Fasihi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
dNo edit summary
No edit summary
Mstari 1: Mstari 1:
'''Fasihi''' ni utanzu (tawi) wa sanaa ambao hutumia lugha ya mazungumzo au maandishi ili kufikisha (kuwasilisha) ujumbe kwa hadhira husika.katika kazi yoyote ya fasihi ni lazima pawepo na ustadi wenye kuleta mvuto fulani kwa hadhira (wasikilizaji au wasomaji) husika. Ustadi (ufundi)huo unaovutia hadhira huitwa FANI, ambayo hujumuisha mambo kama vile:
'''Fasihi''' (kutoka [[neno]] la [[Kiarabu]]) ni [[utanzu]] ([[tawi]]) wa [[sanaa]] ambao hutumia [[lugha]] ya mazungumzo au maandishi ili kufikisha (kuwasilisha) ujumbe kwa hadhira husika.
Katika kazi yoyote ya fasihi ni lazima pawepo na ustadi wenye kuleta mvuto fulani kwa hadhira (wasikilizaji au wasomaji) husika. Ustadi (ufundi) huo unaovutia hadhira huitwa FANI, ambayo hujumuisha mambo kama vile:
*Muundo
*Muundo
*Mtindo
*Mtindo
Mstari 13: Mstari 15:

Vilevile kazi yoyote ya fasihi huwa na ujumbe na malengo mbalimbali ambayo hukusudiwa yaifikie jamii husika. Yale yote ambayo msanii wa kazi ya fasihi anakusudia yaifikie jamii husika huitwa MAUDHUI. Maudhui ya kazi ya fasihi hujumuisha:

*Dhamira
*Dhamira
*Ujumbe
*Ujumbe
Mstari 19: Mstari 20:
*Falsafa/misimamo na
*Falsafa/misimamo na
*Mtazamo
*Mtazamo

==Sifa za fasihi==
==Sifa za fasihi==
*Fasihi ni utanzu wa sanaa
*Fasihi ni utanzu wa sanaa
Mstari 24: Mstari 26:
*Fasihi ni maelezo ya FANI na MAUDHUI.
*Fasihi ni maelezo ya FANI na MAUDHUI.
*Fasihi ni ufundi unaotumia lugha ili kulete mguso au hisia fulani za watu katika muktadha fulani.
*Fasihi ni ufundi unaotumia lugha ili kulete mguso au hisia fulani za watu katika muktadha fulani.

==Aina za fasihi==
==Aina za fasihi==
Kuna aina kuu mbili za fasihi nazo ni:
Kuna aina kuu mbili za fasihi nazo ni:

*[[Fasihi simulizi]] - huwasilishwa kwa lugha ya mazungumzo/masumilizi
*[[Fasihi simulizi]] - huwasilishwa kwa lugha ya mazungumzo/masumilizi
*[[Fasihi andishi]] - huwasilishwa kwa lugha ya maandishi
*[[Fasihi andishi]] - huwasilishwa kwa lugha ya maandishi
Mstari 33: Mstari 35:
**Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya lugha ya mazungumzo au masimulizi ya mdomo
**Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya lugha ya mazungumzo au masimulizi ya mdomo
**Fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya lugha ya maandishi
**Fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya lugha ya maandishi

==Kufanana kwa fasihi simulizi na fasihi andishi==
==Kufanana kwa fasihi simulizi na fasihi andishi==
Kimsingi fasihi ni moja ingawa imegawanyika katika sehemu kuu mbili, yaani, fasihi simulizi na fasihi andishi. Mbali na mgawanyiko huo kuna mambo ambayo yanafanana katika fasihi zote mbili. Mambo hayo ni pamoja na:

Mstari 40: Mstari 43:
*Zote zina wahusika ambao ni Fanani na Hadhira
*Zote zina wahusika ambao ni Fanani na Hadhira
*Zote zina vipengele vya Fani na Maudhui
*Zote zina vipengele vya Fani na Maudhui

==Tofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi==
==Tofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi==
{| class="wikitable"
{| class="wikitable"
Mstari 72: Mstari 76:
|}
|}
==Viungo vya Nje==
==Viungo vya nje==
*[http://chomboz.blogspot.co.uk/p/fasihi_4.html blogu ya Eric Ndumbaro kuhusu Fasiki simulizi ya Kiafrika]
*[http://chomboz.blogspot.co.uk/p/fasihi_4.html blogu ya Eric Ndumbaro kuhusu Fasiki simulizi ya Kiafrika]

{{mbegu-lugha}}

[[Category:Fasihi]]
[[Category:Fasihi]]
[[Jamii:Sanaa]]

Pitio la 08:44, 27 Machi 2016

Fasihi (kutoka neno la Kiarabu) ni utanzu (tawi) wa sanaa ambao hutumia lugha ya mazungumzo au maandishi ili kufikisha (kuwasilisha) ujumbe kwa hadhira husika.

