: Vietnam]. WHO.</ref>
Mstari 101: Mstari 107:
*[http://kenya.thebeehive.org/sw/content/124/965 Maelezo ya kipindupindu na namna za kujikinga kwenye beehive.com (swa.)]
*[http://kenya.thebeehive.org/sw/content/124/965 Maelezo ya kipindupindu na namna za kujikinga kwenye beehive.com (swa.)]


[[Jamii:Biolojia]]
[[Jamii:Bakteria]]
[[Jamii:Maradhi ya kuambukiza]]
[[Jamii:Maradhi ya kuambukiza]]
[[Jamii:Translators without Borders]]

Pitio la 14:07, 21 Agosti 2016

Kipindupindu (kwa Kilatini na Kiingereza cholera kutoka neno la Kigiriki χολέρα, kholera, lililotokana na χολή, kholē, nyongo) ni ugonjwa hatari unaosababishwa na bakteria hasa katika utumbo mwembamba. Bakteria hizo ambazo huitwa vibriocholerae huweza kusababisha kuhara sana na kutapika sana pamoja na homa kali.

Maambukizi hutokea hasa kupitia maji au vyakula vilivyochafuliwa na wadudu kama vile nzi. Wadudu hao huweza kuchafua vyakula endapo vyakula hivyo vitaachwa wazi bila kufunikwa na chombo chochote na kuvutia nzi hao kutua juu ya vyakula hivyo na kuacha bakteria zitakazosababisha ugonjwa wa kipindupindu kwa mtu atakayekula chakula kile.

Kiwango cha kuhara na kutapika kinaleta upungufu wa maji na uwiano wa chumvi mwilini. Baada ya dalili hizo kutokea kuna hatari ya kifo kwa asilimia 20 - 70 ya wagonjwa kama hawana tiba.

Tunaweza kujilinda na kipindupindu endapo tukajilinda na vitu vifuatavyo ambavyo ni kunywa maji safi na salama na kula chakula kisichopoa. Bila kusahau kusafisha maeneo yote yanayomzunguka kiumbe hai, hasa binadamu. Yatupasa kufanya usafi katika mikoa yetu yote, hasa majijini ambako kunashutumiwa sana kuwa machafu.

Bakteria wa Vibrio cholerae

[1][2]

Kutokea kwa kipindupindu duniani. Nyekundu: kinatokea mara kwa mara; Njano: kinatokea mara kadhaa; Nyeupe: kinatokea mara chache.

Ambukizo

Kipindupindu husababishwa na bakteria aina ya Vibrio cholerae zinazosababisha kuhara majimaji yenye rangi kama maji ya kupikia mchele. Bakteria hiyo ilitambuliwa mwaka 1854 na Filippo Pacini.

Robert Koch alifaulu mwaka 1883 kufuga bakteria kutokana na utumbo wa watu waliokufa kwa kipindupindu huko Misri.

Kipindupindu hutokea hasa katika nchi pasipo maji safi, hasa ambako maji ya kunywa na majimaji ya choo yanaweza kuchanganyikana. Bakteria ya vibrio cholerae hupatikana hasa katika mavi na maji ya choo na pia katika maji ya bahari, maziwa na mito kama maji machafu huingizwa katika magimba ya maji bila kusafishwa kwanza.

Vilevile samaki na vyakula vingine kutoka maji yenye bakteria vinachafuliwa na vinaweza kusababisha ambukizo. Vilevile vyakula vinavyooshwa kwa maji yaliyochafuliwa na bakteria ya kipindupindu.

Katika mazingira yenye maji ya bomba, yaliyopitia karakana ya kusafisha maji machafu, kipindupindu hutokea mara chache tu. Kujulikana kwa njia za kuambukizwa kulikuwa sababu ya kuanzishwa na kugharamiwa kwa teknolojia hizo katika nchi nyingi.

Matibabu

Hospitali mjini Dhaka inayoonyesha vitanda vya wanaougua ugonjwa wa kipindupindu

1. Mgonjwa hunyweshwa maji mengi, kwa sababu mwili wake hupoteza maji mengi anapougua maradhi haya.

2. Dawa zinazojulikana kufanya kazi ni kama cotrimoxazole, erythromycin, doxycycline, chloramphenicol, na furazolidone.[3] 3. Chanjo za kuzuia Kipindipindu hutolewa katika baadhi za nchi.[4]

Kuepukana na Kipindupindu

Kinga ni kama ifuatavyo:

  • wakati wowote kunawa mikono kabla ya kutayarisha au kula chakula, kusafisha vyombo kama sahani, vikombe n.k.
  • kunawa mikono kabisa kwa sabuni – kiganja, upande wa nyuma wa mkono, katikati ya vidole na kucha kwa sekunde. Baada ya haja na kabla ya kula.
  • kuwa na akiba ya maji yaliyochemshwa pasipo na maji safi ya bomba
  • kupika chakula vizuri maana halijoto juu ya 75 °C (hadi 85 mlimani) inaua bakteria;
  • kumenya matunda yote
  • kufunika chakula maana nzi wanapitisha bakteria kwa miguu yao
  • maji ya choo yanayotokamana na wagonjwa wa kipindupindu yanapasa kupitia mashimo ya choo yaliyohifadhiwa vizuri ili kuzuia usambazaji wa bakteria
  • vifaa vyote vinavyotumiwa na wagonjwa vinapaswa kuchemshwa kwa maji ya moto
  • mikono inayoshika wagonjwa au nguo zao inapaswa kunaniwa kwa sabuni
  • mashimo ya choo yanapaswa kutiwa dawa za kuua bakteria kwa kutumia klorini
  • Tumia maji yaliyotibiwa pekee hasa ikiwa ya kunywa; yachemshe au utie matone 5 ya klorini kwa kila galoni 1 au utumie dawa ya kutakasa maji. Yaache maji yatulie kwa dakika 30 kabla ya kunywa.
  • Tumia choo kila mara – usiende haja karibu au ndani ya chanzo cha maji.

Historia

Mnamo miaka 1816-1826 kulikuwa na janga la kwanza la kipindupindu mkoani Bengal, nchini India. Waingereza 10,000 na Wahindi walikufa.[5]

Janga la pili la kipindupindu lilikuwa mnamo 1829-1851 kilipoenea nchini Urusi, Hungaria, Ujerumani na Uingereza. Zaidi ya watu 55,000 walikufa katika Uingereza pekee.[6] Mwaka 1831, watu 150,000 walikufa kutokana na janga hili nchini Misri.[7]

Mwaka 1849, kipindupindu kilizuka tena kwa mara ya pili mjini Paris.[8] Mjini London watu 14,137 walikufa.

Miaka ya 1961-1970: kulikuwa na janga lingine la kipindupindu nchini Indonesia. Ilianzia Afrika Kaskazini na kuenea hadi nchi ya Italia. Katika miaka ya 1970, watu waliathirika kidogo nchini Ujapani.

Mnamo 1991-1994 kulikuwa na janga lingine huko Amerika Kusini, lililosababishwa na meli iliyomwaga maji machafu. Nchini Peru watu takriban 10,000 waliuawa.

Mwaka 2000, wagonjwa 14,000 waliripotiwa kuugua kipindupindu. Takriban 87% waliripotiwa kutoka bara la Afrika.[9]

Julai - Desemba 2007: ukame wa maji salama kwa ajili ya kunywa nchini Irak ulisababisha tena janga la kipindupindu.[10] Watu 22 walifariki.[11]

Mnamo Agosti 2007 jimboni Orissa, India, zaidi ya watu 2,000 walilazwa hospitalini.[12]

Machi - Aprili 2008: watu 2,490 walilazwa hospitalini nchini Vietnam kutokana na janga la kipindupindu.[13]

Waathirika maarufu

Tanbihi

  1. Ryan KJ, Ray CG (editors) (2004). Sherris Medical Microbiology (toleo la 4th). McGraw Hill. ku. 376–7. ISBN 0838585299. 
  2. Faruque SM; Nair GB (editors) (2008). Vibrio cholerae: Genomics and molecular biology. Caister Academic Press. ISBN 978-1-904455-33-2. 
  3. "Cholera treatment". Molson Medical Informatics. 2007. Iliwekwa mnamo 2008-01-03. 
  4. "Is a vaccine available to prevent cholera?". CDC disease info: Cholera. Iliwekwa mnamo 2008-07-23. 
  5. The 1832 Cholera Epidemic in New York State, By G. William Beardslee.
  6. Asiatic Cholera Pandemic of 1826-37.
  7. Cholera Epidemic in Egypt (1947).
  8. The Irish Famine.
  9. Disease fact sheet: Cholera. IRC International Water and Sanitation Centre.
  10. "U.N. reports cholera outbreak in northern Iraq", CNN. Retrieved on 2007-08-30. 
  11. Cholera crisis hits Baghdad, The Observer, 2 Desemba 2007.
  12. Cholera death toll in India rises, BBC News.
  13. Cholera Country Profile: Vietnam. WHO.

Viungo vya nje