Kipindupindu : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 1: Mstari 1:
'''Kipindupindu''' (''[[ing.]] cholera'') ni ugonjwa hatari unaosababishwa na bakteria hasa katika utumbo mwembamba. Dalili zake ni kuhara sana na kutapika sana pamoja na homa kali. Kuambukizwa hutokea hasa kupitia maji au vyakula vilivyochafuliwa. Kiwango cha kuhara na kutapika kinaleta upungufu wa maji na uwiano wa chumvi mwilini. Baada ya dalili kutokea kuna hatari ya kifo kwa asilimia 20 - 70 ya wagonjwa kama hawana tiba.
'''Kipindupindu''' (kwa [[Kilatini]] na [[Kiingereza]] ''cholera'' kutoka neno la [[Kigiriki]] χολέρα, kholera, lililotokana na χολή, kholē, [[nyongo]]) ni [[ugonjwa]] hatari unaosababishwa na [[bakteria]] hasa katika [[utumbo mwembamba]].
[[Dalili]] zake ni [[kuhara]] sana na [[kutapika]] sana pamoja na [[homa]] kali. Kuambukizwa hutokea hasa kupitia [[maji]] au vyakula vilivyochafuliwa. Kiwango cha kuhara na kutapika kinaleta upungufu wa maji na uwiano wa [[chumvi]] mwilini. Baada ya dalili hizo kutokea kuna hatari ya [[kifo]] kwa [[asilimia]] 20 - 70 ya wagonjwa kama hawana [[tiba]].


[[Picha:Cholera bacteria SEM.jpg|thumb|right|Bakteria wa ''Vibrio cholerae'']]<ref name=Sherris>
[[Picha:Cholera bacteria SEM.jpg|thumb|right|Bakteria wa ''Vibrio cholerae'']]<ref name=Sherris>
Mstari 18: Mstari 20:
| isbn = 978-1-904455-33-2
| isbn = 978-1-904455-33-2
}}</ref>
}}</ref>
[[Picha:Distribution of the cholera.PNG|thumbnail|250px|Kutokea kwa kipindupindu duniani; Nyekundu: kinatokea mara kwa mara; Njano: kinatokea mara kadhaa; nyeupe: kinatokea mara chache ]]
[[Picha:Distribution of the cholera.PNG|thumbnail|250px|Kutokea kwa kipindupindu duniani; Nyekundu: kinatokea mara kwa mara; Njano: kinatokea mara kadhaa; Nyeupe: kinatokea mara chache ]]
==Ambukizo==
==Ambukizo==
Kipindupindu husababishwa na bakteria aina ya [[vibrio cholerae]] vinavyosababisha kuhara majimaji yenye rangi kama maji ya kupikia mchele. Bakteria hii ilitambuliwa mwaka 1854 na [[Filippo Pacini]]. [[Robert Koch]] alifaulu mwaka 1833 kufuga bakteria kutokana na utumbo wa wagonjwa waliokufa kipindupindu huko Misri.
Kipindupindu husababishwa na bakteria aina ya [[Vibrio cholerae]] zinazosababisha kuhara majimaji yenye rangi kama maji ya kupikia [[mchele]]. Bakteria hiyo ilitambuliwa mwaka [[1854]] na [[Filippo Pacini]]. [[Robert Koch]] alifaulu mwaka [[1883]] kufuga bakteria kutokana na [[utumbo]] wa wagonjwa waliokufa kwa kipindupindu huko [[Misri]].


Kipindupindu hutokea hasa katika nchi pasipo na maji safi hasa ambako maji ya kunywa na maji ya choo yanaweza kuchanganywa. Bakteria ya vibrio cholerae hupatikana hasa katika mavi na maji ya choo na pia katika maji ya bahari, maziwa na mito kama maji machafu huingizwa katika magimba ya maji bila kusafishwa kabla.
Kipindupindu hutokea hasa katika nchi pasipo maji safi hasa ambako maji ya kunywa na maji ya [[choo]] yanaweza kuchanganyikana. Bakteria ya vibrio cholerae hupatikana hasa katika [[mavi]] na maji ya choo na pia katika maji ya [[bahari]], ma[[ziwa]] na mito kama maji machafu huingizwa katika ma[[gimba]] ya maji bila kusafishwa kwanza.


