Methali : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Addbot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 87 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q35102 (translate me)
+kubadili maelezo ya mwanzo katika makala.. Angalau maelezo ya sasa yana-mantiki!
Mstari 1: Mstari 1:
'''Methali''' ni aina ya usemi wa kisanii wa kimapokeo unaofikiriwa na [[jamii]] kuwa wa kweli na unaotumiwa kufumbia au kutolea mfano na huwa umebeba maana pana kuliko maneno yenyewe yanayotumiwa.
'''Methali''' ni usemi mfupi wa mapokeo unaodokeza kwa muhtasari fikra au mafunzo mazito yatokanayo na uzoefu wa maisha ya jamii husika. Kauli fupi yenye pande mbili za fikra.


Kila [[taifa]] na kila [[kabila]] lina methali zake, baadhi ya methali za [[Kiswahili]] ni kama: Mficha [[ugonjwa]], [[kifo]] humuumbua na mcheza kwao hutunzwa.
Kila [[taifa]] na kila [[kabila]] lina methali zake, baadhi ya methali za [[Kiswahili]] ni kama: Mficha [[ugonjwa]], [[kifo]] humuumbua na mcheza kwao hutunzwa.

Pitio la 10:27, 22 Julai 2014

Methali ni usemi mfupi wa mapokeo unaodokeza kwa muhtasari fikra au mafunzo mazito yatokanayo na uzoefu wa maisha ya jamii husika. Kauli fupi yenye pande mbili za fikra.

Kila taifa na kila kabila lina methali zake, baadhi ya methali za Kiswahili ni kama: Mficha ugonjwa, kifo humuumbua na mcheza kwao hutunzwa.

Methali za Kiswahili

Methali Maana/Matumizi Tafsiri ya Kiingereza
Asiyesikia la mkuu, huvunjika guu. Asiyefuata ushauri wa wakuu wake, mabaya humpata. He that does not heed the elderly advice, evil befalls him.
Aisifiaye mvua, ujue imemnyeshea. Mtu asifiaye jambo fulani, bila shaka ameshatambua utamu wake. He that praises rain,has seen it.
Aliye juu, mngojee chini. Anayejitapa ameshafaulu maishani, punde atafeli. Pride comes before the fall.
Usimwamshe aliyelala, utalala wewe. Usimkumbushe aliyesahau kufanya jambo fulani, maana utalisahau wewe. Do not wake one who is sleeping; you will fall asleep yourself.
Adhabu ya kaburi, aijuaye maiti. Taabu na dhiki ya kaburini,aijuaye ni maiti. Aijuaye taabu na dhiki ya jambo lolote ni yule aliyehusika nalo. The discomfort of the grave is only known by the deceased.
Kitanda usichokilalia hujui kunguni wake. Kitanda ambacho hujalala juu yake huwezi kujua kama kina kunguni wengi au kidogo, yule anachokilalia kitanda hicho ndiye ajuaye hasa adhabu ya kunguni wake. Shida inayompata mwenzio huwezi kujua taabu yake maana haikukufika wewe. You can't judge how many bugs are in a bed that you're not sleeping in.
Afadhali dooteni, kama ambari kutanda. Afadhali kibaya kidogo ulichonacho, kuliko kingi kizuri usichonacho wala huna njia ya kukipata. Hutumiwa kumnasihi mtu akinai na atoshelezeke na alichonacho, ingawaje kidogo. Better the little you own than a lot that you don't or can't archieve.

Viungo vya Nje (Methali za Kiswahili)