Mapokeo : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 9: Mstari 9:


Wazo hilo linatumika pia katika [[siasa]], [[falsafa]] na [[dini]], k.mf. kwa kwenda kinyume cha [[usasa]].
Wazo hilo linatumika pia katika [[siasa]], [[falsafa]] na [[dini]], k.mf. kwa kwenda kinyume cha [[usasa]].

==Katika Ukristo==
Katika [[Ukristo]], kuna [[mapokeo ya Kanisa]] yanayozingatiwa sana na baadhi ya [[madhehebu]] (hasa [[Wakatoliki]], [[Waorthodoksi]] na [[Waorthodoksi wa Mashariki]], lakini pia [[Waanglikana]] na wengineo) kwa sababu [[asili]] yao ni wakati wa [[Mitume wa Yesu]], ambao ulikuwa bado wakati wa [[Ufunuo]] wa [[Mungu]] katika [[imani]] ya madhehebu hayo.

Mapokeo ya namna hiyo yanaitwa [[mapokeo ya Mitume]] kwa kuyatofautisha na mapokeo mengi yaliyotokea baadaye na ambayo yanaweza kuwa mazuri lakini pia mabayaː kwa vyovyote hayambani Mkristo kwa msingi wa imani.

Hata hivyo madhehebu mengine, hasa ya [[Uprotestanti]], yanakataa yale yote yasiyopatikana wazi katika [[Biblia ya Kikristo]].


==Tanbihi==
==Tanbihi==

Pitio la 09:21, 15 Oktoba 2015

Maadhimisho ya sikukuu yanaweza kuendelea kama mapokeo, kama katika meza na mapambo haya ya Krismasi huko Polandi.

Mapokeo (kutoka kitenzi kupokea) ni imani au desturi zilizorithishwa katika kundi au jamii fulani zikiwa na maana maalumu tangu zamani.[1]

Kati yake kuna sikukuu, salamu na mavazi ambayo hayafai sana kutumika lakini yana maana kijamii, hasa kwa kumtambulisha mtu aliyeyavaa (k.mf. askari, mwanasheria, mtawa).

Mapokeo yanaweza kudumu na kubadilika kwa miaka elfuelfu, lakini yanaweza kuanzishwa na kuenea haraka.

Jina la Kiingereza "tradition" linatokana na kitenzi cha Kilatini tradere, yaani kueneza au kukabidhi.

Wazo hilo linatumika pia katika siasa, falsafa na dini, k.mf. kwa kwenda kinyume cha usasa.

Katika Ukristo

Katika Ukristo, kuna mapokeo ya Kanisa yanayozingatiwa sana na baadhi ya madhehebu (hasa Wakatoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki, lakini pia Waanglikana na wengineo) kwa sababu asili yao ni wakati wa Mitume wa Yesu, ambao ulikuwa bado wakati wa Ufunuo wa Mungu katika imani ya madhehebu hayo.

Mapokeo ya namna hiyo yanaitwa mapokeo ya Mitume kwa kuyatofautisha na mapokeo mengi yaliyotokea baadaye na ambayo yanaweza kuwa mazuri lakini pia mabayaː kwa vyovyote hayambani Mkristo kwa msingi wa imani.

Hata hivyo madhehebu mengine, hasa ya Uprotestanti, yanakataa yale yote yasiyopatikana wazi katika Biblia ya Kikristo.

Tanbihi

  1. Thomas A. Green (1997). Folklore: an encyclopedia of beliefs, customs, tales, music, and art. ABC-CLIO. ku. 800–. ISBN 978-0-87436-986-1. Iliwekwa mnamo 5 February 2011.  Check date values in: |accessdate= (help)