Manispaa : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
+wilaya mpya 2, Ubungo na Kigamboni
d Muddyb alihamisha ukurasa wa Manisipaa hadi Manispaa: Typo shida!
(Hakuna tofauti)

Pitio la 11:50, 14 Agosti 2016

Manispaa (ing. municipality) ni mji mwenye kiwango fulani ya kujitawala katika shughuli zake.

Madaraka haya ni pamoja na haki ya kutawaliwa na serikali ya kimahali iliyochaguliwa na watu wa manisipaa (badala ya kusimamiwa na mwakilishi wa serikali kuu), kuamulia na kukusanya kodi fulani katika eneo la manisipaa na kupanga makisio yake yenyewe.

Manispaa za Tanzania

Nchini Tanzania manispaa ni mji mwenye wakazi zaidi ya 100,000 hadi 500,000.

Katika muundo wa utawala manispaa za Tanzania zinahesabiwa kama wilaya. Serikali ya manisipaa huitwa Halmashauri ya manispaa (Municipal Council).

Manisipaa za Tanzania ni Bukoba , Dodoma , Iringa , Kigoma , Lindi , Morogoro , Moshi , Mtwara , Musoma , Shinyanga , Singida , Songea , Sumbawanga , Tabora .

Halafu kuna masisipaa tano ambazo ni sehemu ya majiji mawili.