Burundi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
→‎Ukoloni: kiungo
Mstari 81: Mstari 81:


== Hali ya nchi kijamii na kisiasa ==
== Hali ya nchi kijamii na kisiasa ==
Burundi ilundwa kama ufalme ulioongozwa na Watutsi waliotawala Wahutu. Lakini kabla ya ukoloni mipaka kati ya vikundi hivi havikuwa imara mno; Wahutu matajiri katika utumishi wa mwami waliweza kupanda ngazi an kuwa Watutsi na pia Watutsi maskini waliweza kushuka ngazi na kuhesabiwa kati ya Wahutu, hasa baada ya kuoa au kuolewa na mtu wa upande mwingine. Uhusiano wa vikundu ulifanana zaidi ule wa matabaka si makabila.
Mara kadhaa nchi hii imekuwa na misukosuko na machafuko ya ki[[siasa]] na ya ki[[jamii]]. Shida kubwa ni kuwa Burundi haina [[maliasili]] ya kutosheleza [[umma]] na kutosheleza ratili ya kisiasa kwa walio wengi [[Wahutu]] (85%) na walio wachache [[Watutsi]] (14%) na [[Watwa]] (1%).


Utawala wa kikoloni uliimarisha mipaka kati ya makundi mawili maana kila mtu aliandikishwa na kupangwa katika moja wa vikundi hivi. Pia Wabelgiji walipendelea Watutsi na kuangalia wapate nafasi zote za uchifu ambako walipaswa kutoa kibali. Kuhamia kati ya vikundi kulikwisha. Mwishowe wa ukoloni sehemu ya Wabelgiji walibadilisha msimamo na kupendelea Wahutu.
Pia kuna [[Warundi]] wanaojinasibu kuwa wao sio Watutsi wala Wahutu bali ni [[Waswahili]]. Hilo kabila lilikuwepo toka enzi za tawala za kifalme nchini humo, na ndio wenyeji wa [[jiji]] la [[Bujumbura]], waliomsaidia [[Mwanamfalme]] [[Louis Rwagasore]] katika [[harakati]] za kutafuta [[uhuru]] wa Burundi.

Katika hali hii Burundi ilikaribia uhuru. Vyama vya kisiasa viliundwa vilivyofuata ugawaji wa kimbari kati Tutsi na Hutu. Mapigano ya kwanza kati ya Wahutu na Watutsi yalianza 1959, kabla ya uhuru yakikomeshwa na Wabelgiji.

Baada ya uhuru katika Burundi kinyume na Rwanda utawala ulibaki upande wa Watutsi kwa sababu jeshi lilikuwa mkononi mwao. Vipindi vya mashambulio kati ya vikundi vilifuata.1972 malakhi ya Wahutu waliuawa na jeshi la Kitutsi. 1993 uongozi wa Kitutsi ilikubali tena uchaguzi huru ambako Mhutu Melchior Ndadaye alichaguliwa kuwa raisi. Alipouawa na wanajeshi Watutsi malakhi ya Watutsi waliuawa na Wahutu wakali.

Kipindi kilichofuata kilikuwa vita ya wenyewe ya wenyewe katika sehemu mbalimbali za nchi. Tangu mwaka 1995 Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa zilijitahidi kujenga mapatano kati ya vikundi. Boutros Boutros-Ghali for them to intervene in the humanitarian crisis. Maraisi na wanasiasa walioshiriki katika jitihada hizi walikuwa pamoja na [[Julius Nyerere]], [[Boutros Boutros-Ghali]], [[Nelson Mandela]], [[Thabo Mbeki]] na rais wa Marekani [[Bill Clinton]].

Mapatano yaliyofikiwa na kusainiwa mwaka 2000 na washiriki karibu wote huko Arusha. Majadiliani yaliendelea hadi mwaka 2003 vita ilisiamishwa hatimaye. Mapatano yaliyofikiwa yanasema ya kwamba Watutsi pamoja na Watwa ambao ni asilimia 15 za wananchi watakuwa na asilimia 40 ya nafasi kwenye bunge na ya kwamba jeshini kila upande utashika asilimia 50% za nafasi. Pia kwenye senati ya bunge kila upande utakuwa na asilimia 50. <ref>[http://www.usip.org/library/pa/burundi/pa_burundi_08282000_toc.html Mapatano ya Arusha ya 2000 kuhusua mani na upatanisho kwa ajili ya Burundi, uk. Protocoll II, I, 11, 4a, Appendix I,I B 2-4]</ref>

Rais anachaguliwa na wananchi wote lakini mapatano yalisema rais wa kwanza atachaguliwa na bunge.

