Mkoa wa Dodoma : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
No edit summary
No edit summary
Mstari 11: Mstari 11:
|align=center | 1. || align=center | Dodoma Kijijini || align=center | 14,004 || align=center | 484,249
|align=center | 1. || align=center | Dodoma Kijijini || align=center | 14,004 || align=center | 484,249
|-----
|-----
|align=center | 2. || align=center | Dodoma Mjini || align=center | 4,041 || align=center | 280,781
|align=center | 2. || align=center | [[Dodoma mjini]] || align=center | 4,041 || align=center | 280,781
|-----
|-----
|align=center | 3. || align=center | [[Kondoa]] || align=center | 2,576 || align=center | 450,400
|align=center | 3. || align=center | [[Kondoa]] || align=center | 2,576 || align=center | 450,400

Pitio la 15:01, 2 Mei 2006

Mkoa wa Dodoma uko katikati ya Tanzania umepakana na mikoa ya Manyara, Morogoro, Iringa na Singida. Sehemu kubwa ya eneo lake ni nyanda za juu kati ya mita 830 hadi 2000 juu ya UB.

Eneo lote la mkoa lina 41,310 km². Kuna wilaya tano zifuatazo:

Wilaya za Mkoa wa Dodoma
Na. Wilaya Eneo (km²) Wakazi (2001)
1. Dodoma Kijijini 14,004 484,249
2. Dodoma mjini 4,041 280,781
3. Kondoa 2,576 450,400
4. Mpwapwa 13,210 249,856
5. Kongwa 7,479 228,352
Jumla Mkoa wa Dodoma 41,310 1,693,638

Mawasiliano

Mawasiliano ni mazuri kwa barabara ya lami kuanzia Dodoma mjini kwenda Morogoro - Daressalaam, barabara zingine ni za udongo to pamoja na njia kuu kuelekea Tanzania ya Magharibi - Rwanda - Kongo. Pia hali ya barabara ya kale ya "Cape - Cairo" inayovuka Dodoma kutoka kazkazini (Arusha - Kondoa) kwenda kusini si nzuri tena. Kuna pia njia ya Reli ya Kati kutoka Daressalaam kwenda Kigoma yenye matatizo ya mara kwa mara. Dodoma mjini kuna uwanja wa kitaifa wa ndege.

Hali ya hewa na kilimo

Kwa jumla Dodoma haina mvua nyingi isipokuwa sehemu za wilaya za Mpwapwa na Kondoa. Hivyo hasa mazao yasiyotegemea sana mvua hulimwa kama vile mtama, wimbi, muhogo; kilimo cha mahindi hupatikana mara kwa mara na matatizo ya kukosa mvua. Mazao ya sokoni ni karanga alizeti na simsim. Dodoma ni pia mwanzo wa ustawishaji wa mizabibu na uzalishaji wa divai katika Tanzania.

Kutokana na hali ya hewa mifugo ni mingi (ng'ombe 1,600,000, mbuzi 954,000, kondoo 274,000, nguruwe 23,000, kuku takriban 1,400,000). Idadi ya mifugo imeongeza tatizo la mmomonyoko wa ardhi katika sehemu za Mkoa wa Dodoma.

Wakazi na utamaduni

Idadi kubwa ya wakazi asilia ni Wagogo. Kondoa kuna Wangulu na pia Wasandawe wanaotumia lugha ya aina ya Khoikhoi. Wanasemekana ya kwamba babu zao wamewahi kukaa eneo la Tanzania kabla ya kuingia kwa Wabantu. Kondoa kuna pia sehemu penye michoro ya kale juu ya uso ya miamba ya aina ya Khoikhoi inayofanana na sanaa ya kale huko Zimbabwe au Afrika Kusini.