Biashara ya watumwa : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Addbot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 15 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q118382 (translate me)
Addbot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 1 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q118382 (translate me)
Mstari 32: Mstari 32:
[[de:Sklaverei innerhalb von Schwarzafrika]]
[[de:Sklaverei innerhalb von Schwarzafrika]]
[[en:African slave trade]]
[[en:African slave trade]]
[[fr:Traites négrières]]
[[pl:Handel czarnymi niewolnikami]]
[[pl:Handel czarnymi niewolnikami]]
[[pt:Escravidão africana]]
[[pt:Escravidão africana]]

Pitio la 16:24, 20 Machi 2013

Soko la watumwa katika Roma ya Kale (picha ya karne ya 19).
Kusafirisha watumwa katika Afrika ya karne ya 19.

Biashara ya watumwa ni biashara inayohusu watumwa yaani watu wasio huru wakitazamwa kuwa mali ya binadamu wengine.

Historia

Katika historia ilitokea mara nyingi.

Uchumi wa Roma ya Kale ulitegemea watumwa waliokamatwa na kusafirishwa kutoka pande zote za mazingira ya Bahari Mediteranea.

Milki za makhalifa wa Uislamu ziliendelea kutegemea watumwa. Waosmani walichukua watoto wa Kikristo, hasa kutoka nchi za Balkani, na kuwapeleka kama watumwa katika sehemu za kusini za milki yao kama Misri walipofanya kazi kama wanajeshi. Biashara ya Waarabu kuhusu watumwa ilidumu miaka 1,300, na kupeleka mamilioni ya Waafrika upande wa Asia.

Mahitaji ya uchumi wa kimataifa tangu karne ya 15 yalisababisha kuongezeka kwa biashara ya watumwa hasa kutoka Afrika; mamilioni walikamatwa na watawala wa milki kwenye pwani za Afrika au Waarabu na kuuzwa kwa wafanyabiashara Wazungu waliowapeleka Amerika walipohitajika kwa kazi kwenye mashamba makubwa ya miwa na pamba.

Biashara hii ilianza kupingwa zaidi tangu mwisho wa karne ya 18; Mkutano wa Vienna (1814-1815) ulikuwa mapatano ya kwanza ya kimataifa yaliyolenga kukataza biashara ya watumwa kutoka Afrika.

Hata hivyo iliendelea kwa miaka kadhaa hasa upande wa bahari Hindi ambako wanafayabiashara Waislamu kama Tippu Tip waliendelea kukamata watumwa na kuwapeleka pwani na Zanzibar kulikokuwa na soko la watumwa kubwa kuliko yote.

Ukoloni ulimaliza kwa kiasi kikubwa biashara hiyo Afrika pia, ingawa Mauritania ilifanya utumwa kuwa kosa la jinai mwaka 2007 tu.

Tangu karne ya 20 utumwa na pia biashara ya watumwa zimepigwa marufuku katika mapatano ya kimataifa chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa.

Lakini miaka ya hivi karibuni imeona biashara mpya inayotumia nafasi za usairi wa kisasa; hata kama duniani hakuna utumwa kisheria tena, ni hasa wanawake na mabinti wanaouzwa kwa kazi haramu ya ukahaba kati ya nchi na nchi.

Utumwa, Ukaburu na Ubeberu