Vilevile samaki na vyakula vingine kutoka maji yenye bakteria haya zinachafuliwa na zinaweza kusababisha ambukizo. Vilevile vyakula vinavyooshwa kwa maji yaliyochafuliwa na bakteria ya kipindupindu.
Vilevile [[samaki]] na vyakula vingine kutoka maji yenye bakteria vinachafuliwa na vinaweza kusababisha [[ambukizo]]. Vilevile vyakula vinavyooshwa kwa maji yaliyochafuliwa na bakteria ya kipindupindu.

Katika mazingira penye maji ya bomba yaliyosafishwa na karakana ya kusafisha maji machafu kipindupindu hutokea mara chache tu. Kujulikana kwa njia za kuambukizwa kulikuwa sababu ya kuanzishwa na kugharamiwa kwa teknolojia hizi katika nchi nyingi.


Katika [[mazingira]] yenye maji ya [[bomba]], yaliyosafishwa na [[karakana]] ya kusafisha maji machafu, kipindupindu hutokea mara chache tu. Kujulikana kwa njia za kuambukizwa kulikuwa sababu ya kuanzishwa na kugharamiwa kwa [[teknolojia]] hizo katika nchi nyingi.


== Matibabu ==
== Matibabu ==
[[Picha:Cholera hospital in Dhaka.jpg|thumb|right|Hospitali mjini Dhaka inayoonyesha vitanda vya wanaougua ugonjwa wa kipindupindu]]
[[Picha:Cholera hospital in Dhaka.jpg|thumb|right|[[Hospitali]] mjini [[Dhaka]] inayoonyesha vitanda vya wanaougua ugonjwa wa kipindupindu]]
1. Mgonjwa hunyweshwa maji mengi, kwa ajili mwili wake hupoteza maji mengi anapougua maradhi haya.
1. [[Mgonjwa]] hunyweshwa maji mengi, kwa sababu [[mwili]] wake hupoteza maji mengi anapougua [[maradhi]] haya.


2. Dawa zinazojulikana kufanya kazi ni kama cotrimoxazole, erythromycin, doxycycline, chloramphenicol, na furazolidone.<ref>
2. [[Dawa]] zinazojulikana kufanya kazi ni kama cotrimoxazole, erythromycin, doxycycline, chloramphenicol, na furazolidone.<ref>


{{cite web
{{cite web
Mstari 50: Mstari 51:


== Kuepukana na Kipindupindu ==
== Kuepukana na Kipindupindu ==
* wakati wowote kunawa mikono kabla ya kutayarisha au kula chakula, kusafisha vyombo kama sahani, vikombe n.k.
* kuwa na akiba ya maji yaliyochemshwa pasipo na maji safi ya bomba
* kupika chakula vizuri maana halijoto juu ya 75 °C (hadi 85 mlimani) inaua bakteria; kumenya matunda yote.
*kufunika chakula maana inzi zinapitisha bakteria kwa miguu yao
* Maji ya choo yanayotokamana na wagonjwa wa maradhi ya kipindupindu yanapasa kupitia shimo za choo zilizohifadhiwa vizuri ili kuzuia usambazaji wa bakteria. Vifaa vyote vinavyotumiwa na wagonjwa vinapaswa kuchemshwa kwa maji ya moto.
* Mikono inayoshika wagonjwa au nguo zao yanapaswa kuoshwa kwa sabuni.
* Mashimo ya choo yanapaswa kutiwa dawa za kuuwa bakteria kwa kutumia klorini.