Katika kazi yoyote ya fasihi ni lazima pawepo na ustadi wenye kuleta mvuto fulani kwa hadhira (wasikilizaji au wasomaji) husika. Ustadi (ufundi) huo unaovutia hadhira huitwa FANI, ambayo hujumuisha mambo kama vile:

  • Muundo
  • Mtindo
  • Wahusika
  • Matumizi ya lugha na,
  • Mandhari
    • Muundo - mtitiriko/msuko/mpangilio wa matukio / visa
    • Mtindo - ni mbinu inayotumiwa na fanani ili atofautiane na fanani mwingine
    • Wahusika - ni watu au vitu vyenye uhai au la ambavyo hutumiwa na fanani katika kazi yake
    • Mandhari - ni eneo ambalo fanani hulitumia kujenga matukio na au mtiriko katika kuumba kazi yake
    • Matumizi ya lugha - lugha anayotumia fanani katika kujenga wasifu wa wahusika kihaiba kazi yake

Vilevile kazi yoyote ya fasihi huwa na ujumbe na malengo mbalimbali ambayo hukusudiwa yaifikie jamii husika. Yale yote ambayo msanii wa kazi ya fasihi anakusudia yaifikie jamii husika huitwa MAUDHUI. Maudhui ya kazi ya fasihi hujumuisha:

  • Dhamira
  • Ujumbe
  • Migogoro
  • Falsafa/misimamo na
  • Mtazamo

Sifa za fasihi

  • Fasihi ni utanzu wa sanaa
  • Kazi ya fasihi ni kujaribu kusawiri vipengele vya maisha, mahusiano, na hisia za watu katika jamii husika.
  • Fasihi ni maelezo ya FANI na MAUDHUI.
  • Fasihi ni ufundi unaotumia lugha ili kulete mguso au hisia fulani za watu katika muktadha fulani.

Aina za fasihi

Kuna aina kuu mbili za fasihi nazo ni:

Fasihi hizi zina dhima sawa katika jamii ingawa ni tofauti. Utofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi hujitokeza katika uwasilishwa wake katika jamii husika.

    • Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya lugha ya mazungumzo au masimulizi ya mdomo
    • Fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya lugha ya maandishi

Kufanana kwa fasihi simulizi na fasihi andishi

Kimsingi fasihi ni moja ingawa imegawanyika katika sehemu kuu mbili, yaani, fasihi simulizi na fasihi andishi. Mbali na mgawanyiko huo kuna mambo ambayo yanafanana katika fasihi zote mbili. Mambo hayo ni pamoja na:

  • Zote hutumia ufundi wa lugha ili kuwasilisha ujumbe kwa hadhira husika
  • Zote zina dhima inayofanana katika jamii, yaani, kuelimisha na kuburudisha jamii
  • Zote zina wahusika ambao ni Fanani na Hadhira
  • Zote zina vipengele vya Fani na Maudhui

Tofauti kati ya fasihi simulizi na fasihi andishi

Na. Kipengele Fasihi simulizi Fasihi andishi
1 Uwasilishwaji Fasihi simulizi huwasilishwa kwa njia ya masimulizi ya mdomo pamoja na vitendo Fasihi andishi huwasilishwa kwa njia ya maandishi bila vitendo
2 Umri Fasihi simulizi ni kongwe kuliko fasihi andishi Fasihi andishi ni changa kuliko fasihi simulizi
3 Umilikaji Fasihi simulizi humilikiwa na jamii nzima, ni mali ya jamii Fasihi andishi humilikiwa na mwandishi, ni mali ya mwandishi
4 Tanzu Fasihi simulizi ina tanzu nyingi kuliko fasihi andishi Fasihi andishi ina tanzu chache kuliko fasihi simulizi
5 Hadhira Hadhira ya fasihi simulizi ni watu wote katika jamii Hadhira ya fasihi andishi ni wale tu wanaojua kusoma na kuandika
6 Mabadiliko Fasihi simulizi hubadilika haraka kutegemeana na mahitaji ya hadhira na wakati Fasihi andishi haibadiliki haraka kutegemeana na mahitaji ya hadhira na wakati
7 Utunzi Fasihi simulizi hutungwa kwa muda mfupi Fasihi andishi hutungwa kwa muda mrefu
8 Mazingira ya uwasilishaji wake (mandhari) Huambatana na tukio maalumu la jamii Kusoma au kusomewa ni ya kufikirika au mahali popote
9 Marekebisho Mtunzi/msimulizi anaweza kurekebisha kazi yake wakati wa kuwasilisha au baadaye kidogo Kitabu kikishaandikwa ni vigumu kukifanyia marekebisho mpaka toleo jipya litakapoandikwa
10 Uhifadhi Huhidhiwa kwa njia ya kichwa (kichwani) kwa sehemu kubwa na sehemu ndogo sana huhifadhiwa kwenye maandishi, vinasa sauti au kanda mbalimbali za kurekodi Huhifadhiwa kwa njia ya maandishi (vitabu)
11 Gharama Fasihi andishi ina gharama ndogo ukilinganisha na fasihi andishi Fasihi andishi ina gharama kubwa ukilinganisha na fasihi simulizi
12 Wahusika Fasihi simulizi mara nyingi hutumia wahusika wa kubuni wasi binadamu Fasihi andishi hutumia wahusika wa kubuni ambao mara nyingi ni binadamu
13 Uhai Fasihi simulizi ni hai kuliko fasihi andishi Fasihia andishi si hai kuliko fasihi simulizi

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Fasihi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.