Sukulenti : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
kiungo
link
Mstari 1: Mstari 1:
[[Picha:Split Aloe.jpg|300px|thumbnail|Jani la Aloe lililokatwa; utomvu unatoka nje]]
[[Picha:Split Aloe.jpg|300px|thumbnail|Jani la [[Aloe vera]] lililokatwa; utomvu unatoka nje]]
'''Sukulenti''' ([[lat.]] ''sucus'' = utomvu; [[ing.]] ''succulents'') au '''Mimea wenye utomvu mwingi''' ni [[mimea]] iliyojitohoa kwa maisha katika mazingira [[Tabianchi#B:_Tabianchi_yabisi_au_nusuyabisi|yabisi]].
'''Sukulenti''' ([[lat.]] ''sucus'' = utomvu; [[ing.]] ''succulents'') au '''Mimea wenye utomvu mwingi''' ni [[mimea]] iliyojitohoa kwa maisha katika mazingira [[Tabianchi#B:_Tabianchi_yabisi_au_nusuyabisi|yabisi]].



Pitio la 10:28, 1 Desemba 2014

Jani la Aloe vera lililokatwa; utomvu unatoka nje

Sukulenti (lat. sucus = utomvu; ing. succulents) au Mimea wenye utomvu mwingi ni mimea iliyojitohoa kwa maisha katika mazingira yabisi.

Mimea hii ya familia na jenasi tofauti ina uwezo wa kutunza maji ndani ya majani au mashina yao. Kwa hiyo mara nyingi ama majani au shina ni nono kutokana na uwingi wa utomvu ndani yao.

Kwa hiyo "sukulenti" si jina la spishi au familia maalumu ya mimea lakini inataja umbo la mmea unaotkuwa tofauti kutokana na mazingira. Mimea ya aina (jenasi) moja inaweza kupatikana kwa majani nono yenye utomvu mwingi au kwa majani ya kawaida yakikua katika mazingira tofauti.

Pia kuna tofauti kati ya watalaamu eti ni nini inayostahili kuitwa sukulenti. Wengi wanaangalia majani na mashina pekee lakini kuna wengine wanaoingiza mle pia mizizi inayotunza maji lakini wengine hawakubali.

Mifano ya sukulenti iliyokubalika na pande zote ni mbuyu, mkonge, aloe vera na aina za mpungate.