Uingereza : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d robot Adding: su:Inggris
d robot Adding: jv:Inggris
Mstari 154: Mstari 154:
[[it:Inghilterra]]
[[it:Inghilterra]]
[[ja:イングランド]]
[[ja:イングランド]]
[[jv:Inggris]]
[[ka:ინგლისი]]
[[ka:ინგლისი]]
[[ko:잉글랜드]]
[[ko:잉글랜드]]

Pitio la 05:23, 5 Desemba 2007

England
English Flag English Coat of Arms
(Bendera ya Uingereza) (Nembo la Uingereza)
Wito (Kifaransa): Dieu et mon droit
("Mungu na haki yangu")
Uingereza katika Ulaya
Uingereza kwenye visiwa vya Britania
Mahali pa Uingereza (kijani cheusi) kwenye visiwa vya Britania ndani ya Ufalme wa Maungano (kijani nyeupe) pamoja na Jamhuri ya Ueire (buluu) upande wa magharibi
Lugha Kiingereza
Mji Mkuu London
Mji Mkubwa London
Eneo
– jumla

130,395 km²
Wakazi

2004
–sensa ya 2001
– Msongamano wa watu

50.1 millioni [1]

49,138,831 [2]
377/km²

Umoja wa nchi yote 927 BK na mfalme
Athelstan
Dini rasmi Church of England (Anglikana)
Pesa Pound sterling (£) (GBP)
Masaa UTC / (GMT)
Summer: UTC +1 (BST)
Ua la Taifa Waridi ya Tudor (nyekundu, nyeupe)
Mtakatifu wa kitaifa Mt George

Uingereza ni nchi kubwa ndani ya Ufalme wa Maungano yenye wakazi milioni 50 au 83% ya wakazi wa Ufalme wote na eneo lake ni theluthi mbili ya kisiwa cha Britania.

Katika lugha ya kila siku "Uingereza" hutaja mara nyingi Ufalme wote au kisiwa.

Jiografia

Uingereza iko kwenye kisiwa cha Britania ambayo ni kisiwa kikubwa cha Ulaya. Imepakana na Welisi upande wa magharibi na Uskoti upande wa kaskazini. Mji Mkuu ni London. Ufaransa iko upande wa kusini ng'ambo ya Mfereji wa Kiingereza. Tangu mwaka 1994 kuna njia ya reli kwa tobwe chini ya mfereji inayounganisha Uingereza na Ufaransa.

Kati ya miji mikubwa ya Uingereza ni: London, Birmingham, Manchester, Leeds, Sheffield, Bradford na Liverpool.

Uingereza ina visiwa vingi vidogo; kikubwa ni Isle of Wight katika kusini.

Mito ya Uingereza

Mto Thames katika London mnamo mwaka 1750

Historia

Uingereza ilikaliwa na makabila ya Wabritania wenye lugha za Kikelti na kuvamiwa na Dola la Roma katika karne ya pili BK. Ikawa sehemu ya Dola la Roma hadi karne ya tano BK. Wakati ule Waroma walipaswa kuondoa wanajeshi wao kisiwani kwa ajili ya ulinzi wa nchi za bara.

Uvamizi wa Waanglia-Saksoni

Katika karne za 5 na 6 BK makabila ya Kigermanik walivamia kisiwa hasa Wasaksoni, Waanglia na Wadenmark. Walileta lugha zao za Kigermanik zilizochukua nafasi ya lugha ya Wabritania.

Wabritania na Waroma waliokuwa wamebaki walihamia maeneo ya kando kama Welisi au Cornwall au kuvuka mfereji wa Uingereza kwenda Britania Ndogo (Kiingereza:Brittany; Kifaransa: Bretagne).

Karne zilizofuata kisiwa kiliona madola madogo na hali ya vita. Mwaka 937 Mfalme Athelstan aliweza kuunganisha karibu eno lote la Uingereza ya leo.

Uvamizi wa Wanormani

Mwaka 1066 wanajeshi Wanormani kutoka kaskazini ya Ufaransa walivamia Uingereza na kuteka yote chini ya mtemi William Mshindi. Wavamizi walitawala wakitumia aina ya Kifaransa. Lugha zote mbili za wananchi na za mabwana ziliendelea pamoja sambamba hadi kuwa lugha moja cha Kiingereza.

Ufalme wa Maungano

Tangu mwaka 1601 mfalme James VI wa Uskoti alichaguliwa kuwa mfalme wa Uingereza pia. Nchi jirani zote mbili ziliendelea na mfalme mmoja hadi mwaka 1707. Mwaka ule Uingereza pamoja na Welisi na Uskoti ziliunganishwa kuwa Ufalme wa Maungano ya Britania. Tangu 1801 jina likawa Ufalme wa Maungano ya Britania na Eire (United Kingdom of Great Britain and Ireland) hadi 1927 wakati sehemu kubwa ya Eire ikapata uhuru wake. Tangu 1927 Uingereza ni sehemu ya Ufalme wa Maungano ya Britania na Eire ya Kaskazini (United Kingdom of Great Britain and Northern Ireland).

Mji wa Liverpool

Viungo vya nje

ak:Ngyiresi

  1. Office for National Statistics - UK population approaches 60 million
  2. Office for National Statistics - 2001 census Population profile - England.