Yosefu Oriol : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '[[image:Statue of Saint Joseph Oriol - Santa Maria del Mar - Barcelona 2014.jpg|thumb|right|250px|Sanamu ya Mt. Josep Oriol - [[Basilica de Santa Maria del Mar]...'
(Hakuna tofauti)

Pitio la 14:41, 7 Machi 2016

Sanamu ya Mt. Josep Oriol - Basilica de Santa Maria del Mar, Barcelona, Hispania.
Kaburi la Mt. Yosefu Oriol.

Yosefu Oriol (kwa Kikatalunya Sant Josep Oriol; kwa Kihispania José Orioli) (Barcelona, 23 Novemba 1650 – Barcelona 23 Machi 1702) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mwanachama wa Utawa wa Tatu wa Mt. Fransisko nchini Hispania.

Tangu wakati wa uhai wake amejulikana kama "Mtendamiujiza wa Barcelona"

Papa Pius VII alimtangaza mwenye heri tarehe 5 Septemba 1806, halafu Papa Pius X alimfanya mtakatifu tarehe 20 Mei 1909.

Maisha

Mzaliwa wa Barcelona, alisoma katika chuo kikuu cha mji huo, akapata udaktari wa teolojia tarehe 1 Agosti 1674.

Alipewa upadrisho tarehe 30 Mei 1676.

Alitembelea Roma mwaka 1686 akapewa cheo katika kanisa la Santa Maria del Pi mjini Barcelona, ambapo amezikwa.

Akitamani kuwa mfiadini, alisafiri kwenda Roma mnamo Aprili 1698 ili ajitolee kwenda umisionari, lakini akaugua huko Marseille akarudi Barcelona.

Alisemekana kuwa na karama za unabii na uponyaji wa mara moja.

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.