Miriam Makeba : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.6.5) (Roboti: Imeongeza pam:Miriam Makeba Imebadilisha sk:Miriam Makebová
d r2.6.5) (Roboti: Imeongeza vep:Makeba Miriam, xh:Zenzile Miriam Makeba
Mstari 110: Mstari 110:
[[uk:Міріам Макеба]]
[[uk:Міріам Макеба]]
[[ur:میریم مکیبا]]
[[ur:میریم مکیبا]]
[[vep:Makeba Miriam]]
[[xh:Zenzile Miriam Makeba]]
[[yo:Miriam Makeba]]
[[yo:Miriam Makeba]]
[[zh:米瑞安·馬卡貝]]
[[zh:米瑞安·馬卡貝]]

Pitio la 11:22, 4 Machi 2013

Miriam Makeba

Miriam Makeba (4 Machi 193210 Novemba 2008), aliyeitwa pia Mama Afrika, alikuwa mwanamuziki kutoka nchi ya Afrika Kusini. Yeye ni mashuhuri hasa kwa kufahamisha muziki ya Afrika nje ya bara lake.

Maisha

Miriam Makeba alizaliwa tarehe 4 Machi 1932 katika jiji la Johannesburg, Afrika Kusini. Mama yake ni wa kabila la Swazi sangoma na Baba yake ni wa kabila la Xhosa. Baba yake Miriam alifariki wakati Miriam akiwa na umri wa miaka sita. Miriam alikuwa ni mwanamuziki pekee wakati huo aliyeweza kufanikiwa kuzieneza nyimbo zenye asili ya Kiafrika. Pia alikuwa ni miongoni mwa wanamuziki waasisi wa kuchanganya mitindo tofauti ya muziki na kutengeneza muziki wa kuvutia kama Kwaito. Alianza kazi ya muziki mwanzoni mwa 1950 akiwa na kundi la The Skylarks, baadaye alijiunga na kundi la Manhattan Brothers. Makundi hayo yalikuwa yakipiga muziki wa Jazz wenye vionjo vya Kiafrika kusini.

Mwaka 1959, Miriam alifanya onyesho kubwa pamoja na Hugh Masekela, mume wake wa baadaye. Maonyesho aliyofanya pamoja na albamu nzuri alizorekodi havikumpatia faida, baadaye alifanya matamasha katika nchi za Ulaya na Amerika. Ulipoanza mkakati wa kupinga Ubaguzi wa rangi uliyokuwa ukiendelea Afrika ya kusini Miriam aliamua kurudi nyumbani kupigania uhuru. Baadaye alialikwa Italia katika tamasha la filamu la Venice. Kati ya nyimbo za Miriam zilizo maarufu ni Patapata (kwa lugha ya KiXhosa ni "Qongaqothwan"). Wimbo maarufu wa Malaika uliotungwa na Fadhili William Miriam aliuimba akishirikiana na Harry Belafonte. Miriam alirudi tena nyumbani mwaka 1990, na mwaka 1992 alicheza filamu ya sarafina. Mwaka 2001 alitunukiwa tuzo ya dhahabu iliyoitwa Otto Hahn Peace Medal, pia alishika nafasi ya 38 ya wanamuziki bora kati ya mia moja waliopewa tuzo nchini Afrika ya kusini.

Mwaka wa 2005, Miriam alifanya ziara ya kimuziki kwa ajili ya kuwaaga marafiki wake wote duniani iliyomchukua miezi kumi na minne; alifanya maonyesho katika nchi zote alizotembelea wakati alipokuwa akifanya kazi ya muziki. Aliaga dunia kwa shtuko la moyo alfajiri ya tarehe 10 Novemba 2008, nchini Italia baada ya kutoa onyesho la muziki.

Orodha ya Albamu Kadhaa