Wapangwa : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Addbot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 3 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q3847550 (translate me)
No edit summary
Mstari 11: Mstari 11:

Mavazi yao ya asili ni nguo zilitengenezwa kwa ngozi za wanyama pamoja na magome ya miti ya misambi ambayo hupondwapondwa,hufumwa na kupakwa mono.
Mavazi yao ya asili ni nguo zilitengenezwa kwa ngozi za wanyama pamoja na magome ya miti ya misambi ambayo hupondwapondwa,hufumwa na kupakwa mono.

Lugha yao ni [[Kipangwa]].
Lugha yao ni [[Kipangwa]].

(ADDITION, BY LEWIS LINUS WILLIHEM WILLAH, E-MAIL ADDRESS, willahlewis@yahoo.com), Wapangwa wamekusanyika pamoja hasa katika maeneo ya Ludewa(Madunda, Mawengi, Mlangali,Masimbwe, Mkiu, Ulayasi, Lupanga, Madilu, n.k) kuelekea Njombe. Chanzo cha wao kuwa karibukaribu kiukoo, ni Vita, maana wao walitokea katika maeneo mbalimbali, kama vile Malawi na Msumbiji, kwa ajili ya [vita].
== Viungo vya Nje ==
== Viungo vya Nje ==
[http://www.ethnologue.com/show_language.asp?code=pbr Ethnologue]
[http://www.ethnologue.com/show_language.asp?code=pbr Ethnologue]

Pitio la 09:05, 22 Juni 2013

Wapangwa ni kabila kutoka Milima Livingstone karibu na pwani ya mashariki ya Ziwa Nyasa, wilaya ya Ludewa, Mkoa wa Njombe, kusini ya nchi ya Tanzania. Mwaka 2002 idadi ya Wapangwa ilikadiriwa kuwa 150,000.

Chakula chao ni ugali wa mahindi, ulezi na mtama kidogo. Kitoweo cha vyakula hivyo ni maharage, samaki, nyama na jamii ya mboga mboga. Kinywaji chao ni pombe (ukhimbi) yaani kangala, komoni, ulanzi ambao hugemwa kutoka katika mmea uitwao mlanzi. Pia Wapangwa ni hodari sana kwa utegaji na uwindaji wa wanyama pori kama vile ( kwa lugha yao) Nyhaluchi,mahtu ngwehe, sudi,ng'ese,ng'wali ni videke.

Hulima mazao mbalimbali ya chakula katika maeneo ya miinuko na mabondeni kandokando ya mito.Hulima kwa ushirika unaoitwa njhiika.Pia ni wafugaji wa makundi madogomadogo ya ng'ombe, mbuzi, kondoo na nguruwe (kitimoto). Pia hulima mazao ya biashara kama kahawa, chai, pareto, mahindi. Kabila hili pia hupata matunda ya asili kama vile; masada, savula, makuhu, mahofita,mafudo, minhingi, vudong'o na nisongwa.

Usafiri wao wa asili ni kwa chombo kiitwacho ngwichili ambacho kinatengenezwa kwa kutumia miti asilia.

Nyumba zao za asili kwa sasa ni za matofali ya udongo ya kuchoma na kuezekwa kwa bati, hata hivyo nyumba zao za asili zinajengwa kwa kutumia miti asili kugandikwa kwa udongo wa mfinyanzi na kuezekwa kwa nyasi aina ya hunji na lihanu.

Mavazi yao ya asili ni nguo zilitengenezwa kwa ngozi za wanyama pamoja na magome ya miti ya misambi ambayo hupondwapondwa,hufumwa na kupakwa mono.

Lugha yao ni Kipangwa.

               (ADDITION, BY LEWIS LINUS WILLIHEM WILLAH, E-MAIL ADDRESS, willahlewis@yahoo.com), Wapangwa wamekusanyika pamoja hasa katika maeneo ya Ludewa(Madunda, Mawengi, Mlangali,Masimbwe, Mkiu, Ulayasi, Lupanga, Madilu, n.k) kuelekea Njombe. Chanzo cha wao kuwa karibukaribu kiukoo, ni Vita, maana wao walitokea katika maeneo mbalimbali, kama vile Malawi na Msumbiji, kwa ajili ya [vita].

Viungo vya Nje

Ethnologue

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wapangwa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.