Yosia : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
Mstari 45: Mstari 45:
*[http://www.jewishvirtuallibrary.org/jsource/judaica/ejud_0002_0011_0_10368.html Jewish Virtual Library Josiah]
*[http://www.jewishvirtuallibrary.org/jsource/judaica/ejud_0002_0011_0_10368.html Jewish Virtual Library Josiah]


{{mtu}}
{{mbegu-mtu-Biblia}}


[[Category:Waliozaliwa 648 KK]]
[[Category:Waliozaliwa 648 KK]]

Pitio la 15:44, 18 Juni 2014

Mfalme Yosia katika ibada hekaluni

Yosia, kwa Kiebrania יֹאשִׁיָּהוּ, Yoshiyyáhu|Yôšiyyāhû, maana yake "aliyeponywa na YHWH" au "aliyetegemezwa na Yah"[1][2]; kwa Kigiriki Ιωσιας; kwa Kilatini Josias; (649 KK609 KK) alikuwa mfalme wa Yuda (641 KK – 609 KK) aliyejitahidi kufanya urekebisho upande wa dini ya Israeli ili kufuata zaidi Torati iliyoelekea kukamilika.

Familia

Mwana wa mfalme Amon na Jedidah[3], Yosia alirithi utawala akiwa mtoto wa miaka 8 tu, kutokana na uuaji wa baba yake, akatawala miaka 31,[4] kuanzia 641/640 KK to 610 KK/609 KK.[5]

Anatajwa pia katika Injili ya Mathayo kama babu wa Yesu.

Lakini nje ya Biblia hatajwi popote.[6]

Babu yake, Manase anatajwa na Biblia kama mmojawapo kati ya wafalme waovu zaidi wa ukoo wa Daudi kwa jinsi alivyoelekeza raia zake kuacha ibada ya Mungu mmoja ili kufuata dini za mataifa makuu ya wakati huo, hata kutumia Hekalu la Yerusalemu, kinyume cha uaminifu wa baba yake Hezekia.

Yosia alizaa watoto wa kiume wanne: Yohane, Eliakimu[7], Matania na Shallum.[8]

Kwanza Shallum alimrithi Yosia kwa jina la Yehoahazi.[9] lakini baada ya miezi tu nafasi yake ilishikwa na Eliakimu kwa jina la Yehoyakimu,[10] halafu na mtoto wa huyo, Yekonia;[11] hatimaye alitawala Mattania kwa jina la Zedekia.[12] Huyo akawa malme wa mwisho wa Yuda kwa kushindwa na Babuloni akapelekwa uhamishoni huko pamoja na Wayahudi wengi mwaka 586 KK.

Urekebisho

Ua wa ndani wa Hekalu la Solomoni.

Kwa miaka 13 tu (622 - 609 K.K.) Yosia alifanya urekebisho wa kidini kuanzia Yerusalemu hadi kwa mabaki ya Waisraeli wa kaskazini, akizuia wote wasiabudu miungu mingine wala wasimtolee Mungu sadaka nje ya hekalu la Yerusalemu.

Kipindi hicho mji mkuu wa Ashuru uliangamizwa alivyotabiri kwa furaha nabii Nahumu (612 hivi K.K.).

Lakini mambo yakaharibika haraka sana Yosia alipokufa vitani kabla ya wakati, kwa sababu urekebisho ulitokana zaidi na juhudi zake binafsi.

Tanbihi

  1. Josiah definition - Bible Dictionary - Dictionary.com. Retrieved 25 July 2011.
  2. Wells, John C. (1990). Longman pronunciation dictionary. Harlow, England: Longman. uk. 386. ISBN 0-582-05383-8.  entry "Josiah"
  3. "Josiah", Jewish Encyclopedia
  4. 2Fal 22:1; 2Fal 21:23-26; 2Fal 21:26
  5. Edwin Thiele, The Mysterious Numbers of the Hebrew Kings, (1st ed.; New York: Macmillan, 1951; 2d ed.; Grand Rapids: Eerdmans, 1965; 3rd ed.; Grand Rapids: Zondervan/Kregel, 1983). ISBN 0-8254-3825-X, 9780825438257, 217.
  6. Alpert, Bernard; Alpert, Fran (2012). Archaeology and the Biblical Record. Hamilton Books. uk. 74. ISBN 978-0761858355. 
  7. 2 Kings 23:34
  8. 1Nya 3:15; 2Fal 23:36; 2Fal 24:18; 2Fal 23:31
  9. 1Nya 3:15; Yer 22:11
  10. 2Nya 36:4;
  11. 2Nya 36:8
  12. 2Fal 24:17

Marejeo

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Yosia kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.