Izazi : Tofauti kati ya masahihisho
d
→top: wa wa --> wa; new lines; double spaces using AWB
d (Bot: Replacements: fix URL prefix) |
|||
'''Izazi ''' ni jina la kata ya [[Wilaya ya Iringa Vijijini]] katika [[Mkoa wa Iringa]], [[Tanzania]].
Kwa sasa imebaki na vijiji vitatu tu, yaani Izazi, [[Makuka]] na [[Mnadani]], vyote vikiwa katika [[Bonde la Ufa]] kwenye [[bwawa la Mtera]] (ambalo likijaa kabisa liko katika [[mita]] 698.5 juu ya [[usawa wa bahari]]). Ni sehemu ya chini zaidi katika [[Nyanda za Juu]] Kusini mwa Tanzania.
Eneo ni kubwa sana na lenye [[rutuba]] lakini watu ni wachache hasa kutokana na uhaba wa [[mvua]] ambayo kwa kawaida inaishia [[milimita]] 300 kwa mwaka. Kwa sababu hiyohiyo [[kilimo]] kikuu ni cha [[mtama]].
Muhimu zaidi kiuchumi ni [[ufugaji]]: utovu wa [[ndorobo]] ulivutia kwanza [[Wasagara]] kutoka wilaya ya [[Kilosa]] (mwisho wa [[karne XIX]]), halafu [[Wamasai]] kutoka [[Mkoa wa Arusha]] (mwanzo wa [[karne XX]]). Ni vigumu kusema kama [[Wahehe]], watawala wa eneo hilo, walikuwa wanaishi huko kabla ya wote, au walihamia pamoja na Wasagara. Baada yao [[Wagogo]] wengi walihamia kutoka [[Mkoa wa Dodoma]]. Ndiyo makabila manne yaliyochangia zaidi mwanzo wa makazi.
|