Atomu : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 12: Mstari 12:
Kiini huzungukwa na ganda ambalo ni si dutu imara lakini nafasi ya njia ambako elektroni huzunguka kiini. Nafasi hizi huitwa [[mizingo elektroni]]. Kielezo hiki kimekuwa msingi wa vielelezo vingine kama kile cha Bohr.
Kiini huzungukwa na ganda ambalo ni si dutu imara lakini nafasi ya njia ambako elektroni huzunguka kiini. Nafasi hizi huitwa [[mizingo elektroni]]. Kielezo hiki kimekuwa msingi wa vielelezo vingine kama kile cha Bohr.


Kiini huitwa kwa lugha ya Kilatini (pia kiingereza) "nucleus" na hapa lugha ya Kiswahili imepokea neno "nyuklia" kutoka ing. "nuclear" kwa ajili ya mambo yanayohusu matumizi ya nguvu ya atomi, kwa mfano [[nishati ya nyuklia]].
Kiini huitwa kwa lugha ya [[Kilatini]] (pia kwa [[Kiingereza]]) "nucleus" na hapa lugha ya Kiswahili imepokea neno "nyuklia" kutoka ing. "nuclear" kwa ajili ya mambo yanayohusu matumizi ya nguvu ya atomi, kwa mfano [[nishati ya nyuklia]].


== Chaji na ioni ==
== Chaji na ioni ==

Pitio la 19:20, 16 Aprili 2015

Mfumo wa atomi kwa mfano wa atomi ya Heli: Elektroni mbili (njano) kwenye mzingo wa atomi huzunguka kiini chenye Protoni mbili (nyekundu) na Neutroni mbili (kijani).

Atomi (pia: atomu; kutoka kigiriki ἄτομος átomos "yasiyogawiwa") ni sehemu ndogo ya maada yenye tabia ya kikemia kama elementi. Kila kitu duniani hujengwa kwa atomi. Atomi ni ndogo kiasi ya kwamba hazionekani kwa macho hata hazionekani kwa hadubini za kawaida. Kuna aina nyingi za atomi na idadi za aina hizi tofauti ni sawa na elementi zilizopo duniani.

Lakini atomi yenyewe hufanywa na vyembe vidogo zaidi hasa protoni, neutroni na elektroni. Sehemu hizi ndogo zaidi hazina tabia ya elementi fulani ila tu atomi yote ni elementi. Atomi zinatofautiana kutokana na idadi tofauti ya vyembe hivi vidogo ndani yao.

Muundo wa atomi

Atomi ni ndogo kiasi ya kwamba hazionekani. Kwa sababu hiyo wataalamu waliunda vielelezo mbalimbali vinavyojaribu kuunganisha tabia mbalimbali za atomi zinazopimiwa.

Kielelezo cha Ernest Rutherford kinasema ya kwamba kwamba katikati ya atomi kuna kiini chenye sehemu kubwa ya mada ya atomi yote. Kiini cha atomi hufanywa na protoni na neutroni.

Kiini huzungukwa na ganda ambalo ni si dutu imara lakini nafasi ya njia ambako elektroni huzunguka kiini. Nafasi hizi huitwa mizingo elektroni. Kielezo hiki kimekuwa msingi wa vielelezo vingine kama kile cha Bohr.

Kiini huitwa kwa lugha ya Kilatini (pia kwa Kiingereza) "nucleus" na hapa lugha ya Kiswahili imepokea neno "nyuklia" kutoka ing. "nuclear" kwa ajili ya mambo yanayohusu matumizi ya nguvu ya atomi, kwa mfano nishati ya nyuklia.

Chaji na ioni

Protoni zina chaji ya chanja, neutroni hazina chaji na elektroni zina chaji ya hasi. Kiini inafanywa na protoni zenye chaji chanja pamoja na neutroni zisizo na chaji hivyo kiini cha kila atomi kina chaji chanja. Elektroni zenye chaji hasi zazunguka kiini.

Kwa jumla chaji hizo husawazishana na atomi yote ni batili yaani haionyeshi chaji maalumu.

Atomi inaweza kuingia katika hali ya kuwa na chaji kama elektroni moja inaongezwa au kuondolewa katika ganda lake halafu atomi hiyo huitwa "ioni".

Kama idadi ya elektroni imepungua chini ya kiwango cha kawaida atomi yote ina chaji chanja na kuitwa "kationi". Kama elektroni imeongezwa chaji ya atomi yote huwa hasi na kuitwa "anioni".

Njia za elektroni

Kufuatana na kielezo cha Niels Bohr kiini huzungukwa na mizingo elektroni mbalimbali kama kitunguu. Idadi ya mizingo hutegemeana na idadi ya elektroni au ukubwa wa atomi kwa jumla.

Ukubwa wa atomi yote hutegemeana na umbali wa mzingo elektroni wa nje. Ieleweke ya kwamba mizingo hii yote si dutu au mada lakini nafasi ambako elektroni zazunguka kiini kwa mkasi mkubwa.

Tovuti za Nje

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Atomu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Atomu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA