Morisi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 98: Mstari 98:
* [[Utalii nchini Morisi]]
* [[Utalii nchini Morisi]]


{{mbegu-jio-Afrika}}
{{Afrika}}
{{Afrika}}
{{mbegu-jio-Afrika}}


[[Jamii:Visiwa vya Afrika|M]]
[[Jamii:Visiwa vya Afrika|M]]
Mstari 105: Mstari 105:
[[Jamii:Morisi|*]]
[[Jamii:Morisi|*]]
[[Jamii:Nchi za Afrika|M]]
[[Jamii:Nchi za Afrika|M]]
[[Jamii:Nchi za visiwa]]
[[Jamii:Jumuiya ya Madola]]

Pitio la 14:33, 21 Februari 2015

Morisi
Ramani ya kisiwa cha Morisi

Morisi ni kisiwa karibu na Afrika, pia ni nchi inayoitwa rasmi Jamhuri ya Morisi (Kiingereza: Republic of Mauritius, Kifaransa: République de Maurice) ni nchi ya visiwa katika Bahari Hindi takriban 900 km mashariki kwa Madagaska na 4000 km kusini-magharibi kwa Bara Hindi.

Nchi ilipata uhuru tarehe 12 Machi 1968, ikawa jamhuri tarehe hiyohiyo mwaka 1992.

Eneo la jamhuri ni pamoja na kisiwa cha Morisi yenyewe, kisiwa cha Rodrigues, visiwa vidogo vya Cargados Carajos na Agalega.

Hivi vyote ni sehemu ya funguvisiwa ya Maskarena pamoja na kisiwa cha Kifaransa cha Réunion.

Mji mkuu wa jamhuri ni Port Louis.

Eneo la Jamhuri ya Morisi

Visiwa vya jamhuri vimesambaa katika eneo pana sana:

Kisiwa kikuu cha Morisi ni 1,865km² au 91 % za ardhi yote ya jamhuri. Karibu wakazi wote (1,261,208) huishi hapo.

Kisiwa cha Rodrigues kipo 560 km mashariki kwa Morisi yenyewe. Eneo lake ni 109 km²; kuna wakazi 41,000.

Visiwa vya Makarena kati ya visiwa vya Kiafrika katika Bahari Hindi

Visiwa vya Cargados Carajos (vinaitwa pia Saint Brandon) ni visiwa 16 vidogo sana, vyenye eneo la 1.3 km² pekee. Viko 300 km kaskazini kwa Morisi. Kuna wakazi mia chache wavuvi.

Agalega ni visiwa viwili, yaani Kisiwa cha Kaskazini na Kisiwa cha Kusini, takriban 1,122 Km kaskazini kwa Morisi yenyewe. Visiwa hivyo vina eneo la 70 km². Kuna vijiji vya Vingt Cinq na La Fourche kwenye kisiwa cha kaskazini na kijiji cha Ste Rita kwenye kisiwa cha kusini. Wenyeji wanalima mazao ya mnazi pamoja na mboga kwa matumizi yao wenyewe.

Wakazi

Watu wa Morisi ni mchanganyiko mkubwa kutokana na historia ya visiwa hivi.

Baada ya Waarabu na Wareno kuvumbua Morisi, wakazi wa kwanza (1638) walikuwa Waholanzi, lakini hawakuacha dalili isipokuwa majina ya mahali kwa sababu waliacha visiwa na kuondoka mwaka 1710 baada ya kushindwa kiuchumi.

Wafaransa walitawala visiwa kati ya 1715 hadi 1810. Walianzisha miji na mashamba ya miwa. Nje ya walowezi, Wafaransa walipeleka pia watumwa kutoka bara la Afrika. Mwaka 1767 walikuwepo Wafaransa 3,163 pamoja na watumwa Waafrika 15,000, pia Wahindi 587.

Uingereza ulichukua utawala wa visiwa mwaka 1810 katika vita dhidi ya Napoleon. Tangu siku zile Kiingereza kilikuwa lugha rasmi ya serikali, lakini wakazi waliendelea kutumia lahaja za Kifaransa.

Baada ya kuwapatia watumwa uhuru, Waingereza walileta Wahindi wengi, baadaye pia Wachina kama wafanyakazi kwenye mashamba ya sukari. Leo hii idadi kubwa ya wakazi ni wa asili ya Kihindi.

Lakini 80% ya wananchi hutumia aina ya Kifaransa kama lugha ya kwanza (pamoja na krioli ya Kimorisyen. Asilimia 15 hutumia lugha za Kihindi kama vile Kibhojpuri, Kiurdu, Kitamil, na wengine Kichina na Kiingereza.

Karibu nusu (48.5%) ya wakazi hufuata dini ya Uhindu, 32.7% Ukristo (hasa Wakatoliki), 17.3% ni Waislamu (hasa Wasunni, lakini pia Washia), 0.4% Wabuddha.

Uchumi

Hadi leo kilimo cha miwa (sukari) ni uti wa mgongo wa uchumi wa Morisi.

Nchi iliendelea na serikali zilizochaguliwa bila kupinduliwa: hali hii ya utulivu ilisaidia kukua kwa uchumi. Hali ya maisha ni ya juu kuliko nchi nyingi za Afrika.

Tazama pia


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Morisi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.