Kinga ni kama ifuatavyo:
* wakati wowote kunawa mikono kabla ya kutayarisha au kula chakula, kusafisha vyombo kama [[sahani]], [[vikombe]] n.k.
* kuwa na [[akiba]] ya maji yaliyochemshwa pasipo na maji safi ya bomba
* kupika [[chakula]] vizuri maana [[halijoto]] juu ya 75 °C (hadi 85 mlimani) inaua bakteria;
* kumenya ma[[tunda]] yote
* kufunika chakula maana [[nzi]] wanapitisha bakteria kwa miguu yao
* maji ya choo yanayotokamana na wagonjwa wa kipindupindu yanapasa kupitia ma[[shimo]] ya choo yaliyohifadhiwa vizuri ili kuzuia [[usambazaji]] wa bakteria
* vifaa vyote vinavyotumiwa na wagonjwa vinapaswa kuchemshwa kwa maji ya moto
* mikono inayoshika wagonjwa au [[nguo]] zao inapaswa kunaniwa kwa [[sabuni]]
* mashimo ya choo yanapaswa kutiwa dawa za kuua bakteria kwa kutumia [[klorini]]


== Historia ==
== Historia ==
Mnamo mwaka 1816-1826 ndio kulikuwa na '''janga la kwanza la kipindupindu''' mjini [[Bengal]], nchini [[India]]. [[Waingereza]] 10,000 na wenyeji [[India]] walikufa.<ref>[http://www.earlyamerica.com/review/2000_fall/1832_cholera_part1.html The 1832 Cholera Epidemic in New York State], By G. William Beardslee.</ref>
Mnamo miaka [[1816]]-[[1826]] kulikuwa na '''[[janga]] la kwanza la kipindupindu''' mkoani [[Bengal]], nchini [[India]]. [[Waingereza]] 10,000 na [[Wahindi]] walikufa.<ref>[http://www.earlyamerica.com/review/2000_fall/1832_cholera_part1.html The 1832 Cholera Epidemic in New York State], By G. William Beardslee.</ref>


Janga la '''pili la kipindupindu''' lilikuwa mnamo 1829-1851 iliyoenea nchini [[Urusi]], [[Hungaria]], [[Ujerumani]] na [[London]]. Zaidi ya watu 55,000 walikufa kutoka Uingereza.<ref>[http://www.ph.ucla.edu/EPI/snow/pandemic1826-37.html Asiatic Cholera Pandemic of 1826-37].</ref> Mwaka wa 1831, watu 150,000 walikufa kutokana na janga hili nchini [[Misri]].<ref>[http://whqlibdoc.who.int/bulletin/1947-1948/Vol1-No2/bulletin_1948_1(2)_353-381.pdf Cholera Epidemic in Egypt (1947)].</ref>
Janga la '''pili la kipindupindu''' lilikuwa mnamo [[1829]]-[[1851]] kilipoenea nchini [[Urusi]], [[Hungaria]], [[Ujerumani]] na [[Uingereza]]. Zaidi ya watu 55,000 walikufa kutoka Uingereza pekee.<ref>[http://www.ph.ucla.edu/EPI/snow/pandemic1826-37.html Asiatic Cholera Pandemic of 1826-37].</ref> Mwaka [[1831]], watu 150,000 walikufa kutokana na janga hili nchini [[Misri]].<ref>[http://whqlibdoc.who.int/bulletin/1947-1948/Vol1-No2/bulletin_1948_1(2)_353-381.pdf Cholera Epidemic in Egypt (1947)].</ref>


Mwaka wa 1849, kipindupindu ilizuka tena kwa mara ya pili mjini [[Paris]].<ref>[http://www.oocities.com/CapitolHill/Congress/2807/irishfamine.html The Irish Famine].</ref> Mjini [[London]], watu 14,137 walikufa.
Mwaka [[1849]], kipindupindu kilizuka tena kwa mara ya pili mjini [[Paris]].<ref>[http://www.oocities.com/CapitolHill/Congress/2807/irishfamine.html The Irish Famine].</ref> Mjini [[London]] watu 14,137 walikufa.


Miaka ya 1961-1970: kulikuwa na janga lingine la kipindupindu nchini [[Indonesia]]. Ilianzia [[Afrika Kaskazini]] na kuenea hadi nchi ya [[Italia]]. Katika miaka ya 1970, watu kidogo waliathirika nchini [[Ujapani]].
Miaka ya [[1961]]-[[1970]]: kulikuwa na janga lingine la kipindupindu nchini [[Indonesia]]. Ilianzia [[Afrika Kaskazini]] na kuenea hadi nchi ya [[Italia]]. Katika [[miaka ya 1970]], watu waliathirika kidogo nchini [[Ujapani]].


Mnamo 1991-1994 kulikuwa na janga lingine nchini [[Marekani ya Kusini]], iliyosababishwa na meli iliyomwaga maji machafu. Mjini [[Peru]], watu takriban 10,000 waliuawa.
Mnamo [[1991]]-[[1994]] kulikuwa na janga lingine huko [[Amerika Kusini]], lililosababishwa na [[meli]] iliyomwaga maji machafu. Nchini [[Peru]] watu takriban 10,000 waliuawa.


Mwaka wa 2000, wagonjwa 14000 waliripotiwa kuugua kutokana na kipindupindu. Takriban 87% waliripotiwa kutoka bara la [[Afrika]].<ref>[http://www.worldwaterday.org/wwday/2001/disease/cholera.html Disease fact sheet: Cholera]. IRC International Water and Sanitation Centre.</ref>
Mwaka [[2000]], wagonjwa 14,000 waliripotiwa kuugua kutokana na kipindupindu. Takriban 87% waliripotiwa kutoka bara la [[Afrika]].<ref>[http://www.worldwaterday.org/wwday/2001/disease/cholera.html Disease fact sheet: Cholera]. IRC International Water and Sanitation Centre.</ref>


Julai - Desemba 2007: ukame wa maji safi ya kunywa nchini [[Irak]] ilisababisha janga la [[Kipindupindu]].<ref>{{cite news |first= |last= |authorlink= |author= |coauthors= |title=U.N. reports cholera outbreak in northern Iraq |url=http://www.cnn.com/2007/WORLD/meast/08/29/iraq.cholera/index.html |work= |publisher=CNN |id= |pages= |page= |date= |accessdate=2007-08-30 |quote= }}</ref> Watu 22 walifariki.<ref>[http://www.guardian.co.uk/world/2007/dec/02/iraq.davidsmith Cholera crisis hits Baghdad], The Observer, 2 Desemba 2007.</ref>
Julai - Desemba [[2007]]: [[ukame]] wa [[maji salama]] kwa ajili ya kunywa nchini [[Irak]] ulisababisha tena janga la kipindupindu.<ref>{{cite news |first= |last= |authorlink= |author= |coauthors= |title=U.N. reports cholera outbreak in northern Iraq |url=http://www.cnn.com/2007/WORLD/meast/08/29/iraq.cholera/index.html |work= |publisher=CNN |id= |pages= |page= |date= |accessdate=2007-08-30 |quote= }}</ref> Watu 22 walifariki.<ref>[http://www.guardian.co.uk/world/2007/dec/02/iraq.davidsmith Cholera crisis hits Baghdad], The Observer, 2 Desemba 2007.</ref>


Mnamo Agosti 2007 mjini Orissa, India. Zaidi ya watu 2,000 walilazwa hospitalini.<ref>[http://news.bbc.co.uk/2/hi/south_asia/6968281.stm Cholera death toll in India rises], BBC News.</ref>
Mnamo Agosti [[2007]] jimboni [[Orissa]], [[India]], zaidi ya watu 2,000 walilazwa hospitalini.<ref>[http://news.bbc.co.uk/2/hi/south_asia/6968281.stm Cholera death toll in India rises], BBC News.</ref>


Machi - Aprili 2008: Watu 2,490 walilazwa hospitalini mjini [[Vietnam]] kutokamana na janga la kipindupindu.<ref>[http://www.who.int/cholera/countries/VietNamCountryProfile2008.pdf Cholera Country Profile: Vietnam]. WHO.</ref>
Machi - Aprili [[2008]]: watu 2,490 walilazwa hospitalini nchini [[Vietnam]] kutokana na janga la kipindupindu.<ref>[http://www.who.int/cholera/countries/VietNamCountryProfile2008.pdf Cholera Country Profile: Vietnam]. WHO.</ref>


