Seif Shariff Hamad : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
File:Seif Sharif Hamad at the 2013 Zanzibar International Film Festival.jpg
Mstari 1: Mstari 1:
[[File:Seif Sharif Hamad at the 2013 Zanzibar International Film Festival.jpg|thumb|Maalim Seif]]
[[Image:Maalim Seif.png|thumb|300px|Maalim Seif Shariff Hamad]]
[[Image:Maalim Seif.png|thumb|300px|Maalim Seif Shariff Hamad]]



Pitio la 23:50, 30 Julai 2015

Maalim Seif
Maalim Seif Shariff Hamad

Maalim Seif Shariff Hamad ni Katibu Mkuu wa chama cha upinzani CUF ( Chama cha Wananchi ). Alizaliwa 22 Oktoba mwaka 1943, katika kijiji cha Nyali, Mtambwe kisiwani Pemba, Tanzania.

Alipata elimu yake ya msingi katika skuli ya msingi Uondwe, 1950 na baadaye alijiunga na elimu ya sekondari katika skuli ya watoto wa kiume Wete Pemba 1952. Baadaye aliendelea na elimu ya sekondari katika skuli ya King George na kuhitimu kidato cha sita mwaka 1963 ambapo baadaye kati ya mwaka 1972 na 1975 alihitimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutunukiwa shahada ya kwanza ya Sayansi ya Siasa (Political Science).

Kazi

Kati ya mwaka 1972 na 1975 alifundisha katika skuli mbali mbali za Unguja na Pemba, zikiwemo Fidel Castro na Lumumba,

Siasa

Baadaye Maalim Seif alianza kuingia katika Masuala ya siasa, ambapo 1977 aliteuliwa kuwa Waziri wa Elimu na Utamaduni na Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi.

Mwaka 1977 hadi 1987, alikuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na kuwa Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama hicho.

Mwaka 1982 hadi 1987 alikuwa Mkuu wa Idara ya Uchumi na Mipango ya Chama cha Mapinduzi na 1984 aliteuliwa kuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar hadi mwaka 1988.

Baada hapo, misukosuko mikubwa ya kisiasa ilianza kumkumba ambapo Januari 1988 alipoteza nafasi ya Uwaziri Kiongozi na Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi baada ya aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Idrisa Abdulwakil kutangaza kulivunja Baraza la Mawaziri.

Kujiengua na CCM

  • Mei 1988, Maalim Seif alitoka katika chama cha CCM.

Kuanza kuwa chama cha upinzani

  • Mwaka 1992, Maalim Seif alichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CUF. Hivi sasa ni Katibu Mkuu wa chama hicho.

Ona Pia

Viungo vya Nje