Burundi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
historia
Mstari 81: Mstari 81:


== Historia ==
== Historia ==
===Ufalme wa Burundi==
Dola la kwanza katika eneo hili lilikuwa Ufalme wa Burundi. Katika mapokeo ya wenyeji ulianzishwa katika karne ya 17 na mtu kwa jina la Cambarantama aliyefika ama kutoka Rwanda au kutoka Buha katika [[Mkoa wa Kigoma]], Tanzania ya leo.
Dola la kwanza katika eneo hili lilikuwa Ufalme wa Burundi. Katika mapokeo ya wenyeji ulianzishwa katika karne ya 17 na mtu kwa jina la Cambarantama aliyefika ama kutoka Rwanda au kutoka Buha katika [[Mkoa wa Kigoma]], Tanzania ya leo.


Mstari 87: Mstari 88:
Ufalme huu ulienea katika karne zilizofuata. Mwami Ntare IV Rutaganzwa Rugamba aliyetawala mnamo 1796 hadi 1850 aliweza kupanusha mipaka ya ufalme wake hadi kushika sehemu kubwa ya eno la leo.
Ufalme huu ulienea katika karne zilizofuata. Mwami Ntare IV Rutaganzwa Rugamba aliyetawala mnamo 1796 hadi 1850 aliweza kupanusha mipaka ya ufalme wake hadi kushika sehemu kubwa ya eno la leo.


===Ukoloni===
Wazungu wa kwanza waliofika walikuwa wapelelezi Waingereza [[Richard Burton]] and [[John Hanning Speke]] mnamo mwaka 1854. Walifuatwa na wengine na 1894 Mjerumani wa kwanza alipita hapa aliyekuwa [[Oskar Baumann.]] Wakati ule Ujerumani uliwahi tayari kuanzisha koloni yake ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani lakini Wajerumani walichelewa kufika kwenye kaskazini-magharibi ya maeneo waliyotazama kuwa sehemu yao. Katika Burundi kikosi cha kwanza cha Kijerumani kilifika mnamo 1896 wakakuta ufalme wa mwami wakaridhika kumwacha mwakilishi mkazi (resident) ktika mji mkuu [[Gitega]] ambaye hakuhusika na mambo ya utwala wa ndani. S
Wazungu wa kwanza waliofika walikuwa wapelelezi Waingereza [[Richard Burton]] and [[John Hanning Speke]] mnamo mwaka 1854. Walifuatwa na wengine na 1894 Mjerumani wa kwanza alipita hapa aliyekuwa [[Oskar Baumann.]] Wakati ule Ujerumani uliwahi tayari kuanzisha koloni yake ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani lakini Wajerumani walichelewa kufika kwenye kaskazini-magharibi ya maeneo waliyotazama kuwa sehemu yao. Katika Burundi kikosi cha kwanza cha Kijerumani kilifika mnamo 1896 wakakuta ufalme wa mwami wakaridhika kumwacha mwakilishi mkazi (resident) katika mji mkuu [[Gitega]] ambaye hakuhusika na mambo ya utwala wa ndani. Wakati ule eneo lilijulikana kwa jina "Urundi". Hapa sawa na Rwanda na Bukoba Wajerumani walitumia mbinu wa [[eneo lindwa]] ingawa vyanzo wa nyakati zile zinaonyesha ya kwamba walikuwa pia na majadiliano kuingiza falme hizi za kienyeji moja kwa moja ndani ya koloni yao.

Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Burundi pamoja na Rwanda ilikabidhiwa kwa Ubelgiji kwa niaba ya [[Shirikisho kwa Mataifa]]. Kimsingi Wabelgiji waliendelea na mfumo wa Wajerumani uliomwacha mtemi mamlaka makubwa.


== Utawala ==
== Utawala ==

Pitio la 11:41, 9 Mei 2015

Burundi
Map of Burundi
Satellite image of Burundi
NASA photo of Burundi

Jamhuri ya Burundi (iliyojulikana zamani kama Urundi) ni nchi ndogo ambayo iko katika eneo la Maziwa Makubwa ya Afrika. Burundi imepakana na Rwanda upande wa kaskazini, Tanzania upande wa mashariki, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa magharibi.

