Nishati : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Addbot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 119 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q11379 (translate me)
Addbot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 1 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q11379 (translate me)
Mstari 72: Mstari 72:


[[Jamii:Fizikia]]
[[Jamii:Fizikia]]

[[fr:Énergie (physique)]]

Pitio la 03:25, 21 Machi 2013

Nishati inamaanisha uwezo wa kufanya kazi na kusababisha mabadiliko. Katika sayansi nishati hupimwa kwa kipimo cha SI joule.

Katika sayansi lina mtizamo wa kipekee.

Radi ni uvunjiko wa nguvu za kiumeme katika hewa unaotokana na uwindi umeme mkali(kutoka nishati uweza kiumeme na kuwa nishati ya kimakanika ya mwendo hovyo wa kimolekyuli(kusuguana nakufanya Ngurumo,Joto, na Mwanga).

Aina Za Nishati

Hutokana na asili au chanzo chake. Zifuatazo ni Baadhi yake:-

Makundi ya Nishati

Nishati kuwekwa katika makundi kulingana na matumizi ya mwanadamu na ukubwa wa uhitaji wake katika sura ya kijamii halafu pia na aina ya matumizi.

Nadharia Juu Ya Nishati

Fizikia hueleza nishati na tabia zake kimaumbile na msababisho kimatukio. Nayo tajwa kama nadharia; kufafanua mienendo.

Ufafanuzi

Ni nguvu iwezeshayo kazi kufanyika.

Kazi, kifizikia; ni kitendo kinachohusisha mabadilishano ya namna moja ya nishati hadi ingine ama pia kubadili hali ya kimaumbile na nafasi. Kwa mfano, kusogeza kiti ni kazi inayojidhirisha kwa kuhamisha kiti toka nukta moja hadi ingine.

Kizio cha kazi ni Juli.

Thathmini ya kihesabu ya kazi kulingana na nishati kifizikia hukokotolewa kwa thamani ya Juli na kadhaa.


Hali Kuu Mbili


Hujidhihirisha katika sura mbili na kutathminiwa hivi:

  • Nishati Uweza
  • Nishati Mwendeko


Nishati Uweza

Hii ni hali ya kiutathmini uwezo wa nishati kufanya kazi ama kuleta zao fulani la kikazi katika wakati ambao tukio halisi halijatendeka. K.m. jiwe juu ya kigingi cha mlima kabla halijadondoka lina tathmini ya uwezo wa nguvukazi sawa na mara litakapofika chini wakati wa kudondoka.


Nishati Mwendeko

Hii ni hali ya kiutathmini uwezo wa nishati kufanya kazi endelevu kiwakati. K.m. Jiwe lililorushwa lina nguvukazi alhali likipea.


Kanuni ya Uhifadhi Sawia Wa Nishati

Hii ni kanuni inayo elezea mbadilishano wa nishati kutoka hali moja hata nyingine; nayo inasema:

Nishati haiwezi kujengwa wala kubomolewa bali hubadilika kutoka hali moja had ingine.

Hii ni kusema kuwa, kiasi cha nishati kitumikacho kufanya kazi huwa sawa sawa na kiasi cha kazi kiutathmini. Hivyo kama kitendo kinaweza kurudishwa kilikotekea, kiasi kile kile cha nishati itapatikana.

Vile vile nishati inaposababisha tukio ambalo nishati za aina ingine kutukia, basi kiasi cha tathmini yake ni sawa sawa na nishati iliyosababisha.

Mifumo perepetua ya kimakanika

Mfano wa kanuni hii unaonekana kwenye bembea kama ile kwenye saa ya ukutani ya kimakanika. Jiwe la kuning'inia linapofika usawa wa juu kabisa; huwa na nishati uweza ya juu kabisa. Halafu Nishati Mwenendo huwa ni sifuri pale linapokuwa limesimama kabla ya kubembea na kuruidi chini. Katika hali ya wima kabisa, nishati uweza huwa ni sifuri na wakati nishati mwenendo huwa juu kabisa. Na hivyo kufanya mabadilishano ya Nishati Uweza na Nishati Mwenendo vinavyohusiana katika mifumo ya kazi za kimakanika.

Changamoto ya Nadharia ya Uhifadhi Sawia wa Nishati

Kanuni hii katika nyanja ya kifizikia imefika njia panda baada ya mifumo mpya wa uzalishaji nishati kugunduliwa.