Ruaha Mkuu : Tofauti kati ya masahihisho
d Bot: Migrating 1 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q1861088 (translate me) |
No edit summary |
||
Mstari 17: | Mstari 17: | ||
*Ecohydrology of Great Ruaha River: www.iwmi.cgiar.org/Africa/files/RIPARWIN/05/_downloads/Fact-Factsheet_EcoHyd_GRR.doc |
*Ecohydrology of Great Ruaha River: www.iwmi.cgiar.org/Africa/files/RIPARWIN/05/_downloads/Fact-Factsheet_EcoHyd_GRR.doc |
||
{{Mito ya Tanzania}} |
|||
[[Jamii:Mito ya Tanzania]] |
[[Jamii:Mito ya Tanzania]] |
Pitio la 15:48, 22 Mei 2016
Ruaha Mkuu (pia: Ruaha Mkubwa) ni mto muhimu nchini Tanzania na tawimto wa Rufiji. Huitwa "Ruaha Mkuu" kwa kuutofautisha na "Ruaha Mdogo" unaoishia ndani yake si mbali na Iringa mjini.
Chanzo na mwendo wa mto
Chanzo chake ni mito mingi midogo inayotelemka milima za nyanda za juu za kusini Tanzania hasa safu za milima ya Uporoto na Kipengere. Mito hii inakusanya maji yao kwenye tambarare ya Usangu na Ruaha inaanza hapa. Mito mikubwa zaidi inayojiunga hapa na Ruaha ni pamoja na mto Mbarali, mto Kimani na mto Chimala.
Karibu na Ng’iriama mto unatoka katika Usangu na kuingia hifadhi ya kitaifa ya Ruaha. Inaendelea kupokea Ruaha Mdogo na mto Kisigo kabla ya kuingia katika ziwa la lambo la Mtera halafu inaendelea hadi ziwa la lambo la Kidatu.
Baada ya Kidatu Ruaha Mkuu unapita tambarare ya Kilombero hadi kuishia katika mto Rufiji.
Matatizo ya ekolojia ya mto
Maji ya Ruaha Mkuu ni muhimu kwa ekolojia ya beseni yake pamoja na watu wote wanaoishi hapa. Lakini matumizi ya kibinadamu yameleta mvurugo kwa ekolojia ya mto na tangu 1993 mto umeanza kukauka wakati wa ukame. Uhaba wa maji yamesababishwa na matumizi mabaya ya maji upande wa miradi mikubwa ya mpunga katika Usangu.
Viungo vya Nje
- Ecohydrology of Great Ruaha River: www.iwmi.cgiar.org/Africa/files/RIPARWIN/05/_downloads/Fact-Factsheet_EcoHyd_GRR.doc