Periheli : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|300px|1. Sayari kwenye afeli yake 2. Sayari kwenye periheli yake 3. Jua '''Periheli''' (ing. ''perihelion'') ni mahali ka...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 19:42, 6 Mei 2016

1. Sayari kwenye afeli yake 2. Sayari kwenye periheli yake 3. Jua

Periheli (ing. perihelion) ni mahali katika obiti ya sayari au magimba mengine ya angani ambako ni karibu zaidi na jua. Jina latokana na kigiriki Περι na Ήλιο peri (karibu) na "helio" (jua).

Kinyume chake ni afeli inayomaanisha sehemu ya obiti iliyo mbali kabisa na jua.

Majina haya hutumiwa kama obiti ina umbo la duaradufu, yasingekuwa na maana kama obiti ingekuwa duara kamili lakini hii haitokei hali halisi.