Polisario : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza id:Polisario
d r2.6.5) (Roboti: Imeongeza fa:جبهه پولیساریو
Mstari 30: Mstari 30:
[[es:Frente Polisario]]
[[es:Frente Polisario]]
[[eu:Fronte Polisarioa]]
[[eu:Fronte Polisarioa]]
[[fa:جبهه پولیساریو]]
[[fi:Polisario]]
[[fi:Polisario]]
[[fr:Front Polisario]]
[[fr:Front Polisario]]

Pitio la 14:28, 5 Machi 2013

Polisario ni vuguvugu la harakati za wenyeji asilia ya Sahara ya Magharibi kuipatia nchi yao uhuru.

"Polisario" ni kifupi cha jina la Kihispania Frente Popular de Liberación de Saguía el Hamra y Río de Oro ("Harakati ya watu kwa aijili ya Uhuru wa Saguia el Hamra na Rio de Oro") (Kiarabu:: الجبهة الشعبية لتحرير الساقية الحمراء ووادي الذهب al-jabHa ash-sha'biya litaHrir as-saaqiya al-Hamra wa wadi ad-dhaHab")

Kiongozi wa Polisario ni Katibu Mkuu Mohamed Abdelaziz aliyechaguliwa 1976. Ndiye pia mkuu wa jeshi la ukombozi wa Sahara lenye askari wa kiume na kike takriban 6000-7000. Anawajibika kama kiongozi wa chama mbele ya Kamati Kuu na Mkutano Mkuu unaofanyika kila baada ya miaka minne. Mkutano una wawakilishi waliochaguliwa katika makambi ya wakimbizi na wajumbe kutoka shirika za wanawake, vijana na wafanyakazi pia ktuoka vikosi vya jeshi. Kamati Kuu ina wajumbe 44; 12 kati ya hawa ni wajumbe wa siri kutoka Sahara ya Magharibi iliyoko chini ya utawala wa Maroko.

Polisario ilianza vita dhidi ya wakoloni Wahispania mwaka 1973 baada ya Hispania kuua viongozi wengi waliotafuta uhuru kwa njia za amani bila silaha.

Wahispania waliondoka Sahara ya Magharibi mwaka 1975 lakini Mauretania na Moroko walivamia nchi. Polisario ilifaulu dhidi ya Wamauretania lakini ilishindwa kuwaondoa Wamoroko. Ilipigana na jeshi la Moroko kati ya 1976 na 1991.

Polisario inatawala makambi ya wakimbizi katika Sahara ndani ya Algeria pamoja na kanda la jangwa nje ya ukuta uliojengwa na Maroko katika Sahara ya Magharibi. Wakazi wa makambi ni wakimbizi 100.000 walioondoka wakati wa vita; pamoja na watoto wao wamekuwa watu 155,000.

Kura ya wananchi katika Sahara ya Magharibi na makambi ya wakimbizi ilipataniwa mwaka 1990 kati ya Polisario na Maroko lakini haikufanyiwa hadi leo.

Viungo vya nje