== Waathirika Maarufu ==
== Waathirika maarufu ==
George Bradshaw
*[[George Bradshaw]]
Nicolas Léonard Sadi Carnot
*[[Nicolas Léonard Sadi Carnot]]
Charles X of France
*[[Charles X wa Ufaransa]]
Juan de Veramendi
*[[Juan de Veramendi]]
John Blake Dillon
*[[John Blake Dillon]]
Alexandre Dumas, père, mwandishi wa Kifaransa aliyeandika kitabu cha The Three Musketeers
*[[Alexandre Dumas mzee]], [[mwandishi]] wa [[Kifaransa]] aliyeandika [[kitabu]] "The Three Musketeers"
Mary Abigail Fillmore, mtoto wa rais wa Marekani: Millard Fillmore
*Mary Abigail Fillmore, [[mtoto]] wa [[rais]] wa [[Marekani]] [[Millard Fillmore]]
James K. Polk, rais wa kumi na moja wa Marekani
*[[James K. Polk]], rais wa kumi na moja wa Marekani
Pedro V, Mfalme wa nchi ya Portugal
*[[Pedro V]], [[Mfalme]] wa [[Ureno]]


== Marejeo ==
== Tanbihi ==
{{Marejeo}}
{{Marejeo}}


==Viungo vya nje==
*[http://kenya.thebeehive.org/sw/content/124/965 Maelezo ya kipindupindu na namna za kuikinga kwenye beehive.com (swa.)]
*[http://kenya.thebeehive.org/sw/content/124/965 Maelezo ya kipindupindu na namna za kujikinga kwenye beehive.com (swa.)]

[[Jamii:Biolojia]]
[[Jamii:Biolojia]]
[[Jamii:Maradhi]]

Pitio la 13:40, 16 Juni 2014

Kipindupindu (kwa Kilatini na Kiingereza cholera kutoka neno la Kigiriki χολέρα, kholera, lililotokana na χολή, kholē, nyongo) ni ugonjwa hatari unaosababishwa na bakteria hasa katika utumbo mwembamba.

Dalili zake ni kuhara sana na kutapika sana pamoja na homa kali. Kuambukizwa hutokea hasa kupitia maji au vyakula vilivyochafuliwa. Kiwango cha kuhara na kutapika kinaleta upungufu wa maji na uwiano wa chumvi mwilini. Baada ya dalili hizo kutokea kuna hatari ya kifo kwa asilimia 20 - 70 ya wagonjwa kama hawana tiba.

Bakteria wa Vibrio cholerae

[1][2]

Kutokea kwa kipindupindu duniani; Nyekundu: kinatokea mara kwa mara; Njano: kinatokea mara kadhaa; Nyeupe: kinatokea mara chache

Ambukizo

Kipindupindu husababishwa na bakteria aina ya Vibrio cholerae zinazosababisha kuhara majimaji yenye rangi kama maji ya kupikia mchele. Bakteria hiyo ilitambuliwa mwaka 1854 na Filippo Pacini. Robert Koch alifaulu mwaka 1883 kufuga bakteria kutokana na utumbo wa wagonjwa waliokufa kwa kipindupindu huko Misri.

Kipindupindu hutokea hasa katika nchi pasipo maji safi hasa ambako maji ya kunywa na maji ya choo yanaweza kuchanganyikana. Bakteria ya vibrio cholerae hupatikana hasa katika mavi na maji ya choo na pia katika maji ya bahari, maziwa na mito kama maji machafu huingizwa katika magimba ya maji bila kusafishwa kwanza.

Vilevile samaki na vyakula vingine kutoka maji yenye bakteria vinachafuliwa na vinaweza kusababisha ambukizo. Vilevile vyakula vinavyooshwa kwa maji yaliyochafuliwa na bakteria ya kipindupindu.

Katika mazingira yenye maji ya bomba, yaliyosafishwa na karakana ya kusafisha maji machafu, kipindupindu hutokea mara chache tu. Kujulikana kwa njia za kuambukizwa kulikuwa sababu ya kuanzishwa na kugharamiwa kwa teknolojia hizo katika nchi nyingi.

