Papa Alexander VI : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 6: Mstari 6:


==Maisha==
==Maisha==
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa '''Roderic Borgia'''. Alikuwa papa wa pili kutoka familia ya Borgia. [[Papa Kalisti III]], aliyekuwa wa kwanza, alimsaidia [[mpwa]] wake Roderic kupanda [[ngazi]] ndani ya [[Kanisa]]. [[Kijana]] asiyekuwa na mafunzo yoyote wa kiroho, asiyepokea [[daraja takatifu]] ya [[upadri]] bado, alipewa [[cheo]] na mapato ya [[askofu]] mara kadhaa katika [[dayosisi]] mbalimbali.
Jina lake la kuzaliwa lilikuwa ''' Roderic Llançol de Borja'''. Alikuwa papa wa pili kutoka [[familia]] iliyoitwa nchini [[Italia]] '''Borgia'''. [[Papa Kalisti III]], aliyekuwa wa kwanza, alimsaidia [[mpwa]] wake Roderic kupanda [[ngazi]] ndani ya [[Kanisa]]. [[Kijana]] asiyekuwa na mafunzo yoyote wa kiroho, asiyepokea [[daraja takatifu]] ya [[upadri]] bado, alipewa [[cheo]] na mapato ya [[askofu]] mara kadhaa katika [[dayosisi]] mbalimbali.


Mwaka [[1456]] alipewa cheo cha [[kardinali]] na mwaka [[1458]] [[upadrisho|akapadrishwa]].
Mwaka [[1456]] alipewa cheo cha [[kardinali]] na mwaka [[1458]] [[upadrisho|akapadrishwa]].
Mstari 14: Mstari 14:
Lakini kabla hajachaguliwa kuwa papa alimwacha Vannozza akaanza uhusiano na binti Giulia Farnese aliyezaa naye binti mwaka [[1492]], alipokuwa papa tayari.
Lakini kabla hajachaguliwa kuwa papa alimwacha Vannozza akaanza uhusiano na binti Giulia Farnese aliyezaa naye binti mwaka [[1492]], alipokuwa papa tayari.


Mwanawe [[Cesare Borgia]] alipewa cheo cha askofu alipokuwa na umri wa miaka 16 na cha kardinali alipofikia miaka 18. Baadaye aliacha maisha ya Kanisa akafanywa na baba yake [[jemadari]] wa [[jeshi]] la Papa.
Mwanawe [[Cesare Borgia]] alipewa cheo cha askofu alipokuwa na umri wa miaka 16 na cha kardinali alipofikia miaka 18, lakini bila kupewa [[sakramenti]] ya [[daraja takatif]]u. Baadaye aliacha maisha ya Kanisa akafanywa na baba yake [[jemadari]] wa [[jeshi]] la Papa.


Aleksanda VI amejulikana pia kwa [[uamuzi]] wake wa kugawa [[dunia]] kati ya [[Hispania]] na [[Ureno]] katika [[mkataba wa Tordesillas]] mwaka [[1494]]. Mkataba huu ulikuwa msingi wa [[koloni]] la Kireno la [[Brazil]] na [[utawala]] wa Hispania juu ya nchi nyingine za [[Amerika Kusini]] na [[Amerika ya Kati]].
Aleksanda VI amejulikana pia kwa [[uamuzi]] wake wa kugawa [[dunia]] kati ya [[Hispania]] na [[Ureno]] katika [[mkataba wa Tordesillas]] mwaka [[1494]]. Mkataba huu ulikuwa msingi wa [[koloni]] la Kireno la [[Brazil]] na [[utawala]] wa Hispania juu ya nchi nyingine za [[Amerika Kusini]] na [[Amerika ya Kati]].

Pitio la 14:58, 12 Septemba 2014

Papa Aleksanda VI akisali alivyochorwa na Pinturicchio.

Papa Alexander VI (1 Januari 143118 Agosti 1503) alikuwa papa kuanzia tarehe 11 Agosti 1492 hadi kifo chake.

Alimfuata Papa Innocent VIII akafuatwa na Papa Pius III.

Maisha

Jina lake la kuzaliwa lilikuwa Roderic Llançol de Borja. Alikuwa papa wa pili kutoka familia iliyoitwa nchini Italia Borgia. Papa Kalisti III, aliyekuwa wa kwanza, alimsaidia mpwa wake Roderic kupanda ngazi ndani ya Kanisa. Kijana asiyekuwa na mafunzo yoyote wa kiroho, asiyepokea daraja takatifu ya upadri bado, alipewa cheo na mapato ya askofu mara kadhaa katika dayosisi mbalimbali.

Mwaka 1456 alipewa cheo cha kardinali na mwaka 1458 akapadrishwa.

Alizaliana watoto na mke wake wa kando Vannozza dei Cattani akaendelea kuwaangalia na kuwatunza hata alipokuwa papa. Arusi ya binti yake Lucrezia Borgia ilisheherekewa rasmi katika jumba la Kipapa la Vatikano.

Lakini kabla hajachaguliwa kuwa papa alimwacha Vannozza akaanza uhusiano na binti Giulia Farnese aliyezaa naye binti mwaka 1492, alipokuwa papa tayari.

Mwanawe Cesare Borgia alipewa cheo cha askofu alipokuwa na umri wa miaka 16 na cha kardinali alipofikia miaka 18, lakini bila kupewa sakramenti ya daraja takatifu. Baadaye aliacha maisha ya Kanisa akafanywa na baba yake jemadari wa jeshi la Papa.

Aleksanda VI amejulikana pia kwa uamuzi wake wa kugawa dunia kati ya Hispania na Ureno katika mkataba wa Tordesillas mwaka 1494. Mkataba huu ulikuwa msingi wa koloni la Kireno la Brazil na utawala wa Hispania juu ya nchi nyingine za Amerika Kusini na Amerika ya Kati.

Sifa yake nyingine ilikuwa kuhamasisha sanaa za kila aina, kama ilivyokuwa kawaida kwa Mapapa wa Renaissance.

Vilevile alianza urekebisho wa ofisi za Papa.

Wapinzani walimwona kama mfano mbaya wa upotovu wa Upapa wakati wake, wakamsema hata kuliko ukweli wa makosa ambayo aliyafanya na aliyatubu kabla hajafa.

Marejeo

Viungo vya nje

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu Papa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Papa Alexander VI kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.