Izazi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d +en
Addbot (majadiliano | michango)
d Bot: Migrating 1 interwiki links, now provided by Wikidata on d:q6101781 (translate me)
Mstari 44: Mstari 44:
[[Jamii:Mkoa wa Iringa]]
[[Jamii:Mkoa wa Iringa]]
[[Jamii:Wilaya ya Iringa Vijijini]]
[[Jamii:Wilaya ya Iringa Vijijini]]

[[en:Izazi]]

Pitio la 18:55, 9 Machi 2013


Kata ya Izazi
Nchi Tanzania
Mkoa Iringa
Wilaya Iringa Vijijini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 17,346

Izazi ni jina la kata ya Wilaya ya Iringa Vijijini katika tarafa ya Ismani, wilaya ya Iringa vijijini, Mkoa wa Iringa, Tanzania.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kabla kata haijamegwa, ilikuwa na wakazi wapatao 17,346.

Kwa sasa imebaki na vijiji vitatu tu, yaani Izazi, Makuka na Mnadani, vyote vikiwa katika Bonde la Ufa kwenye bwawa la Mtera (ambalo likijaa kabisa liko katika mita 698.5 juu ya usawa wa bahari). Ni sehemu ya chini zaidi katika Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania.

Eneo ni kubwa sana na lenye rutuba lakini watu ni wachache hasa kutokana na uhaba wa mvua ambayo kwa kawaida inaishia milimita 300 kwa mwaka. Kwa sababu hiyohiyo kilimo kikuu ni cha mtama.

Muhimu zaidi kiuchumi ni ufugaji: utovu wa ndorobo ulivutia kwanza Wasagara kutoka wilaya ya Kilosa (mwisho wa karne XIX), halafu Wamasai kutoka Mkoa wa Arusha (mwanzo wa karne XX). Ni vigumu kusema kama Wahehe, watawala wa eneo hilo, walikuwa wanaishi huko kabla ya wote, au walihamia pamoja na Wasagara. Baada yao Wagogo wengi walihamia kutoka Mkoa wa Dodoma. Ndiyo makabila manne yaliyochangia zaidi mwanzo wa makazi.

Baada ya bwawa la Mtera kupatikana, uvuvi umekuwa kivutio kipya kwa watu kutoka Tanzania nzima, ingawa uwezekano wake unategemea wingi wa maji.

Upande wa dini, baada ya ile ya jadi, Waarabu waliohamia kutoka Yemen kwa ajili ya biashara na uwindaji wakati wa ukoloni wa Waingereza walileta Uislamu. Kuanzia mwaka 1953 Ukristo ulienea zaidi kwa juhudi za Wakatoliki, halafu za Waanglikana. Siku hizi mchanganyiko wa watu umezidisha pia mchanganyiko wa madhehebu.

[1]

Marejeo

  1. "2002 Population and Housing Census General Report" (kwa Kiingereza). Government of Tanzania. Iliwekwa mnamo 2008-08-21. 
Kata za Wilaya ya Iringa Vijijini - Tanzania

Idodi | Ifunda | Ilolompya | Itunundu | Izazi | Kalenga | Kihanga | Kihorogota | Kising'a | Kiwere | Luhota | Lumuli | Lyamgungwe | Maboga | Magulilwa | Mahuninga | Malengamakali | Masaka | Mboliboli | Mgama | Migoli | Mlenge | Mlowa | Mseke | Nyang'oro | Nzihi | Ulanda | Wasa


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Iringa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Izazi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.