Bamba la gandunia : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
kiungo
No edit summary
Mstari 1: Mstari 1:
[[Image:Mabamba gandunia (tectonic plates).png|thumb|350px|Mabamba gandunia ya dunia yetu]]
[[Image:Mabamba gandunia (tectonic plates).png|thumb|350px|Mabamba gandunia ya dunia yetu]]
'''Bamba gandunia''' ni kipande kikubwa cha [[ganda la dunia]] lenye mwendo wake wa pekee pamoja na au dhidi ya mabamba [[gandunia]] mengine.
'''Bamba gandunia''' ni kipande kikubwa cha [[ganda la dunia]]. Hoja la sayansi ni ya kwamba ganda la dunia limevunjika kwa vipande mbalimbali vinavyoitwa mabamba. Kila bamba lapakana na mabamba mengine. Mabamba yasukumwa na mikondo ya moto chini yao kama majani yanayokaa usoni wa maji inayoanza kuchemka katika sufuria. Hivyo kila bamba lina mwendo wake wa pekee pamoja na au dhidi ya mabamba mengine.


Mabamba haya ni sehemu ya nje ya [[tabakamwamba]] (lithosferi). Tabaka hili limevunjika katika vipande vikubwa 7 na vingine vidogo vinavyoelea juu ya tabaka lenye hali ya kiowevu chenye mnato mzito.
Mabamba haya ni sehemu ya nje ya [[tabakamwamba]] (lithosferi). Tabaka hili limevunjika katika vipande vikubwa 7 na vingine vidogo vinavyoelea juu ya tabaka lenye hali ya kiowevu chenye mnato mzito.


Mabamba haya yote yameonekana kuwa na mwendo wa [[mita|sentimita]] kadhaa (2 - 20 [[cm]] zimepimwa) kwa mwaka. Mwendo huu husababishwa na nguvu ya [[magma]] (mwamba moto wa kiowevu) inayopanda juu na kusukuma mabamba haya. Ulinganisho ni kama vipande vya ganda inayotokea juu ya maziwa vinaanza kuonyesha mwendo kama sufuria ya maziwa imepashwa moto.
Mabamba haya yote yameonekana kuwa na mwendo wa [[mita|sentimita]] kadhaa (2 - 20 [[cm]] zimepimwa) kwa mwaka. Mwendo huu husababishwa na nguvu ya [[magma]] (mwamba moto wa kiowevu) inayopanda juu na kusukuma mabamba haya.


==Mabamba makuu ya dunia==
==Mabamba makuu ya dunia==

Pitio la 17:10, 4 Desemba 2007

Mabamba gandunia ya dunia yetu

Bamba gandunia ni kipande kikubwa cha ganda la dunia. Hoja la sayansi ni ya kwamba ganda la dunia limevunjika kwa vipande mbalimbali vinavyoitwa mabamba. Kila bamba lapakana na mabamba mengine. Mabamba yasukumwa na mikondo ya moto chini yao kama majani yanayokaa usoni wa maji inayoanza kuchemka katika sufuria. Hivyo kila bamba lina mwendo wake wa pekee pamoja na au dhidi ya mabamba mengine.

Mabamba haya ni sehemu ya nje ya tabakamwamba (lithosferi). Tabaka hili limevunjika katika vipande vikubwa 7 na vingine vidogo vinavyoelea juu ya tabaka lenye hali ya kiowevu chenye mnato mzito.

Mabamba haya yote yameonekana kuwa na mwendo wa sentimita kadhaa (2 - 20 cm zimepimwa) kwa mwaka. Mwendo huu husababishwa na nguvu ya magma (mwamba moto wa kiowevu) inayopanda juu na kusukuma mabamba haya.

Mabamba makuu ya dunia

Mabamba makubwa ya ganda la nje ya dunia ni:

Kati ya mabamba madogo ni:

Mwendo wa mabamba: jinsi Pangaea ilivyoachana na kutokea kwa bara za leo

Mendo wa mabamba

Mwendo wa mabamba haya umesababisha kutokea na kuvunjika kwa mabara katika historia ya dunia yetu.

Wataalamu hufikiri ya kwamba dunia ilikuwa na bara kubwa moja tu (Pangaea) miaka milioni 300 - 150 iliyopita iliyovunjika katika vipande au mabamba mbalimbali.

Hata mabamba yaliyopo kwa sasa yanategemewa kuendelea kuhamahama, kuvunjika au kupotea kabisa.

Kwa mfano Afrika iko katika mwenendo wa kupasuliwa kwenye mstari wa Bonde la Ufa yaani Afrika ya Mashariki inaelekea kujitenga na sehemu nyingine ya bara ikiwa bamba la pekee. Penye Bonde la Ufa la sasa bahari itatandiwa baada ya miaka milioni 20.

Bara Hindi au bamba la Uhindi inaendelea kusukuma dhidi ya bamba la Asia na kujisukuma chini ya milima ya Himalaya - kuna uwezekano ya kwamba itaingia kabisa na kutoweka.

Makala hiyo kuhusu "Bamba la gandunia" inatumia neno ambalo si kawaida na matumizi yake ni jaribio kwa jambo linalotajwa.
Wasomaji wanaombwa kuchangia mawazo yao.

Kamusi za Kiswahili ama zinatofautiana kuhusu matumizi ya neno hili au hazieleweki au hazina neno kwa jambo linalojadiliwa.