Pia kuna [[Warundi]] wachache wanaojinasibu kuwa wao sio Watutsi wala Wahutu bali ni [[Waswahili]]. Hilo kabila lilikuwepo toka enzi za tawala za kifalme nchini humo, na ndio wenyeji wa [[jiji]] la [[Bujumbura]], waliomsaidia [[Mwanamfalme]] [[Louis Rwagasore]] katika [[harakati]] za kutafuta [[uhuru]] wa Burundi.


Upande wa [[dini]], [[Wakristo]] ni 80-90% kati ya wakazi wote, hasa [[Wakatoliki]] (65%), halafu Waprotestanti (26%). [[Asilimia]] 5 wanafuata [[dini za jadi]] na 3 [[Uislamu]].
Upande wa [[dini]], [[Wakristo]] ni 80-90% kati ya wakazi wote, hasa [[Wakatoliki]] (65%), halafu Waprotestanti (26%). [[Asilimia]] 5 wanafuata [[dini za jadi]] na 3 [[Uislamu]].

Pitio la 23:00, 13 Mei 2015

Burundi
Map of Burundi
Satellite image of Burundi
NASA photo of Burundi

Jamhuri ya Burundi (iliyojulikana zamani kama Urundi) ni nchi ndogo ambayo iko katika eneo la Maziwa Makubwa ya Afrika. Burundi imepakana na Rwanda upande wa kaskazini, Tanzania upande wa mashariki, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa magharibi.

Burundi ni mwanachama wa Umoja wa Afrika na wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Jina

Jina lenyewe la nchi hii, limetokana kwa msingi na kutanuka kwa lugha ya Kirundi ambacho ni lugha ya Kibantu kama vile Kiswahili ambacho pia kinatumika sana ingawa si lugha rasmi mojawapo.

Jiografia

Burundi ni kati ya nchi ndogo zaidi zilizomo barani Afrika. Wakazi milioni 10 ni wengi kulingana na eneo dogo la nchi, msongamano wa watu ni wakazi 314.3 kwenye kila kilomita ya mraba.

Ingawa Burundi haina bahari, sehemu ya mpaka wake eneo la mashariki unaishia kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika.

Eneo lote ni nyanda za juu zenye kimo cha mita 1700 juu ya UB kwa wastani. Sehemu ya juu zaidi ni kilele cha mlima Heha chenye mita 2685 juu ya uwiano wa bahari uliopo katika safu ya milima inayopakana na bonde la ufa la Afrika ya Mashariki.

Sehemu ya magharibi ya nchi ni sehemu ya bonde la ufa yenye kimo cha mita 760-850 juu ya uwiano wa bahari. Sehemu ya kusini ya bonde la ufa katika Burundi imejaa maji ya Ziwa Tanganyika.

Upande wa mashariki wa safu ya milima inayopakana na bonde la ufa kuna chanzo cha mto Ruvyironza (pia: Luvironza) unaoishia katika mto Kagera na hivyo huhesabiwa kati ya vyanzo vya mto Naili.[1]

Hali ya hewa ni ya kitropiki: kuna vipindi viwili vya mvua. Joto linapungua kutokana na kimo cha nchi. Kuna mvua kwa wastani wa milimita 1,000 kwa mwaka.

Matumizi ya ardhi ni kwa ajili ya kilimo au mifugo. Msongamano wa watu umesababisha kuenea kwa ukataji wa misitu, mmomonyoko wa ardhi na kupotea kwa ardhi yenye rutuba[2]. Eneo la misitu lililobaki ni kilomita cha mraba 600 pekee linalopungua kwa kasi ya asilimia 9 kwa mwaka[3].

Kuna hifadhi mbili za taifa ambazo ni Hifadhi ya Taifa ya Kibira kwenye kaskazini-magharibi (inapakana na Msitu wa Nyungwe huko Rwanda), na Hifadhi ya Taifa ya Ruvubu upande wa kaskazni-mashariki karibu na mto Rurubu (pia Ruvubu au Ruvuvu). Hifadhi zote mbili zilianzishwa mwaka 1982 kwa shabaha ya kuhifadhi wanyamapori[4].

Hali ya nchi kijamii na kisiasa

Burundi ilundwa kama ufalme ulioongozwa na Watutsi waliotawala Wahutu. Lakini kabla ya ukoloni mipaka kati ya vikundi hivi havikuwa imara mno; Wahutu matajiri katika utumishi wa mwami waliweza kupanda ngazi an kuwa Watutsi na pia Watutsi maskini waliweza kushuka ngazi na kuhesabiwa kati ya Wahutu, hasa baada ya kuoa au kuolewa na mtu wa upande mwingine. Uhusiano wa vikundu ulifanana zaidi ule wa matabaka si makabila.

Utawala wa kikoloni uliimarisha mipaka kati ya makundi mawili maana kila mtu aliandikishwa na kupangwa katika moja wa vikundi hivi. Pia Wabelgiji walipendelea Watutsi na kuangalia wapate nafasi zote za uchifu ambako walipaswa kutoa kibali. Kuhamia kati ya vikundi kulikwisha. Mwishowe wa ukoloni sehemu ya Wabelgiji walibadilisha msimamo na kupendelea Wahutu.

Katika hali hii Burundi ilikaribia uhuru. Vyama vya kisiasa viliundwa vilivyofuata ugawaji wa kimbari kati Tutsi na Hutu. Mapigano ya kwanza kati ya Wahutu na Watutsi yalianza 1959, kabla ya uhuru yakikomeshwa na Wabelgiji.

Baada ya uhuru katika Burundi kinyume na Rwanda utawala ulibaki upande wa Watutsi kwa sababu jeshi lilikuwa mkononi mwao. Vipindi vya mashambulio kati ya vikundi vilifuata.1972 malakhi ya Wahutu waliuawa na jeshi la Kitutsi. 1993 uongozi wa Kitutsi ilikubali tena uchaguzi huru ambako Mhutu Melchior Ndadaye alichaguliwa kuwa raisi. Alipouawa na wanajeshi Watutsi malakhi ya Watutsi waliuawa na Wahutu wakali.

Kipindi kilichofuata kilikuwa vita ya wenyewe ya wenyewe katika sehemu mbalimbali za nchi. Tangu mwaka 1995 Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa zilijitahidi kujenga mapatano kati ya vikundi. Boutros Boutros-Ghali for them to intervene in the humanitarian crisis. Maraisi na wanasiasa walioshiriki katika jitihada hizi walikuwa pamoja na Julius Nyerere, Boutros Boutros-Ghali, Nelson Mandela, Thabo Mbeki na rais wa Marekani Bill Clinton.

Mapatano yaliyofikiwa na kusainiwa mwaka 2000 na washiriki karibu wote huko Arusha. Majadiliani yaliendelea hadi mwaka 2003 vita ilisiamishwa hatimaye. Mapatano yaliyofikiwa yanasema ya kwamba Watutsi pamoja na Watwa ambao ni asilimia 15 za wananchi watakuwa na asilimia 40 ya nafasi kwenye bunge na ya kwamba jeshini kila upande utashika asilimia 50% za nafasi. Pia kwenye senati ya bunge kila upande utakuwa na asilimia 50. [5]

Rais anachaguliwa na wananchi wote lakini mapatano yalisema rais wa kwanza atachaguliwa na bunge.

Pia kuna Warundi wachache wanaojinasibu kuwa wao sio Watutsi wala Wahutu bali ni Waswahili. Hilo kabila lilikuwepo toka enzi za tawala za kifalme nchini humo, na ndio wenyeji wa jiji la Bujumbura, waliomsaidia Mwanamfalme Louis Rwagasore katika harakati za kutafuta uhuru wa Burundi.

Upande wa dini, Wakristo ni 80-90% kati ya wakazi wote, hasa Wakatoliki (65%), halafu Waprotestanti (26%). Asilimia 5 wanafuata dini za jadi na 3 Uislamu.

Historia

Ufalme wa Burundi

Dola la kwanza katika eneo hili lilikuwa Ufalme wa Burundi. Katika mapokeo ya wenyeji ulianzishwa katika karne ya 17 na mtu kwa jina la Cambarantama aliyefika ama kutoka Rwanda ama kutoka Buha katika Mkoa wa Kigoma, Tanzania ya leo.

Ufalme huo ulitawaliwa na kundi la Watutsi waliokuwa wafugaji wa ng'ombe na kutawala wenyeji waliokuwa wakulima Wabantu. Watutsi walikuwa tabaka la kikabaila. Mfalme au mwami alikuwa mkuu wa makabaila hao ambao walitazamiwa kama mabwana wa ardhi iliyolimwa na watu wa kawaida. Hao wakulima waliruhusiwa kulima nchi wakipaswa kutoa huduma na sehemu ya mavuno kwa mabwana waliopaswa kuwatetea dhidi ya maadui.

Ufalme huo ulienea katika karne zilizofuata. Mwami Ntare IV Rutaganzwa Rugamba aliyetawala tangu mwaka 1796 hadi 1850 aliweza kupanua mipaka ya ufalme wake hadi kushika sehemu kubwa ya eneo la leo.

Ukoloni

Wazungu wa kwanza waliofika walikuwa wapelelezi Waingereza Richard Burton na John Hanning Speke mnamo mwaka 1854. Lakini habari za falme kwenye eneo kati ya maziwa makubwa hazikuenea sana. Wakati wa Mkutano wa Berlin 1885 Wajerumani hawakujua ya kwamba falme za Burundi na Rwanda zilikuwepo ndni ya eneo waliotegemea kutwaa. Waliitambua baadaye tu.

Mwaka 1894 Mjerumani wa kwanza alipita Burundi aliyekuwa Oskar Baumann. Wakati ule Ujerumani uliwahi tayari kuanzisha koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani lakini Wajerumani walichelewa kufika kaskazini-magharibi mwa maeneo waliyotazama kuwa sehemu yao.

Katika Burundi kikosi cha kwanza cha Kijerumani kilifika mnamo 1896 wakakuta ufalme wa mwami wakaridhika kumwacha mwakilishi mkazi (resident) katika mji mkuu Gitega ambaye hakuhusika na mambo ya utawala wa ndani. Wakati ule eneo lilijulikana kwa jina "Urundi". Hapa sawa na Rwanda na Bukoba Wajerumani walitumia mbinu ya eneo lindwa ingawa walikuwa pia na majadiliano kuingiza falme hizi za kienyeji moja kwa moja ndani ya koloni lao.

Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Burundi pamoja na Rwanda ilikabidhiwa kwa Ubelgiji kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa. Kimsingi Wabelgiji waliendelea na mfumo wa Wajerumani uliomwachia mtemi mamlaka kubwa.

Utawala

Burundi imegawiwa katika mikoa 17 (kwa Kifaransa province, kwa Kirundi: IProvense) inayoitwa kufuatana na miji yenye makao makuu ya utawala.

*Angalia Mikoa ya Burundi

Mikoa imegawiwa kwa wilaya inayoitwa "communes" na hii imegawiwa kwa "collines" (vilima).

Tazama pia

Tanbihi

  1. [Klohn, Wulf and Mihailo Andjelic. [http://www.fao.org/ag/AGL/AGLW/webpub/lakevic/LAKEVIC4.htm Lake Victoria: A Case in International Cooperation]. Food and Agriculture Organization of the United Nations. Retrieved on July 20, 2008]
  2. [Bermingham, Eldredge, Dick, Christopher W. and Moritz, Craig (2005). ''Tropical Rainforests: Past, Present, and Future''. Chicago, Illinois: [[University of Chicago]] Press, p. 146. ISBN 0-226-04468-8]
  3. [http://www.mongabay.com/deforestation.htm Worldwide Deforestation Rates] Food and Agriculture Organization of the U.N.: The State of the World's Forests 2003. Published on Mongabay.com. Retrieved on June 29, 2008.
  4. East, Rob (1999). ''African Antelope Database 1998''. [[Gland, Switzerland]]: [[International Union for Conservation of Nature]], p. 74. ISBN 2-8317-0477-4.
  5. Mapatano ya Arusha ya 2000 kuhusua mani na upatanisho kwa ajili ya Burundi, uk. Protocoll II, I, 11, 4a, Appendix I,I B 2-4

Marejeo

  • Mambo mengi ya Burundi yamepatikana kutoka CIA World Factbook 2000 na 2003 U.S. Department of State website.
  • Burundi: Ethnic Conflict and Genocide Reni Lemarchand and Lee H. Hamilton

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Serikali

Habari

Overviews

Maendelezo

Vinginevyo


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira