Ulinganifu : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika 'thumb|250px|Tofauti kati ya umbo linganifu na silinganifu '''Ulinganifu''' (pia: mpachano<ref>"Ulinganifu" ni pendekezo la kamusi ya...'
 
No edit summary
Mstari 32: Mstari 32:




[[Category:Jiometri]]
[[Category:Jiometria]]

Pitio la 21:25, 23 Mei 2015

Tofauti kati ya umbo linganifu na silinganifu

Ulinganifu (pia: mpachano[1], ing. symmetry ) ni tabia ya maumbo na magimba yenye sehemu zinazolingana. Kama sehemu za kitu ni kama pacha zinaitwa linganifu.

Miili ya viumbehai wengi inafuata muundo wa ulinganifu kwa sababu macho, masikio, mikono, miguu na viungo vingine (si vyote!) viko mahali sawa upande wa kushoto kama upande wa kulia. Hii ni kama taswira geu inayoakisiwa. Mfuno huu unaweza kuitwa ulinganifu wa mstari[2] kwa sababu sehemu pacha ya geu inatokea kwenye mstari wa kioo au jira ya ulinganifu.

Kuna mfumo wa pili unaofuata nukta ya ulinganifu (pia: nukta ya pacha[3]). Hapo pande mbili zina umbali sawa na kitovu ambacho ni nukta ya ulinganifu.

Mifano ya maumbo linganifu bapa


Marejeo

  1. "Ulinganifu" ni pendekezo la kamusi ya TUKI KKK/ESD, "mpachano" la KAST
  2. KAST inapendekeza "mstari pacha"; ing. linear symmetry
  3. KAST

Kujisomea

  • Stewart, Ian (2007). Why beauty is truth: the history of symmetry. Basic Books. ISBN 9780465082360. 

Viungo ya Nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons