Kufa : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Addbot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 45 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q186234 (translate me)
d (GR) File renamed: File:Kufic Quran 7th Cent.jpgFile:Kufic Quran, sura 7, verses 86-87.jpg File renaming criterion #3: To correct obvious errors in file names, including misspelled [[c::en:Noun#Pr...
Mstari 8: Mstari 8:

Mwaka [[749]] [[Waabbasi]] baada ya kupindua [[Wamuawiya]] walifanya Kufa mji mkuu wa [[khilafa]] hadi [[762]] walipohamia [[Baghdad]].
Mwaka [[749]] [[Waabbasi]] baada ya kupindua [[Wamuawiya]] walifanya Kufa mji mkuu wa [[khilafa]] hadi [[762]] walipohamia [[Baghdad]].
[[Picha:Kufic Quran 7th Cent.jpg|thumb|200px|Kurani kwa mwandiko wa Kikufa, karne ya 8]]
[[Picha:Kufic Quran, sura 7, verses 86-87.jpg|thumb|200px|Kurani kwa mwandiko wa Kikufa, karne ya 8]]
Umuhimu wa Kufa ulipungua kisiasa lakini uliendelea kiutamaduni hadi karne ya 11. Mji ulikuwa kitovu cha theolojia ya Kiislamu na masomo ya Kurani. [[Abu Hanifa]] mwanzilishaji wa mkondo wa maelezo ya [[fiq]] alikuwa mtu wa Kufa. Mtindo wa kwanza wa mwandiko wa Kiarabu huitwa "[[Mwandiko wa Kufa]]" hadi leo.

Pitio la 13:04, 6 Oktoba 2015

Mahali pa Kufa nchini Irak

Kufa (pia: Kofa; Kar. الكوفة al-kūfah) ni mji wa Irak takriban 170 km kusini ya Baghdad mwenye wakazi 110,000.

Iko 10 km kaskazini ya Najaf kando la mto Frati. Kama mahali pa mauti ya Imam Ali Kufa pamoja na Samarra, Karbala na Najaf ni kati ya miji minne mitakatifu ya Washia nchini Irak.

Historia

Mji ulijulikana kwa jina la Surestan katika milki ya Uajemi wa Kale. Baada ya uvamizi wa Kiislamu mnamo 637 palikuwa na kambi kubwa la kijeshi lililoendelea kuwa mji mkuu wa kwanza wa Uislamu. Wanajeshi Waislamu 30,000 walipelekwa hapo kama walowezi. Khalifa Ali ibn Abu Talib alipeleka makao makuu yake hapo mwaka 656 akafa mjini mwaka .

Mwaka 749 Waabbasi baada ya kupindua Wamuawiya walifanya Kufa mji mkuu wa khilafa hadi 762 walipohamia Baghdad.

Kurani kwa mwandiko wa Kikufa, karne ya 8

Umuhimu wa Kufa ulipungua kisiasa lakini uliendelea kiutamaduni hadi karne ya 11. Mji ulikuwa kitovu cha theolojia ya Kiislamu na masomo ya Kurani. Abu Hanifa mwanzilishaji wa mkondo wa maelezo ya fiq alikuwa mtu wa Kufa. Mtindo wa kwanza wa mwandiko wa Kiarabu huitwa "Mwandiko wa Kufa" hadi leo.

Baada ya karne ya 11 mji uliharibiwa vitani mara kwa mara ukaanza kupungua sana hadi kukua katika karne ya 20.