Jimbo Katoliki la Morogoro : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
kilatini >kanisa la kiroma
Mstari 4: Mstari 4:
Eneo lote lina [[kilometa mraba]] 43,380.
Eneo lote lina [[kilometa mraba]] 43,380.


Kutokana na [[historia]] yake linafuata mapokeo ya [[Kilatini]], kama majimbo mengine yote ya Tanzania.
Kutokana na [[historia]] yake linafuata mapokeo ya [[Kanisa la Kiroma]], kama majimbo mengine yote ya Tanzania.


==Uongozi wake==
==Uongozi wake==

Pitio la 08:50, 5 Januari 2015

Hii ni sehemu ya mfululizo kuhusu
Kanisa Katoliki
Imani

Umoja wa Mungu
Utatu (Baba, Mwana, Roho Mtakatifu)
Umwilisho Maisha ya Yesu
Msalaba Ufufuko Kupaa
Historia ya Wokovu Ufunuo
Biblia Mapokeo Ualimu Dogma
Neema Dhambi Wokovu Sakramenti
Watakatifu Bikira Maria

Muundo

Papa: Fransisko
Urika wa maaskofu Mitaguso mikuu
Kundi la Makardinali
Kanisa la Kilatini
Makanisa Katoliki ya Mashariki

Historia

Historia Ukristo
Ukatoliki Mlolongo wa Kitume
Sifa nne za Kanisa Utetezi Ekumeni
Maisha ya kiroho Amri Kumi Utawa
Sala Falsafa Teolojia
Muziki Sanaa Sayansi

Ibada

Liturujia Mwaka wa Kanisa
Ekaristi Liturujia ya Vipindi

Mapokeo ya liturujia

Liturujia ya Kilatini (Roma Liturujia ya Trento Milano Toledo Braga Lyon Canterbury)
Liturujia ya Armenia Liturujia ya Misri
Liturujia ya Ugiriki Liturujia ya Antiokia
Liturujia ya Mesopotamia

Jimbo la Morogoro ni mojawapo katika ya majimbo 34 ya Kanisa Katoliki nchini Tanzania kwa ajili ya waumini wake katika manispaa ya Morogoro pamoja na wilaya za Bagamoyo, Morogoro vijijini, Mvomero, Kilosa, Gairo n.k.

Eneo lote lina kilometa mraba 43,380.

Kutokana na historia yake linafuata mapokeo ya Kanisa la Kiroma, kama majimbo mengine yote ya Tanzania.

Uongozi wake

Kwa njia ya askofu wake, Telesphore Mkude, ambaye yumo katika urika wa maaskofu unaongozwa na papa wa Roma, lina ushirika kamili na Kanisa Katoliki lote duniani.

Papa analisimamia kupitia Idara ya Uinjilishaji wa Mataifa.

Kazi zake

Likiishi katika eneo ambapo wananchi walio wengi ni Waislamu, linajadiliana nao kwa amani pamoja na kutangaza Injili ya Yesu Kristo.

Likitegemea uwezo wa Roho Mtakatifu katika liturujia linazidi kuwatakasa watu ili waishi kama watoto halisi wa Baba wa mbinguni.

Kwa mamlaka waliyokabidhiwa kwanza Mitume na kurithiwa kwa sakramenti yadaraja, linazidi kuwachunga waamini washuhudie upendo kati yao na kwa wote, hasa kwa kutumikia wanaohitaji huduma zake mbalimbali za kijamii pia (upande wa afya, elimu, n.k.).

Miundo na michango ya waamini mbalimbali

Mbali ya ofisi na taasisi mbalimbali (k.mf. seminari), miundo yake ya msingi ni parokia zilizoenea katika wilaya zake zote na zinazoongozwa na mapadri wanajimbo na wanashirika, ambao baadhi yao ni wazalendo, baadhi walitokea nchi za jirani na za mbali (hasa Asia na Ulaya).

Watawa wa kike na wa kiume wengi wa mashirika 40 hivi wanatoa mchango wa pekee kwa kushuhudia maisha ya Yesu katika useja mtakatifu, ufukara na utiifu.

Hatimaye walei, ambao ndio wanakanisa walio wengi, wanatimiza utume wao katika majukumu ya kila siku ya maisha ya kawaida vijijini na mitaani, wakishirikiana katika mtandao wa vigango, vinavyotegemea sana makatekista, na wa jumuia ndogondogo za Kikristo, zilizopewa kipaumbele na Sinodi ya Afrika.

Malengo

Ni juhudi yao kulenga hali ya kujitegemea hata kiuchumi, ingawa hali halisi ya nchi ni ngumu kwa sababu zilezile zilizoathiri karibu nchi zote za bara hilo.

Wakitegemea neema ya Mungu, ni juhudi yao hasa kushinda dhambi ndani mwao wenyewe na ndani ya miundo ya jamii ili utawala wa Mungu uenee kote na kuleta utakatifu na wokovu, haki na amani.

Takwimu

Mwishoni mwa mwaka 2007 jimbo lilikuwa na waamini waliobatizwa 645,762 kati ya wakazi 1,568,640 (41,2%).

Katika parokia 53 kulikuwa na mapadri 128 (wanajimbo 75 na watawa 53), mabradha 56 na masista 666.

Viungo vya nje