Dolar ya Marekani : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
So How much is fifteen dollars c.d.s in Kenyan money please.
Tags: Mobile edit Mobile web edit
d Masahihisho aliyefanya 105.57.146.103 (Majadiliano) yalirejeshwa hadi sahihisho la mwisho na Legobot
Mstari 12: Mstari 12:


[[Jamii:Marekani]]
[[Jamii:Marekani]]
[[Jamii:Pesa]]kwa hivyo dollar kumina tano ni pesa ngapi za kenya.
[[Jamii:Pesa]]

Pitio la 21:11, 23 Agosti 2015

Dola ya Marekani

Dola ya Marekani (US-Dollar, kifupi USD) ni pesa halali ya Marekani. Alama yake ni USD au mara nyingi alama ya dola tu $.

Dola ya Marekani inapatikana kwa benknoti za dola 1, 2, 5, 10, 20, 50 na 100. Kuna pia sarafu ya dola 1.

Dola moja ina senti 100. Senti huitwa pia "penny" nchini Marekani. Kuna sarafu za nusu dola (half dollar, senti 50), robo dola (quarter, senti 25) na sarafu za senti 10 (dime), 5 (nickel) na 1 (penny).

Hadi 1969 benknoti ya dola ya Marekani ilikuwa na ahadi ya kwamba serikali ya Marekani atampatia kila mtu dhahabu kulingana na thamani ya dola hizi akipenda kuibadilisha. Usawa huu na thamani ya dhahabu ulifutwa. Leo hii dola ya Marekani ni pesa ya kuiamini serikali kama pesa zote. Maana yake watumiaji husadiki ya kwamba serikali haitachapisha dola kushinda uwezo wa uchumi na thamani ya bidhaa zilizopo nchini.

Tangu mwisho wa Vita Kuu ya Pili ya Dunia 1945 dola ya Marekani imekuwa pesa kuu duniani na sehemu kubwa ya biashara ya kimataifa hukadiriwa kwa bei za dola hizi. Lakini tangu kupatikana kwa Euro mwaka 1999 umuhimu wa dola ya Marekani imeanza kupungua polepole.