Orodha ya Messier : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d robot Adding: ca:Catàleg Messier
Mstari 17: Mstari 17:
[[da:Messiers katalog]]
[[da:Messiers katalog]]
[[de:Messier-Katalog]]
[[de:Messier-Katalog]]
[[el:Αντικείμενο Μεσιέ]]
[[en:Messier object]]
[[en:Messier object]]
[[eo:Messier-katalogo]]
[[eo:Messier-katalogo]]

Pitio la 00:03, 12 Desemba 2007

Faili:Messier.all.750pix.jpg
Picha za nebula, nyota na galaksi zote za orodha ya Messier kuanzia M1 hadi M110

Orodha ya Messier ni orodha ya nyota iliyoandikwa na mwanafalaki Mfaransa Charles Messier kati ya 1764 na 1782.

Messier alitafuta hasa nyotamkia angani akitumia darubini. Aliona pia magimba mengine yaliyoonekana kama nebula (wingu dogo linalogn'aa) zisizotembea angani kwa hiyo hazikuwa nyotamkia. Akaamua kuziorodhesha.

Orodha hii ilikuwa orodha ya kwanza iliyokubaliwa na wanafalaki wengi kimataifa. Nyota na nebula zake zilijulikana kufuatana na namba jinsi zilivyoandikwa katika orodha ya Messier yaani M1, M2 na kadhalika. M1 ni nebula ya kaa, M45 ni fungunyota ya kilimia na galaksi ya Andromeda ni M31.

Kuna namba 110 katika orodha hii.

Orodha za nyota za kisasa zinaonyesha nyota malakhi lakini namba za Messier zinaendelea kutumiwa hadi leo kwa vitu vinavyoorodhesha kwake.