Babeli : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
d Removing Link FA template (handled by wikidata)
Mstari 33: Mstari 33:
[[Jamii:Miji ya Biblia]]
[[Jamii:Miji ya Biblia]]
[[Jamii:Nchi ya Kihistoria ya Asia]]
[[Jamii:Nchi ya Kihistoria ya Asia]]

{{Link FA|fr}}

Pitio la 14:14, 22 Aprili 2015

Sehemu ya geti la Ishtar huko Babeli

Babeli ulikuwa mji wa kale katika Mesopotamia muhimu kwa karne nyingi kama mji mkuu wa milki zilizotawala maeneo makubwa ya Mashariki ya Kati.

Inatajwa mara nyingi katika Biblia, hata kwa jina la Babuloni.

Maghofu yake hupatikana karibu na mji wa kisasa wa Al Hillah (Irak) kando ya mto Frati 90 km kusini mwa Baghdad.

Historia

Orodha ya wafalme wake ilianza mnamo mwaka 2300 KK hivi. Mfalme mashuhuri wa kwanza alikuwa Hammurabi.

Babeli ulikuwa mji mkuu wa madola mawili makubwa kabla na baada ya kipindi cha enzi ya Ashuru. Kati ya 1770 KK hadi 1670 KK na mara ya pili kati ya 612 KK na 320 KK inaaminika ulikuwa mji mkubwa zaidi duniani.

Wakati wa Dola la Pili la Babeli mfalme Nebukadreza II alitawala nchi zote kati ya Palestina (Kanaani au Israeli) hadi Ghuba ya Uajemi.

Bustani ya malkia Semiramis ilikuwa moja ya maajabu saba ya dunia.

Piramidi au zigurat kubwa za mji zilikuwa maarufu na mfano wao ni mnara wa Babeli unaotajwa katika kitabu cha Mwanzo (Agano la Kale).

Wakati ule jeshi la Babeli liliteka mji wa Yerusalemu mwaka 587 KK, kubomoa hekalu la Suleimani na kuwapeleka Wayahudi hadi Mesopotamia kwa uhamisho wa Babeli.

Inaaminika ya kwamba sehemu kubwa za Biblia ya Kiebrania ziliandikwa uhamishoni kule Babeli.

Mwaka 539 KK Waajemi walivamia Dola la Babeli na kuliteka. Babeli uliendelea kuwa mji muhimu katika Dola la Uajemi.

Baada ya ushindi wa Aleksanda Mkuu juu ya mfalme Mwajemi Darius III, Babeli ulikuwa chini ya utawala wa Wagiriki. Aleksanda alikufa Babeli mwaka 323 KK katika jumba la kifalme la Nebukadreza.

Mwaka 275 KK Wagiriki walijenga mji mkuu mpya wakawalazimisha wakazi wa Babeli kuhamia huko Seleukia. Huo ulikuwa mwisho wa mji ule mkubwa.

Mataifa ya Kale walikumbuka mji wa Babeli kwa muda mrefu. Barua ya kwanza ya Petro na kitabu cha Ufunuo wa Yohane katika Agano Jipya (kilichoandikwa mnamo mwaka 90 BK) vinatumia jina la Babeli kama jina la kitendawili kuashiria Roma.