Vitenzi vishirikishi vikamilifu : Tofauti kati ya masahihisho
Ukurasa ulianzishwa kwa kuandika '{{ExamplesSidebar|35%| *Sada ali'''kuwa''' mtoro shuleni *Mahmoud '''ni''' mchokozi *Mahmoud '''si''' mchokozi *Mariam '''ana''' gari zuri *Ndoo '''imo''' kisim...' |
No edit summary |
||
Mstari 6: | Mstari 6: | ||
*Ndoo '''imo''' kisimani |
*Ndoo '''imo''' kisimani |
||
}} |
}} |
||
'''Vitenzi vishirikishi vikamilifu''' (alama yake ya [[isimu|kiisimu]] ni: '''t''') ni maneno ambayo yamekamilika, yaani, hayaambatanishwi na mofimu/ '''kiambishi''' / '''silabi''' / '''neno''' au kitenzi kingine. Vitenzi hivi pia hugawanyika katika makundi madogomadogo. |
'''Vitenzi vishirikishi vikamilifu''' (alama yake ya [[isimu|kiisimu]] ni: '''t''') ni maneno ambayo yamekamilika, yaani, hayaambatanishwi na mofimu/ '''kiambishi''' / '''silabi''' / '''neno''' au [[Kitenzi kishirikishi|kitenzi kingine]]. Vitenzi hivi pia hugawanyika katika makundi madogomadogo. |
||
==Uchambuzi== |
==Uchambuzi== |
Pitio la 14:12, 16 Aprili 2014
Mifano |
---|
|
Vitenzi vishirikishi vikamilifu (alama yake ya kiisimu ni: t) ni maneno ambayo yamekamilika, yaani, hayaambatanishwi na mofimu/ kiambishi / silabi / neno au kitenzi kingine. Vitenzi hivi pia hugawanyika katika makundi madogomadogo.
Uchambuzi
Kuna mizizi sita ya vitenzi vishirikishi vikamilifu.
(i) -KUWA
Endapo utakuwa na kitenzi cha mzizi wa -kuwa kimesimama/kimekaa peke yake katika sentensi na kimetoa taarifa kamili - basi hicho ni kitenzi kishirikishi.
- Mifano
- Sada alikuwa mtoro shuleni
- Wanjiru atakuwa mgeni rasmi
- Nguruka amekuwa mshindi wetu
- Anna alikuwa mwimbaji hodari
- Mohamed hakuwa mlevi
- Sisi tutakuwa wanafunzi bora
(ii) NI
Hiki ni kitenzi kishirikishi kinachojulisha uyakinishi wa tendo. Kitenzi hiki hujulisha kuwepo kwa uhusiano baina ya vipashio vya lugha.
- Mifano
- Mahmoud ni mchokozi
- Tembo ni mnyama mkali
- Wanjau ni mwanafunzi mtiifu
- Anna ni mwimbaji hodari
(iii) SI
Hiki ni kitenzi kishirikishi kinachojulisha ukanushi wa tendo. Kitenzi hiki hujulisha kuwepo kwa uhusiano baina ya vipashio vya lugha.
- Mifano
- Mahmoud si mchokozi
- Tembo si mnyama mkali
- Wanjau si mwanafunzi mtiifu
- Anna si mwimbaji hodari
Hivi ni vitenzi vinavyotoa taarifa ya umiliki kwa nomino au kiwakilishi.
- Mifano
- Mariam ana gari zuri
- Chakuna kina chumvi nyingi
- Ulimi hauna mfupa
- Husna ana mme mzuri
- Darasa letu lina vumbi
- Chatu hana meno
(v) Vitenzi vishirikishi vya viambishi vya mahali (po, mo, ko)
Hivi ni vitenzi vinavyotoa taarifa ya mazingira ya tendo husika. Mazingira hayo ni pamoja na kuwa nje, ndani, juu ya, au katika eneo fulani.
- Mifano
- Ndoo imo kisimani
- Kikombe kiko mezani
- Wanafunzi wamo darasani
- Yeye yumo chumbani
- Fedha zimo kabatani
- Jembe lipo shambani
(vi) Kitenzi kishirikishi chaa viambishi vya ngeli vikisimama peke yake
Hivi ni vitenzi vinavyobainisha maana ya ngeli ikisimama peke yake.
- Mifano
- Ndoo i kisimani
- Kikombe ki mezani
- Wanafunzi wa darasani (hapa ni lazima sauti ibadilike ili kutoa maana tofauti na ile maana ya kiwakilishi/kivumishi cha -a unganifu). Bimaana ya kwamba wakati unataja wanafunzi wa - kwenye wa lazima ufanye kama unasimama vile...
- Yeye yu chumbani
- Fedha zi kabatani
- Jembe li shambani
Tazama pia
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Vitenzi vishirikishi vikamilifu kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |