Nyigu : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
dNo edit summary
Nyongeza picha
Mstari 36: Mstari 36:
==Picha==
==Picha==
<gallery>
<gallery>
Prionyx kirbyi, b, Seringveld.jpg|Apoidea (''Prionyx kirbyi'')
Ceraphonidae.jpg|Ceraphronoidea (spishi isiyotambuliwa)
Ceraphonidae.jpg|Ceraphronoidea (spishi isiyotambuliwa)
Chalcis sp.JPG|Chalcidoidea (''Chalcis myrifex'')
Chalcis sp.JPG|Chalcidoidea (''Chalcis myrifex'')

Pitio la 23:00, 16 Mei 2015

Nyigu
Dondora (nyigu mkubwa) (Vespa orientalis)
Dondora (nyigu mkubwa) (Vespa orientalis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Hymenoptera (Wadudu wenye mabawa mangavu)
Nusuoda: Apocrita (Hymenoptera wenye kiuno chembamba sana)
Ngazi za chini

Makundi bila tabaka (2) na familia za juu (14):

  • Aculeata
    • Apoidea
    • Chrysidoidea
    • Vespoidea
  • Parasitica
    • Ceraphronoidea
    • Chalcidoidea
    • Cynipoidea
    • Evanioidea
    • Ichneumonoidea
    • Megalyroidea
    • Mymarommatoidea
    • Platygastroidea
    • Proctotrupoidea
    • Stephanoidea
    • Trigonaloidea

Nyigu ni wadudu wa nusuoda Apocrita katika oda Hymenoptera wasio nyuki au sisimizi. Wadudu hawa wote ni mbuai au vidusia lakini ni lava tu ambao hula mawindo au mwathirika. Wadudu wapevu hula mbochi, mbelewele au vitu vyingine vyenye sukari. Nyigu mbuai hukamata wadudu (viwavi mara nyingi) au arithropodi wengine. Huwaweka katika tundu ardhini au katika tundu lililoundwa kwa matope au kwa aina ya “karatasi” baada ya kuwapooza kwa sumu katika ganglioni kuu. Halafu nyigu hulitaga yai juu ya mdudu aliyekamatwa. Huyu aendelea kuwa hai na kwa hivyo lava wa nyigu akitoka kwenye yai anapata chakula kisichooza. Hata mdudu bila bahati afa tu akiwa ameliwa takriban kabisa. Jambo la nyigu vidusia linafanana lakini nyigu hawa huacha mwathirika ambapo alimpata. Hutaga yai au mayai juu au ndani yake na lava wakitoka kwenye mayai wanaanza kula mwathirika. Kwa sababu ya mwenendo huu nyigu vidusia hutumika sana kwa kufanya udhibiti wa kibiolojia dhidi ya visumbufu.

Kinyume na nyigu wengine spishi za familia Chalcidae (nyigu-kidutu) husababisha vidutu kwa majani ya mimea na lava hula tishu yao. Spishi jamaa za familia Agaonidae (nyigu-matini) huyataga mayai yao katika ovari za maua ya mitini.

Picha