Jina lenyewe la nchi hii, limetokana kwa msingi na kutanuka kwa lugha ya Kirundi ambacho ni lugha ya Kibantu.

Jiografia

Burundi ni kati ya nchi ndogo zaidi zilizomo barani Afrika. Wakazi milioni 10 ni wengi kulingana na eneo dogo la nchi, msongamano wa watu ni wakazi 379 kwenye kila kilomita ya mraba.

Ingawa Burundi haina bahari, sehemu ya mpaka wake eneo la mashariki unaishia kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika.

Eneo lote ni nyanda za juu zenye kimo cha mita 1700 juu ya UB kwa wastani. Sehemu ya juu zaidi ni kilele cha mlima Heha chenye mita 2685 juu ya uwiano wa bahari uliopo katika safu ya milima inayopakana na bonde la ufa la Afrika ya Mashariki.

Sehemu ya magharibi ya nchi ni sehemu ya bonde la ufa yenye kimo cha mita 760-850 juu ya uwiano wa bahari. Sehemu ya kusini ya bonde la ufa katika Burundi imejaa maji ya Ziwa Tanganyika.

Upande wa mashariki wa safu ya milima inayopakana na bonde la ufa kuna chanzo cha mto Ruvyironza (pia: Luvironza) unaoishia katika mto Kagera na hivyo huhesabiwa kati ya vyanzo vya mto Naili.[1]

Hali ya hewa ni ya kitropiki: kuna vipindi viwili vya mvua. Joto linapungua kutokana na kimo cha nchi. Kuna mvua kwa wastani wa milimita 1,000 kwa mwaka.

Matumizi ya ardhi ni kwa ajili ya kilimo au mifugo. Msongamano wa watu umesababisha kuenea kwa ukataji wa misitu, mmomonyoko wa ardhi na kupotea kwa ardhi yenye rutuba[2]. Eneo la misitu lililobaki ni kilomita cha mraba 600 pekee linalopungua kwa kasi ya asilimia 9 kwa mwaka[3].

Kuna hifadhi mbili za taifa ambazo ni Hifadhi ya Taifa ya Kibira kwenye kaskazini-magharibi (inapakana na Msitu wa Nyungwe huko Rwanda), na Hifadhi ya Taifa ya Ruvubu upande wa kaskazni-mashariki karibu na mto Rurubu (pia Ruvubu au Ruvuvu). Hifadhi zote mbili zilianzishwa mwaka 1982 kwa shabaha ya kuhifadhi wanyamapori[4].

Hali ya nchi kijamii na kisiasa

Mara kadhaa nchi hii imekuwa na misukosuko na machafuko ya kisiasa na ya kijamii. Shida kubwa ni kuwa Burundi haina maliasili ya kutosheleza umma na kutosheleza ratili ya kisiasa kwa walio wengi Wahutu na walio wachache Watutsi na Watwa. Pia kuna kabila la Warundi wanaojinasibu kuwa wao sio Watutsi wala Wahutu bali ni Waswahili. Hilo kabila la Waswahili lilikuwepo toka enzi za tawala za kifalme nchini humo, na ndio wenyeji wa jiji la Bujumbura, waliomsaidia Mwanamfalme Louis Rwagasore katika harakati za kutafuta uhuru wa Burundi.

Historia

=Ufalme wa Burundi

Dola la kwanza katika eneo hili lilikuwa Ufalme wa Burundi. Katika mapokeo ya wenyeji ulianzishwa katika karne ya 17 na mtu kwa jina la Cambarantama aliyefika ama kutoka Rwanda au kutoka Buha katika Mkoa wa Kigoma, Tanzania ya leo.

