Tungamo : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika ''''Masi''' katika elimu ya fizikia ni tabia ya mata, na kwa njia hii pia tabia ya gimba au dutu. Kipimo sanifu cha kimataifa cha masi ni kilogram...'
 
Mstari 8: Mstari 8:


==Masi na inesha==
==Masi na inesha==
Masi inafanya pia [[inesha]] (''inertia'') ya gimba fulani. Inesha ni tabia ya masi kubakia hali yake ya kutulia au kuwa na mwendo fulani hadi inaathiriwa na nguvu ya nje. Masi kubwa zaidi huwa na inesha kubwa zaidi na inahitaji nguvu kubwa zaidi kwa kubadilisha mwendo wake. Tunaiona kirahisi tukijaribu kusukuma baisikeli, gari au lori: masi zao no tofauti hivyo nguvu inayohitajika kuzisukuma au kuzisimamisha inatofautiana.
Masi inafanya pia [[inesha]] (''inertia'') ya gimba fulani. Inesha ni tabia ya masi kubakia katika hali yake ya kutulia au kuwa na mwendo fulani hadi iathiriwe na nguvu ya nje. Masi kubwa zaidi huwa na inesha kubwa zaidi na inahitaji nguvu kubwa zaidi kwa kubadilisha mwendo wake. Tunaiona kirahisi tukijaribu kusukuma baisikeli, gari au lori: masi zao ni tofauti hivyo nguvu inayohitajika kuzisukuma au kuzisimamisha inatofautiana.
.
.



Pitio la 13:17, 30 Mei 2015

Masi katika elimu ya fizikia ni tabia ya mata, na kwa njia hii pia tabia ya gimba au dutu. Kipimo sanifu cha kimataifa cha masi ni kilogramu. Alama yake katika fomula kwa kawaida ni .

Masi na uzani

Masi ni tofauti na uzani lakini katika maisha ya kawaida hatuoni tofauti. Hivyo tunatumia kipimo cha kilogramu pia kwa kutaja uzani wa sukari tunayonunua. Lakini hali halisi uzani wa gimba au masi ileile ni tofauti kutegemeana na graviti mahali ilipo. Kwa mfano mtu akifika mwezini uzani ni sehemu ya sita ya uzani wake duniani. Kwa hiyo mtu mweye uzito wa kilogramu 60 duniani atakuwa na kilogramu 10 pekee akipimwa mwezini. Sababu yake ni ya kwamba graviti ya mwezi ni ndogo kuliko duniani.

Masi na graviti

Graviti ya gimba fulani inategemeana na masi yake. Kila kitu hata gimba dogo kama jiwe, meza au mtu kina graviti yake. Ila tu masi kubwa ya dunia yetu inafanya graviti yake yaani nguvu inayosababisha ya kwamba watu na vitu havielei hewani bali kukaa kwenye uso wa ardhi tukivutwa kuelekea kitovu cha sayari yetu. Vitu vyote vinyvoshikwa na graviti ya dunia vina graviti yao vilevile lakini kwa sababu masi ya watu na vitu ni ndogo kabisa kuliko masi ya dunia hatuwezi kusikia tofauti. Pia mwezi unavutwa na graviti ya dunia yetu lakini masi ya mwezi ni kubwa kiasi graviti ya mwezi inathiri pia dunia. Hii inaonekana kirahisi kutokana na mabadiliko ya bahari kuwa maji kujaa na kupwa yanayosababishwa na uvutano wa graviti ya mwezi.

Masi na inesha

Masi inafanya pia inesha (inertia) ya gimba fulani. Inesha ni tabia ya masi kubakia katika hali yake ya kutulia au kuwa na mwendo fulani hadi iathiriwe na nguvu ya nje. Masi kubwa zaidi huwa na inesha kubwa zaidi na inahitaji nguvu kubwa zaidi kwa kubadilisha mwendo wake. Tunaiona kirahisi tukijaribu kusukuma baisikeli, gari au lori: masi zao ni tofauti hivyo nguvu inayohitajika kuzisukuma au kuzisimamisha inatofautiana. .