Tumbaku : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
o>u kufuatana na mwalimu Muddy
d Kipala alihamisha ukurasa wa Tumbako hadi Tumbaku
(Hakuna tofauti)

Pitio la 16:32, 3 Juni 2014

Majani ya tumbaku yaliyokatwa tayari kwa kanda nyembamba sana, tayari kwa kutengeneza sigara

Tumbaku (wakati mwingine pia tumbako) ni majani makavu ya mmea wa mtumbaku ambayo yanatumiwa na binadamu kwa kuvuta kama sigara, kutafuniwa mdomoni au tumbaku ya kunusa. Tumbaku huwa ndani yake kemikali ya nikotini ambayo mwili unazoea haraka sana na kuifanya vigumu kwa wavuta tumbaku kuachana na desturi hii.

Asili ya tumbaku

Asili ya tumbaku iko katika Amerika ambako Maindio wenyeji waliitumia kama dawa la kidini pia la burudani. Tangu Kolumbus Wahispania walipeleka mtumbaku hadi Ulaya ambako uliangaliwa mwanzoni kama mmea wa kiganga. Matumizi hasa kwa njia ya kuvuta na kutafuna yalienea haraka katika Ulaya na kwa njia ya mabaharia Wareno katika pande zote za dunia.

Shamba la tumbaku nchini Kuba

Kazi ya nikotini ndani ya tumbaku

Tumbaku inavutiwa hasa kwa sababu nikotini ambayo ni dawa ndani yake inaathiri ubongo na neva ya binadamu na kupunguza uchovu na kusaidia mtu kusikia utulivu na raha. Tofauti na madawa mengine kama alikoholi, bhangi au afyuni yanayoathiri pia ubongo na neva tumbaku haisababishi hali ya ulevi. Lakini inasababisha haraka uzoefu wa mwili unaoshikwa na hamu ya kupata nikotini tena na tena. Hapo ni vigumu kwa watu walioanza kutumia tumbaku mara kwa mara uachana na matumizi yake.

Hatari za kiafya

Matumizi ya tumbaku yamegunduliwa kuwa kati ya sababu kuu zinazosababisha magonjwa mengi kwa binadamu pamoja na kansa, magonjwa ya moyo na mapafu, na mengine. Magonjwa haya hayasababishwi na nikotini lakini na desturi ya kuvuta tumbaku. Moshi ya majani ya tumbaku huwa na maelfu ya kemikali ndani yake ni hasa kemikali hizi zinazovutwa ndani ya mwili wakati wa kuvuta ambazo ngozi ndani ya mwili, mishipa, moyo na mapavu. Kwa hiyo nikotini inamlazimisha mvutaji kuvuta tena na tena na hivyo kuingiza mwilini kemikali nyingi zenye hasara.

Matumizi ya tumbaku nje ya kuvuta (kutafuna, kunusa) yamegundunduliwa kupunguza hatari za kiafya lakini inaleta matatizo yaleyale ya kutegemea nikotini na kutoachana nayo.

Nchi zilizolima zaidi ya tani 100,000 za tumbaku mwaka 2000

Kilimo

Kilimo cha tumbaku ni tawi muhimu la uchumi kwa nchi mbalimbali. Kilwa mavuno ya duniani ni takriban tani milioni 6.7. Wazalishaji wakuu ni China (39.6%), Uhindi (8.3%), Brazil (7.0%) na Marekani (4.6%). [1] Tanzania ni kati ya nchi kumi za kwanza zinazolima tumbaku inavuna asilimia 1.6 ya tumbaku ya dunia.[2]

Katika nchi zilizoendelea kilimo cha tumbaku kimepungua na kiasi cha China kumeongezeka.

Majani ya tumbaku wakati wa kukauka

Baada ya mavuno

Mavuno hutokea siku 70 hadi 130 baada ya kulima shamba. Majani huvuniwa wakati majani yanaanza kuonyesha rangi ya manjano maana yameiva. Mavuno yanaenda kwa uangalifu kwa sababu mashimo katika majani yanapunguza ubora na bei, Baada ya mavuno majani yanafungwa pamoja kwa kamba na kukaushwa. Kuna mbinu za kuzikausha polepole kivulini au juu ya moto au penye hewa ya moto haraka katika muda wa siku chache tu.

Majani yaliyokauka hufungwa pamoja kwa mchakato wa kuchachua. Huu unabadilisha ladha ya tumbaku kwa njia inayotakiwa. Baadaye tumbaku hutiwa sosi zenye sukari au vitu vingine vya kutia ladha halafu kukatwa na kufungwa kulingana na matumizi kama tumbaku ya kuvuta katika sigara za kawaida, sigara kubwa, pipo, ya kutafunia au ya kunusu.


Marejeo

  1. US Census Bureau-Foreign Trade Statistics, (Washington DC; 2005)
  2. http://www.factfish.com/statistic-country/tanzania/tobacco,+production+quantity