Gamal Abdel Nasser : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Legobot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 1 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q39524 (translate me)
d All info is kept in Wikidata, removed: {{Link FA|sv}} (3) using AWB (10903)
Mstari 19: Mstari 19:
[[Jamii:Waliofariki 1970]]
[[Jamii:Waliofariki 1970]]
[[Jamii:Marais wa Misri]]
[[Jamii:Marais wa Misri]]

{{Link FA|sv}}
{{Link FA|ur}}
{{Link FA|hr}}

Pitio la 21:24, 22 Aprili 2015

Gamal Abdel Nasser

Gamal Abdel Nasser (Kar. جمال عبد الناصر ‎gamal abd-an-nasir); (* 15 Januari 1918 mjini Alexandria; 28 Septemba 1970 mjini Kairo) alikuwa mwanajeshi na rais wa Misri kati ya 1954 hadi 1970.

Alikuwa kati ya viongozi wa mapinduzi ya kijeshi ya 1952 nchini Misri iliyompindua mfalme na kuanzisha jamhuri.

Alitaifisha mfereji wa Suez mwaka 1956 uliokuwa mali ya kampuni ya kigeni akaamuru kujengwa kwa lambo la Aswan tangu 1958.

Alijenga jeshi kubwa lililoshindwa mara mbili katika vita dhidi ya Israel. Katika siasa ya ndani alijaribu kupeleka Misri mbele kwa kuwapa wakina mama kura katika uchaguzi na elimu bila malipo kwa vijana wote. Wakulima wadogo walipewa mashamba. Lakini utawala wa serikali katika sehemu nyingi za uchumi uligonga ukuta kama katika nchi mbalimbali yaliyofuata utaratibu wa uchumi wa kupangwa na serikali.

Nasser alihesabiwa kati ya mashujaa wa harakati ya nchi zisizofungamana na upande wowote katika vita baridi kati ya Umoja wa Kisovyeti na Marekani.

1967 maazimio yake yalikuwa kati ya sababu za vita ya siku sita kati ya Istael na majirani Waarabu.


Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gamal Abdel Nasser kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.