Serikali ya kiraisi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
mbegu-siasa
link to Ufaransa
Mstari 28: Mstari 28:


==Muundo wa kumbakumba ya Serikali==
==Muundo wa kumbakumba ya Serikali==
Nchi mbalimbali hutumia utaratibu wa kuunganisha tabia za serikali ya kiraisi na serikali ya kibunge. Mfano wake ni Ufaransa ambako rais anayechaguliwa na wanachi wote hushirikiana na waziri mkuu anayetegemea bunge. Rais ana madaraka kadhaa pamoja na haki ya kuongoza mikutano ya mawaziri akitaka. Ana haki ya kutoa mwongozo juu ya siasa ya nje na pia ni mkuu wa jeshi. Lakini anahitaji kushiriki katika kempeni za bunge na kuomba wananchi kumpa wabunge watakoshikamana naye. Kama wananchi wanaamua tofauti anapaswa kushirikiana na waziri mkuu asiyekubali naye katika siasa. Hii ni njia mojawapo kuwapa wanachi nafasi ya kuweka mipaka kwa madaraka na uwezo wa rais wakiona asiamue kila kitu tena pekee yake.
Nchi mbalimbali hutumia utaratibu wa kuunganisha tabia za serikali ya kiraisi na serikali ya kibunge. Mfano wake ni [[Ufaransa]] ambako rais anayechaguliwa na wanachi wote hushirikiana na waziri mkuu anayetegemea bunge. Rais ana madaraka kadhaa pamoja na haki ya kuongoza mikutano ya mawaziri akitaka. Ana haki ya kutoa mwongozo juu ya siasa ya nje na pia ni mkuu wa jeshi. Lakini anahitaji kushiriki katika kempeni za bunge na kuomba wananchi kumpa wabunge watakoshikamana naye. Kama wananchi wanaamua tofauti anapaswa kushirikiana na waziri mkuu asiyekubali naye katika siasa. Hii ni njia mojawapo kuwapa wanachi nafasi ya kuweka mipaka kwa madaraka na uwezo wa rais wakiona asiamue kila kitu tena pekee yake.


[[Category:Siasa]]
[[Category:Siasa]]

Pitio la 11:30, 11 Septemba 2014

Aina za jamhuri duniani
*Nyekundu - Serikali ya kiraisi
*Kijani - Serikali ya raisi pamoja na athira kubwa ya bunge
*Kijani-kizeituni - Serikali ya kiraisi pamoja na waziri mkuu
*Machungwa - Serikali ya kibunge
*Kahawiya - Jamhuri zinazoruhusu chama kimoja pekee
Mengine: Ufalme au serikali ya kijeshi
Angalizi nchi mbalimbali zinazojiita "jamhuri" hutazamiwa na wengine kama udikteta. Ramani ianonyesha hali ya kisheria si hali halisi.

Serikali ya kiraisi ni muundo wa siasa ambako serikali iko mkononi wa rais wa nchi. Rais huyu anaunganisha nafasi za Mkuu wa Dola na pia kiongozi wa serikali. Muundo huu ni tofauti na serikali ya kibunge ambako rais ni zaidi cheo cha heshima tofauti na kiongozi wa serikali huchaguliwa na bunge lenye madaraka ya kumwondoa tena.

Tabia za serikali ya kiraisi

Tabia za utaratibu huu ni mara nyingi:

  • Rais ni mkuu wa dola pia kiongozi wa serikali.
  • Rais hashiriki katika bunge wala yeye si mbunge. Katika nchi kadhaa ana haki ya kupinga sheria za bunge kwa mfano Marekani. Hapa rais anaweza kusimamisha sheria za bunge kwa tamko la "veto" (Kilatini: "Nakataa"). Kura ya pili la theluthi mbili za wabunge linaweza kushinda tamko hili.
  • Rais ana kipindi maalumu kisichoongezeka.
  • Rais hawezi kuondolewa kwa tamko la bunge la kutokuwa na imani naye jinsi ilivyo na waziri mkuu katika serikali ya kibunge. Lakini kwa kawaida kuna utaratibu maalumu wa kumwondoa raisi kwa sababu za pekee, kwa mfano akionekana amevunja sheria kwa tendo la jinai.
  • Kazi ya mawaziri iko mkononi wa rais anayewapa cheo pia kuwaondoa; taratibu za nchi zatofautiana kama bunge lathebitisha mawaziri au la.

Mifano

  • Serikali za kiraise ziko kwa mfano Marekani, Meksiko, Ufilipino na nchi nyingi za Amerika Kusini pia za Afrika.
  • Kuna pia nchi za kidikteta zinazotumia muundo wa karibu na serikali ya kiraisi lakini kwa kawaida uwezo wa bunge ni mdogo sana.
  • Cheo cha rais katika serikali ya kibunge ni tofauti sana na muundo huo wa kiraisi.

Faida na hasara

Kati ya faida za utaratibu wa kiraisi hutajwa mara nyingi serikali imara mwenye nguvu ya utendaji. Kiongozi wa taifa ana nafasi kubwa kufuata siasa anayoiona ni lazima kwa mema ya nchi hata kama wabunge wameanza kusitasita au kuogopa hasira ya wananchi. Kazi ya serikali inategemea nia ya mtu mmoja aliyepewa nafasi na muda wake na wananchi wote. Anayeangaliwa ni haki yake na pia wajibu wake kutumia madaraka haya.

Nguvu hii ni pia udhaifu wa muundo huo kama rais ni mtu hafifu au mtu anayekosa uelewano mwema wa matatizo yaliyopo. Pia madaraka makubwa ya rais yameonekana kurahisisha kuundwa kwa udikteta kama huyu rais akitumia madaraka yake kubadilisha mgawanyo wa madaraka kati ya matawi ya dola yaani serikali, bunge na mahakama.

Muundo wa kumbakumba ya Serikali

Nchi mbalimbali hutumia utaratibu wa kuunganisha tabia za serikali ya kiraisi na serikali ya kibunge. Mfano wake ni Ufaransa ambako rais anayechaguliwa na wanachi wote hushirikiana na waziri mkuu anayetegemea bunge. Rais ana madaraka kadhaa pamoja na haki ya kuongoza mikutano ya mawaziri akitaka. Ana haki ya kutoa mwongozo juu ya siasa ya nje na pia ni mkuu wa jeshi. Lakini anahitaji kushiriki katika kempeni za bunge na kuomba wananchi kumpa wabunge watakoshikamana naye. Kama wananchi wanaamua tofauti anapaswa kushirikiana na waziri mkuu asiyekubali naye katika siasa. Hii ni njia mojawapo kuwapa wanachi nafasi ya kuweka mipaka kwa madaraka na uwezo wa rais wakiona asiamue kila kitu tena pekee yake.