Ufalme huu ulitawaliwa na kundi la Watutsi waliokuwa wafugaji wa ng'ombe na kutawala wenyeji waliokuwa wakulima Wabantu. Watutsi walikuwa takaba la kikabaila. Mfalme au mwami alikuwa mkuu wa makabaila hawa ambao walitazamiwa kama mabwana wa ardhi iliyolimwa na watu wa kawaida. Hao wakulima waliruhusiwa kulima nchi wakipaswa kutoa huduma na sehemu ya mavuno kwa mabwana waliopaswa kuwatetea dhidi maadui.

Ufalme huu ulienea katika karne zilizofuata. Mwami Ntare IV Rutaganzwa Rugamba aliyetawala mnamo 1796 hadi 1850 aliweza kupanusha mipaka ya ufalme wake hadi kushika sehemu kubwa ya eno la leo.

Ukoloni

Wazungu wa kwanza waliofika walikuwa wapelelezi Waingereza Richard Burton and John Hanning Speke mnamo mwaka 1854. Walifuatwa na wengine na 1894 Mjerumani wa kwanza alipita hapa aliyekuwa Oskar Baumann. Wakati ule Ujerumani uliwahi tayari kuanzisha koloni yake ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani lakini Wajerumani walichelewa kufika kwenye kaskazini-magharibi ya maeneo waliyotazama kuwa sehemu yao. Katika Burundi kikosi cha kwanza cha Kijerumani kilifika mnamo 1896 wakakuta ufalme wa mwami wakaridhika kumwacha mwakilishi mkazi (resident) katika mji mkuu Gitega ambaye hakuhusika na mambo ya utwala wa ndani. Wakati ule eneo lilijulikana kwa jina "Urundi". Hapa sawa na Rwanda na Bukoba Wajerumani walitumia mbinu wa eneo lindwa ingawa vyanzo wa nyakati zile zinaonyesha ya kwamba walikuwa pia na majadiliano kuingiza falme hizi za kienyeji moja kwa moja ndani ya koloni yao.

Baada ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Burundi pamoja na Rwanda ilikabidhiwa kwa Ubelgiji kwa niaba ya Shirikisho kwa Mataifa. Kimsingi Wabelgiji waliendelea na mfumo wa Wajerumani uliomwacha mtemi mamlaka makubwa.

Utawala

Burundi imegawiwa katika mikoa 18 (kwa Kifaransa province, kwa Kirundi: IProvense) inayoitwa kufuatana na miji yenye makao makuu ya utawala.

*Angalia Mikoa ya Burundi

Mikoa imegawiwa kwa wilaya inayoitwa "communes" na hii imegawiwa kwa "collines" (vilima).

Watu na Utamaduni

Utafiti

Mambo mengi ya Burundi yamepatikana kutoka CIA World Factbook 2000 na 2003 U.S. Department of State website.

Kichunguzi

Ongezea masomo kwa wingi

  • Burundi: Ethnic Conflict and Genocide Reni Lemarchand and Lee H. Hamilton

Tazama pia

Tanbihi

  1. [Klohn, Wulf and Mihailo Andjelic. [http://www.fao.org/ag/AGL/AGLW/webpub/lakevic/LAKEVIC4.htm Lake Victoria: A Case in International Cooperation]. Food and Agriculture Organization of the United Nations. Retrieved on July 20, 2008]
  2. [Bermingham, Eldredge, Dick, Christopher W. and Moritz, Craig (2005). ''Tropical Rainforests: Past, Present, and Future''. Chicago, Illinois: [[University of Chicago]] Press, p. 146. ISBN 0-226-04468-8]
  3. [http://www.mongabay.com/deforestation.htm Worldwide Deforestation Rates] Food and Agriculture Organization of the U.N.: The State of the World's Forests 2003. Published on Mongabay.com. Retrieved on June 29, 2008.
  4. East, Rob (1999). ''African Antelope Database 1998''. [[Gland, Switzerland]]: [[International Union for Conservation of Nature]], p. 74. ISBN 2-8317-0477-4.

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Serikali

Habari

Overviews

Maendelezo

Vinginevyo


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira