Ufalme wa Kikatiba : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d Roboti: Imeondoa: fi:Monarkia (strongly connected to sw:Ufalme)
Tags: Mobile edit Mobile web edit
Mstari 11: Mstari 11:
==Mfalme kama kiongozi mkuu chini ya katiba==
==Mfalme kama kiongozi mkuu chini ya katiba==
Katika nchi kadhaa nafasi ya mfalme inafanana na maraisi watendaji. Kwa mfano katika nchi kama Moroko au Yordani mfalme anaamua kama bunge linavunjwa au la na kumteua kiogozi wa serikali kwa hiari yake.
Katika nchi kadhaa nafasi ya mfalme inafanana na maraisi watendaji. Kwa mfano katika nchi kama Moroko au Yordani mfalme anaamua kama bunge linavunjwa au la na kumteua kiongozi wa serikali kwa hiari yake.





Pitio la 22:42, 13 Agosti 2016

Ufalme wa kikatiba ambako mfalme ni kiongozi wa heshima tu yanaonyeshwa kwa rangi nyekundu. Rangi ya dhambarau inaonyesha nchi ambako mfalme ana athira kubwa chini ya katiba. Nchi ya Uthai ina mfalme na katiba lakini katiba imepumzishwa kwa sasa na serikaliy a kijeshi (2006/2007).

Ufalme wa Kikatiba ni muundo wa serikali ambako kaisari, sultani, mfalme, malkia au mtemi ni mkuu wa nchi chini ya katiba yake. Hii inamaanisha ya kwamba madaraka ya mfalme yana mipaka yao katika masharti za katiba na sheria za nchi. Pale ambako hakuna katiba ya kimaandishi inayoratibu mambo mengi kuna kawaida inayoweka mipaka kwa madaraka ya mfalme jinsi ilivyo Uingereza.

Madaraka ya mfalme katika muundo huu yanatofautiana sana.

Zamani wafalme walikuwa mara nyingi viongozi wenye madaraka yote wasiobanwa na bunge au sheria. Aina hii ya ufalme umebaki mahali pachache tu kwa mfano Saudia.

Mfalme kama kiongozi wa heshima

Katika nchi kama Uingereza au Uswidi shughuli zote za serikali zinaendeshwa kwa jina la mfalme lakini mamlaka yapo mkononi mwa serikali inayochaguliwa na bunge ambalo limetoke katika kura ya wananchi wote. Hapo mfalme hana athira kubwa katika siasa. Nafasi yake iko hasa pale ambako vikundi vikundi ndani ya bunge havikubaliani kuhusu serikali mpya na hakuna upande mwenye kura nyingi kabisa. Hapo ni mfalme anayemteua mwanasiasa atakayejaribu kukusanya kura za kutosha kwa ajili ya serikali mpya. Kama chama fulani kina wabunge wa kutosha kitamtaja kiongozi wake na mfalme hana cha kufanya ila tu kumpa huyu wito wa kuunda serikali.

Mfalme kama kiongozi mkuu chini ya katiba

Katika nchi kadhaa nafasi ya mfalme inafanana na maraisi watendaji. Kwa mfano katika nchi kama Moroko au Yordani mfalme anaamua kama bunge linavunjwa au la na kumteua kiongozi wa serikali kwa hiari yake.