Ekaristi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d →‎Katika mpangilio wa sakramenti saba: All info is kept in Wikidata, removed: {{Link FA|hu}} using AWB (10903)
No edit summary
Mstari 1: Mstari 1:
[[Picha:01preparation4.jpg|thumb|200 px|right|Vipaji vya [[mkate]] na [[divai]] vilivyoandaliwa kwa [[adhimisho]] la ekaristi.]]
{{Sakramenti}}
{{Ukristo}}
Kwa [[Ukristo|Wakristo]] '''Ekaristi''' ni [[sakramenti]] iliyowekwa na [[Yesu Kristo]] wakati wa [[karamu ya mwisho]] usiku wa kuamkia [[Ijumaa Kuu]], siku ya mateso na kifo chake.
Kwa [[Ukristo|Wakristo]] '''Ekaristi''' ni [[sakramenti]] iliyowekwa na [[Yesu Kristo]] wakati wa [[karamu ya mwisho]] usiku wa kuamkia [[Ijumaa Kuu]], siku ya mateso na kifo chake.

== Jina ==
== Jina ==
[[Picha:01preparation4.jpg|thumb|200 px|right|Vipaji vya [[mkate]] na [[divai]] vilivyoandaliwa kwa [[adhimisho]] la ekaristi.]]

Jina linatokana na neno la lugha ya [[Kigiriki]] εὐχαρίστω (''eukharisto'': nashukuru) lililotumiwa na [[Mtume Paulo]] na [[Wainjili]] katika kusimulia karamu hiyo ya mwisho ya [[Yesu]] na [[Mitume wa Yesu|Mitume]] wake, na muujiza uliotangulia ambao Yesu alidokeza nia yake ya kushibisha [[binadamu]] wote, yaani ule wa kuzidisha mkate na samaki kwa ajili ya umati.

Mstari 12: Mstari 11:

== Mkate na divai ==
== Mkate na divai ==

Yesu alitumia mkate na divai kwa sababu vilikuwa vya maana sana katika utamaduni wake na katika Agano la Kale. Vilikuwa chakula cha kawaida na kinywaji cha karamu. “Divai imfurahishe mtu moyo wake... na mkate umburudishe mtu moyo wake” (Zab 104:15). Vilitokana na chembe za ngano na matunda ya mzabibu ambavyo Yesu alijifananisha navyo. “Amin, amin, nawaambia: Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi” (Yoh 12:24). “Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi; akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote” (Yoh 15:5). Baada ya kulimwa, vilihitaji kusagwa au kushinikizwa, matendo yanayodokeza tena mateso yake pamoja na kazi ya binadamu. Pia wingi wa chembe na wa zabibu zinazoungana ziwe mkate na divai unamaanisha umoja wa waamini ndani ya Kristo. Kwa hiyo ni lazima tutumie daima mkate na divai, si vitu vingine.

Mstari 22: Mstari 20:

== Ushuhuda wa [[Biblia]] ==
== Ushuhuda wa [[Biblia]] ==

[[Agano Jipya]] linasimulia mara nne matendo na maneno ya Yesu ambayo alianzisha ibada hiyo na kuwakabidhi Mitume wake.
[[Agano Jipya]] linasimulia mara nne matendo na maneno ya Yesu ambayo alianzisha ibada hiyo na kuwakabidhi Mitume wake.

Mstari 28: Mstari 25:

== Asili ==
== Asili ==

Kadiri ya ushuhuda huo, Yesu, katika karamu ya mwisho aliwagawia mitume wake mkate na divai akisema ndio mwili wake na damu yake vitakavyotolewa kama [[kafara]] kwa ondoleo la [[dhambi]] za umati, akawaagaiza wafanye vilevile kwa [[ukumbusho]] wake.

Mstari 36: Mstari 32:

== Maendeleo ==
== Maendeleo ==

[[Picha:BentoXVI-51-11052007.jpg|thumb|left|360px|[[Papa Benedikto XVI]] akiadhimisha ekaristi]]
[[Picha:BentoXVI-51-11052007.jpg|thumb|left|360px|[[Papa Benedikto XVI]] akiadhimisha ekaristi]]
Karne zilizofuata ibada ilizidi kubadilika, hasa ilipotenganishwa na mlo wa kawaida ulioendana nayo awali. Badala ya mlo huo, ibada iliunganishwa na masomo ya [[Neno la Mungu]].
Karne zilizofuata ibada ilizidi kubadilika, hasa ilipotenganishwa na mlo wa kawaida ulioendana nayo awali. Badala ya mlo huo, ibada iliunganishwa na masomo ya [[Neno la Mungu]].
Mstari 45: Mstari 40:

== Teolojia ==
== Teolojia ==

Ekaristi inahusiana sana na [[Pasaka]], na [[kifo]] na [[ufufuko]] wa [[Yesu]] vilivyotokea kwenye sikukuu hiyo ya [[Wayahudi]].
Ekaristi inahusiana sana na [[Pasaka]], na [[kifo]] na [[ufufuko]] wa [[Yesu]] vilivyotokea kwenye sikukuu hiyo ya [[Wayahudi]].

Mstari 59: Mstari 53:

Ekaristi inaitwa sakramenti ya upendo kwa sababu kila unapofanyika ukumbusho wa sadaka hiyo pekee waamini wanazidi kujifunza na kupokea upendo ambao siku hiyo Yesu “ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo” (Yoh 13:1). Hivyo tunawezeshwa kutekeleza amri mpya aliyotuachia pamoja na ekaristi. “Amri mpya nawapa: Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo” (Yoh 13:34). Ni sharti tujitoe kama Yesu, tukijiunga na sadaka yake katika ibada na katika maisha. “Katika hili tumelifahamu pendo: kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu. Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma yake, je, upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo? Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli” (1Yoh 3:16-18).

== Katika mpangilio wa sakramenti saba ==
== Katika mpangilio wa sakramenti saba ==
{{sakramenti}}
Katika imani ya [[Kanisa Katoliki]] na [[Waorthodoksi]] sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ekaristi, iliyo kuu kuliko sakramenti zote kwa sababu ndiyo Yesu mzima, Mungu-mtu, katika maumbo ya mkate na divai. Walioshiriki kifumbo kifo na ufufuko wake wakapokea kwake paji la Roho Mtakatifu, wanaalikwa kukaribia mara kwa mara meza anapowalisha na kuwanywesha Mwili na Damu yake ili washiriki uhai wake kwa dhati zaidi na zaidi. “Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi” (Yoh 6:56-57). Ubatizo na kipaimara havirudiwi, vinadumu ndani ya mtu kama mifupa ambayo ekaristi ya mara kwa mara inazidi kuitia mwili na damu.

{{mbegu-Ukristo}}

[[Jamii:Liturujia]]
[[Jamii:Liturujia]]

Pitio la 12:57, 2 Januari 2016

Vipaji vya mkate na divai vilivyoandaliwa kwa adhimisho la ekaristi.

Kwa Wakristo Ekaristi ni sakramenti iliyowekwa na Yesu Kristo wakati wa karamu ya mwisho usiku wa kuamkia Ijumaa Kuu, siku ya mateso na kifo chake.

Jina

Jina linatokana na neno la lugha ya Kigiriki εὐχαρίστω (eukharisto: nashukuru) lililotumiwa na Mtume Paulo na Wainjili katika kusimulia karamu hiyo ya mwisho ya Yesu na Mitume wake, na muujiza uliotangulia ambao Yesu alidokeza nia yake ya kushibisha binadamu wote, yaani ule wa kuzidisha mkate na samaki kwa ajili ya umati.

Jina linaonyesha mazingira ya sala ya matukio hayo, ambapo Yesu alimuelekea Mungu akimshukuru kwa vyakula na kinywaji alivyoshika mikononi kabla hajawagawia wanafunzi.

Shukrani ilikuwa msimamo wa msingi wa Yesu kwa Baba maisha yake yote, hasa alipofikia wakati wa kutolewa awe kafara ya wokovu wetu. “Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, ‘Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu’. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, ‘Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu’” (1Kor 11:23-25).

Mkate na divai

Yesu alitumia mkate na divai kwa sababu vilikuwa vya maana sana katika utamaduni wake na katika Agano la Kale. Vilikuwa chakula cha kawaida na kinywaji cha karamu. “Divai imfurahishe mtu moyo wake... na mkate umburudishe mtu moyo wake” (Zab 104:15). Vilitokana na chembe za ngano na matunda ya mzabibu ambavyo Yesu alijifananisha navyo. “Amin, amin, nawaambia: Chembe ya ngano isipoanguka katika nchi, ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi” (Yoh 12:24). “Mimi ni mzabibu, ninyi ni matawi; akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lolote” (Yoh 15:5). Baada ya kulimwa, vilihitaji kusagwa au kushinikizwa, matendo yanayodokeza tena mateso yake pamoja na kazi ya binadamu. Pia wingi wa chembe na wa zabibu zinazoungana ziwe mkate na divai unamaanisha umoja wa waamini ndani ya Kristo. Kwa hiyo ni lazima tutumie daima mkate na divai, si vitu vingine.

Mara nyingine Wakatoliki wanapokea umbo la mkate tu kwa lengo la kukwepa umwagaji wa Damu ya Kristo na kurahisisha ibada, hasa kama washiriki ni umati (hata milioni 4 katika misa moja). Yesu mwenyewe alizungumzia mkate kuliko divai, kwa sababu chakula ni muhimu kuliko kileo. “Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu” (Yoh 6:51). “Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sisi sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja” (1Kor 10:17). Anayekula umbo la mkate hapokei sehemu tu ya Yesu, bali anampokea mzima, Mwili, Damu, Roho na Umungu. Pamoja na hayo, daima ni lazima walau padri anywe umbo la divai.

“Melkizedeki mfalme wa Salemu alileta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu aliye juu sana” (Mwa 14:18), “amefananishwa na Mwana wa Mungu” (Eb 3:7). “Bwana wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana” (Isa 25:6). “Njoo, ule mkate wangu, ukanywe divai niliyoichanganya” (Mith 9:5-6). Yesu alishiriki karamu nyingi na katika mojawapo ndipo alipoanza miujiza yake kwa kugeuza mapipa ya maji kuwa divai bora. “Kila mtu kwanza huandaa divai iliyo njema; hata watu wakiisha kunywa sana ndipo huleta iliyo dhaifu; wewe umeiweka divai iliyo njema hata sasa” (Yoh 2:10). “Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa, nanyi mwasema, ‘Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki wao watoza ushuru na wenye dhambi” (Lk 7:34).

Hatimaye Yesu alitumia divai kuachia ishara ya damu yake ili wafuasi wake waweze kushiriki mateso yake. “Je, mwaweza kunywea kikombe nitakachonywea mimi?” (Math 20:22). Kisha kushiriki kila mwaka karamu ya Pasaka, ambapo wote walikunywa divai mara nne, safari ya mwisho alikamilisha miujiza yake kwa kuigeuza iwe damu yake. “‘Nimetamani sana kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu; kwa maana nawaambia ya kwamba siili tena hata itakapotimizwa katika ufalme wa Mungu’. Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, ‘Twaeni hiki, mgawanywe ninyi kwa ninyi; maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu utakapokuja’. Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, ‘Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu’. Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula, akisema, ‘Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu’” (Lk 22:15-20). “Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je, si ushirika wa damu ya Kristo?” (1Kor 10:16).

Ushuhuda wa Biblia

Agano Jipya linasimulia mara nne matendo na maneno ya Yesu ambayo alianzisha ibada hiyo na kuwakabidhi Mitume wake.

Simulizi la zamani zaidi ni lile la 1Kor 11:23-25. Likafuata lile la Mk 14:22-24; halafu yale ya Math 26:26-28 na Lk 22:19-20.

Asili

Kadiri ya ushuhuda huo, Yesu, katika karamu ya mwisho aliwagawia mitume wake mkate na divai akisema ndio mwili wake na damu yake vitakavyotolewa kama kafara kwa ondoleo la dhambi za umati, akawaagaiza wafanye vilevile kwa ukumbusho wake.

Hivyo Kanisa tangu hapo, linaendeleza ibada hiyo maalumu na ya msingi katika mazingira mbalimbali.

Simulizi la Paulo linafanana na lile la Mwinjili Luka na kufuata jinsi ekaristi ilivyoadhimishwa kati ya Wakristo wa mataifa; kumbe Mwinjili Marko na Mwinjili Mathayo waliripoti adhimisho lilivyokuwa kati ya Wakristo wa Kiyahudi.

Maendeleo

Papa Benedikto XVI akiadhimisha ekaristi

Karne zilizofuata ibada ilizidi kubadilika, hasa ilipotenganishwa na mlo wa kawaida ulioendana nayo awali. Badala ya mlo huo, ibada iliunganishwa na masomo ya Neno la Mungu.

Ekaristi inaadhimishwa kwa mpangilio wa kupanda: waamini wanalishwa Neno la Mungu katika mimbari, halafu Mwili na Damu ya Kristo katika altare. Vilevile sehemu ya kwanza (liturujia ya Neno) inaleta masomo yakiwa na kilele katika Injili. Halafu katika sehemu ya pili (liturujia ya ekaristi) padri anafuata alichofanya Yesu katika karamu ya mwisho: anatwaa mkate na divai (kuandaa dhabihu zetu), anashukuru juu yake (sala kuu ya ekaristi inayogeuza dhabihu) na kuwapa waamini (komunyo, kilele cha yote, inayotugeuza ndani ya Kristo). Yesu mfufuka “aliwaeleza katika Maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe... Ikawa alipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa. Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua” (Lk 24:27,30-31). “Wakawa wakidumu katika fundisho la mitume, na katika ushirika, na katika kuumega mkate, na katika kusali” (Mdo 2:42). “Siku ya kwanza ya juma, tulipokuwa tumekutana ili kumega mkate, Paulo akawahutubu... akamega mkate, akala” (Mdo 20:7,11). Tusipofuata vizuri hatua za awali, hatutafaidika kweli na sakramenti: ndiyo sababu ni muhimu tuwahi ibada.

Kati ya namna mbalimbali za kuiadhimishwa, yalijitokeza mapokeo ya mashariki na ya magharibi. Kwa jumla mapokeo ya mashariki yanahusisha milango ya fahamu na ni ya fahari kuliko yale ya magharibi.

Teolojia

Ekaristi inahusiana sana na Pasaka, na kifo na ufufuko wa Yesu vilivyotokea kwenye sikukuu hiyo ya Wayahudi.

Kadiri ya Injili Yesu Kristo aliweka ekaristi wakati wa kuadhimisha karamu ya Pasaka ya Kiyahudi, akaipatia maana mpya kuhusiana na kifo na ufufuko wake.

Madhehebu mengi ya Kikristo yamekubali hati ya kiekumeni ya Lima (1982) inayosema "Ekaristi ni ukumbusho wa Yesu msulubiwa na mfufuka, yaani ishara hai na ya nguvu ya sadaka yake, ambayo ilitolewa mara moja tu msalabani na inaendelea kutenda kwa faida ya binadamu wote".

Wakatoliki na Waorthodoksi wanaamini kwamba katika karamu ya Bwana wanakula na kunywa Mwili wa Damu ya Kristo. Katika sala kuu ya ekaristi padri anaporudia maneno ya Yesu juu ya mkate na divai, Roho Mtakatifu anavigeuza kwa dhati: mkate si tena mkate, wala divai si tena divai, ingawa maumbo yanabaki yaleyale kwa hisi zetu. “Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli” (Yoh 6:54-55). “Basi kila aulaye mkate huo, au kukinywea kikombe hicho cha Bwana isivyostahili, atakuwa amejipatia hatia ya mwili na damu ya Bwana” (1Kor 11:27).

Baada ya mageuzo Yesu anabaki katika ekaristi moja kwa moja. Maumbo ya mkate na divai yanazidi kudokeza uwepo wake kama chakula na kinywaji chetu, hata kwa faida ya wagonjwa na wengineo wasiohudhuria. Ndiyo sababu tunazidi kumuabudu katika ekaristi, ingawa hatumuoni. “Tomaso alijibu, akamwambia, ‘Bwana wangu na Mungu wangu!’ Yesu akamwambia, ‘Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki” (Yoh 20:28-29).

Vilevile Wakatoliki na Waorthodoksi wanaamini ekaristi ni kafara ambayo Yesu alimtolea Baba msalabani na anaendelea kumtolea kwa wokovu wetu. “Yeye, kwa kuwa akaa milele, anao ukuhani wake usioondoka. Naye, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wamjiao Mungu kwa yeye; maana yu hai sikuzote ili awaombee... Kila kuhani mkuu huwekwa ili atoe vipawa na dhabihu; kwa hiyo lazima huyu naye awe na kitu cha kutoa” (Eb 7:24-25; 8:3). Katika ekaristi tunajiunga naye kwa kufanya ukumbusho wa kifo na ufufuko wake, tukimtolea tena Baba sadaka ya Mwili na Damu yake iliyolinganishwa na zile za Waisraeli na za Wapagani: “Waangalieni hao Waisraeli walivyokuwa kwa jinsi ya mwili; wale wazilao dhabihu, je, hawana shirika na madhabahu? Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu? Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani. Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani” (1Kor 10:18-21).

Ekaristi inaitwa sakramenti ya upendo kwa sababu kila unapofanyika ukumbusho wa sadaka hiyo pekee waamini wanazidi kujifunza na kupokea upendo ambao siku hiyo Yesu “ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo” (Yoh 13:1). Hivyo tunawezeshwa kutekeleza amri mpya aliyotuachia pamoja na ekaristi. “Amri mpya nawapa: Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo” (Yoh 13:34). Ni sharti tujitoe kama Yesu, tukijiunga na sadaka yake katika ibada na katika maisha. “Katika hili tumelifahamu pendo: kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu. Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma yake, je, upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo? Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli” (1Yoh 3:16-18).

Katika mpangilio wa sakramenti saba

Sakramenti za Wakatoliki na Waorthodoksi

Katika imani ya Kanisa Katoliki na Waorthodoksi sakramenti inayokamilisha ubatizo na kipaimara ni ekaristi, iliyo kuu kuliko sakramenti zote kwa sababu ndiyo Yesu mzima, Mungu-mtu, katika maumbo ya mkate na divai. Walioshiriki kifumbo kifo na ufufuko wake wakapokea kwake paji la Roho Mtakatifu, wanaalikwa kukaribia mara kwa mara meza anapowalisha na kuwanywesha Mwili na Damu yake ili washiriki uhai wake kwa dhati zaidi na zaidi. “Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi” (Yoh 6:56-57). Ubatizo na kipaimara havirudiwi, vinadumu ndani ya mtu kama mifupa ambayo ekaristi ya mara kwa mara inazidi kuitia mwili na damu.

Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ekaristi kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.