Matibabu

Hospitali mjini Dhaka inayoonyesha vitanda vya wanaougua ugonjwa wa kipindupindu

1. Mgonjwa hunyweshwa maji mengi, kwa sababu mwili wake hupoteza maji mengi anapougua maradhi haya.

2. Dawa zinazojulikana kufanya kazi ni kama cotrimoxazole, erythromycin, doxycycline, chloramphenicol, na furazolidone.[3] 3. Chanjo za kuzuia Kipindipindu hutolewa katika baadhi za nchi.[4]

Kuepukana na Kipindupindu

Kinga ni kama ifuatavyo:

  • wakati wowote kunawa mikono kabla ya kutayarisha au kula chakula, kusafisha vyombo kama sahani, vikombe n.k.
  • kuwa na akiba ya maji yaliyochemshwa pasipo na maji safi ya bomba
  • kupika chakula vizuri maana halijoto juu ya 75 °C (hadi 85 mlimani) inaua bakteria;
  • kumenya matunda yote
  • kufunika chakula maana nzi wanapitisha bakteria kwa miguu yao
  • maji ya choo yanayotokamana na wagonjwa wa kipindupindu yanapasa kupitia mashimo ya choo yaliyohifadhiwa vizuri ili kuzuia usambazaji wa bakteria
  • vifaa vyote vinavyotumiwa na wagonjwa vinapaswa kuchemshwa kwa maji ya moto
  • mikono inayoshika wagonjwa au nguo zao inapaswa kunaniwa kwa sabuni
  • mashimo ya choo yanapaswa kutiwa dawa za kuua bakteria kwa kutumia klorini

Historia

Mnamo miaka 1816-1826 kulikuwa na janga la kwanza la kipindupindu mkoani Bengal, nchini India. Waingereza 10,000 na Wahindi walikufa.[5]

Janga la pili la kipindupindu lilikuwa mnamo 1829-1851 kilipoenea nchini Urusi, Hungaria, Ujerumani na Uingereza. Zaidi ya watu 55,000 walikufa kutoka Uingereza pekee.[6] Mwaka 1831, watu 150,000 walikufa kutokana na janga hili nchini Misri.[7]

Mwaka 1849, kipindupindu kilizuka tena kwa mara ya pili mjini Paris.[8] Mjini London watu 14,137 walikufa.

Miaka ya 1961-1970: kulikuwa na janga lingine la kipindupindu nchini Indonesia. Ilianzia Afrika Kaskazini na kuenea hadi nchi ya Italia. Katika miaka ya 1970, watu waliathirika kidogo nchini Ujapani.

Mnamo 1991-1994 kulikuwa na janga lingine huko Amerika Kusini, lililosababishwa na meli iliyomwaga maji machafu. Nchini Peru watu takriban 10,000 waliuawa.

Mwaka 2000, wagonjwa 14,000 waliripotiwa kuugua kutokana na kipindupindu. Takriban 87% waliripotiwa kutoka bara la Afrika.[9]

Julai - Desemba 2007: ukame wa maji salama kwa ajili ya kunywa nchini Irak ulisababisha tena janga la kipindupindu.[10] Watu 22 walifariki.[11]

Mnamo Agosti 2007 jimboni Orissa, India, zaidi ya watu 2,000 walilazwa hospitalini.[12]

Machi - Aprili 2008: watu 2,490 walilazwa hospitalini nchini Vietnam kutokana na janga la kipindupindu.[13]

Waathirika maarufu

Tanbihi

  1. Ryan KJ, Ray CG (editors) (2004). Sherris Medical Microbiology (toleo la 4th). McGraw Hill. ku. 376–7. ISBN 0838585299. 
  2. Faruque SM; Nair GB (editors) (2008). Vibrio cholerae: Genomics and molecular biology. Caister Academic Press. ISBN 978-1-904455-33-2. 
  3. "Cholera treatment". Molson Medical Informatics. 2007. Iliwekwa mnamo 2008-01-03. 
  4. "Is a vaccine available to prevent cholera?". CDC disease info: Cholera. Iliwekwa mnamo 2008-07-23. 
  5. The 1832 Cholera Epidemic in New York State, By G. William Beardslee.
  6. Asiatic Cholera Pandemic of 1826-37.
  7. Cholera Epidemic in Egypt (1947).
  8. The Irish Famine.
  9. Disease fact sheet: Cholera. IRC International Water and Sanitation Centre.
  10. "U.N. reports cholera outbreak in northern Iraq", CNN. Retrieved on 2007-08-30. 
  11. Cholera crisis hits Baghdad, The Observer, 2 Desemba 2007.
  12. Cholera death toll in India rises, BBC News.
  13. Cholera Country Profile: Vietnam. WHO.

Viungo vya nje