Elki : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Addbot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 1 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q35517 (translate me)
d ChriKo moved page Muusi to Elki over redirect: Jina "elki" linatoka jina la Kiingereza "elk" ambalo ni jina la zamani zaidi kuliko "moose".
(Hakuna tofauti)

Pitio la 16:29, 27 Machi 2013

Muusi
Muusi (Alces alces)
Muusi (Alces alces)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mammalia (Wanyama wenye viwele)
Oda: Artiodactyla (Mamalia wanaokanyaga kwa kwato mbili-mbili)
Familia: Cervidae (Wanyama walio na mnasaba na kulungu)
Nusufamilia: Capreolinae (Wanyama wanaofanana na kulungu wa Dunia Mpya)
Jenasi: Alces
J.E. Gray, 1821
Spishi: A. alces
Linnaeus, 1758

Muusi (kutoka Kiing.: moose, Amerika Kaskazini) au elki wa Ulaya (kutoka Kiing.: elk, Ulaya) (Kilat.: Alces alces) ni spishi kubwa inayoishi ya familia ya kulungu. Muusi wanajulikana kwa vichwa vyao vikubwa na mashada yao ya pembe zinazogawanyika kama vidole vya kiganja; spishi nyingine za familia huwa na mashada ya pembe zinazogawanyika katika matawi. Kwa kawaida muusi huishi misituni mwa kaskazini na misitu yenye miti ya kupukutika majani yake ya Nusudunia ya Kaskazini katika hali za nchi za wastani hadi maeneo ya chini ya Aktiki. Kutokana na uwindaji, muusi wana makazi madogo zaidi. Sasa muusi wengi wanapatikana Kanada, Alaska, Skandinavia na Urusi. Wao hula mimea ya ardhini na majini. Wanyama ambao huwinda muusi ni mbwa-mwitu, dubu na binadamu. Tofauti na spishi zingine za kulungu, muusi ni wanyama pweke na huwa hawaishi na kundi la muusi wengine. Ingawa muusi kwa kawaida hutembea polepole, wakasirishwapo muusi waweza kuwa mkali na kusonga haraka. Wakati wa demani iliye majira yao ya kupandana, madume wa spishi hupigana na madume wengine na kumshindania jike.

Etimolojia na jina

Muusi mwenye jina la kisayansi Alces alces hujulikana kama elk "elki" katika Uingereza, na Amerika Kaskazini kama moose "muusi".

Jina la Kiingereza cha Kibritania linatoka lugha zingine za Kihindi-Kizungu, kwa mfano, elg kwa Kideni/Kinorwe, älg kwa Kiswidi, Elch kwa Kijerumani na łoś kwa Kipoli. Hata hivyo, katika Amerika Kaskazini neno la elk "elki" hutumika ili kurejelea mnyama tofauti, elki wa Kanada au pia huitwa wapiti (Cervus canadensis) ambaye ni mdogo zaidi na kisanaba tofauti na kulungu mwekundu wa Ulaya wa kati na magharibi.

Neno la moose kwanza liliingia Kiingereza mwaka wa 1606, na hutoka lugha za Kialgonkini (Kinarragansett moos na Kiabenaki cha Mashariki mos).

Muusi dume aliyekua hurejelewa kama fahali, na muusi jike ni dachia, na mtoto wa muusi ni ndama.

Makazi na eneo

Amerika Kaskazini

Katika Amerika Kaskazini, muusi huishi Kanada (mbali na Aktiki), Alaska, Uingereza Mpya, Milima yenye Miamba, Minesota, Peninsula ya Juu ya Michigan na Kijisiwa cha Kifalme cha Ziwa Kubwa. Katika eneo hili kubwa, kuna nususpishi zingi. Katika magharibi ya bara ya Amerika Kaskazini, idadi za muusi zinafikia kaskazini mwa Kanada (Kolumbia ya Kibritania na Alberta) na spishi wengine wamepatikana milimani mwa Utah na Kolorado.

Ulaya

Katika Ulaya, muusi wanapatikana katika Unorwe, Uswidi, Ufini, Urusi, Upoli na nchi za Kibaltiki, na muusi wachache katika Ucheki, Belarusi na Ukraini.