Luangwa (mto) : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
Addbot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 16 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q1321671 (translate me)
Legobot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 1 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q1321671 (translate me)
Mstari 28: Mstari 28:


[[Category:Mito ya Zambia]]
[[Category:Mito ya Zambia]]

[[ca:Riu Luangwa]]

Pitio la 11:37, 11 Machi 2013

Mto wa Luangwa
Bonde la Luangwa karibu na Ludeva nchini Zambia
Bonde la Luangwa karibu na Ludeva nchini Zambia
Chanzo Milima ya Mafinga, Zambia
Mdomo Mto Zambezi
Nchi za beseni ya mto Zambia, Malawi, Msumbiji
Urefu 806 km
Kimo cha chanzo 1,500 m
Kiasi cha maji kinachotolewa mdomoni 31.6 m³/s
Eneo la beseni (km²) 145,700 km²

Mto Luangwa ni mto mkubwa wa Zambia ya mashariki.

Kuna mto wa pili mdogo zaidi mwenye jina hili unaoishia katika Ziwa Kariba.

Mwendo

Luangwa ina chanzo chake katika milima ya Mafinga karibu na mpaka wa Tanzania na Malawi. Kwa jumla huelekea kusini sambamba na mpaka wa Malawi. Unapita maeneo mapana ya hifadhi za taifa za Luangwa Kaskazini na Luambe hadi Luangwa Kusini.

Takriban kilomita 500 baada ya chanzo bonde la mto linakuwa nyembamba lenye magenge makali kila upande. Kabla ya mdomo wake Luangwa ni mpaka kati ya Zambia na Msumbiji.

Mto unaishia katika Zambezi kwenye mji wa Luangwa.

Mabadiliko makubwa ya kiwango cha maji

Kiasi cha maji ndani ya mto hubadilika sana kufuatana na majira. Wakati wa ukame mto una maji kidogo na mahali pengi unapitika kwa miguu. Lakini kati ya Desemba hadi Machi wakati wa mvua katika milima ya chanzo chake na cha tawimito kuna maji mengi. Kila mwaka mwendo wa mto unaweza kubadilika kiasi kutokana na nguvu ya maji. Hii ni sababu moja ya kwamba hakuna watu wengi wanaokaa kando la mto huu.

Makala hii kuhusu maeneo ya Zambia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Luangwa (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.