Vita kati ya Irak na Uajemi : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.1) (Roboti: Imeongeza oc:Guèrra Iran-Iraq
d r2.7.1) (Boti: Inarbadilisha ro:Războiul Iran-Irak hadi ro:Războiul Irano-Irakian
Mstari 69: Mstari 69:
[[pnb:ایران عراق جنگ]]
[[pnb:ایران عراق جنگ]]
[[pt:Guerra Irã-Iraque]]
[[pt:Guerra Irã-Iraque]]
[[ro:Războiul Iran-Irak]]
[[ro:Războiul Irano-Irakian]]
[[ru:Ирано-иракская война]]
[[ru:Ирано-иракская война]]
[[sh:Iračko-iranski rat]]
[[sh:Iračko-iranski rat]]

Pitio la 16:40, 10 Februari 2013

Eneo la vita
Mstari mwekundu:Mwisho wa kusogea mbele kwa muda upande wa Iraki
Mstari njano:Mwisho wa kusogea mbele kwa muda upande wa Uajemi

Vita kati ya Irak na Uajemi ilitokea kuanzia Septemba 1980 hadi Agosti 1988. Ilipiganiwa kati ya majeshi ya nchi jirani za Irak na Uajemi (Iran) ikisababisha vifo vya watu milioni moja na kuishi bila mshindi. Iliitwa pia "Vita ya ghuba" kutokana na ghuba ya Uajemi ambako nchi zote mbili zinapakana na baadaye illitwa pia "vita ya kwanza ya ghuba" kutokana na vita za Marekani dhidi ya Irak zilizofuata baadaye.

Vita ilianza kwa mashambulio ya Irak dhidi ya Uajemi. Dikteta Saddam Hussein wa Irak alitaka kutumia nafasi ya kudhoofishwa kwa jeshi la Uajemi baada ya mapinduzi ya mwaka 1979. Mwaka ule serikali ya shah ya Uajemi ilipinduliwa na harakati iliyoongozwa na kiongozi Mwislamu Ruhollah Khomeini na maafisa wengi wa jeshi la shah ama waliuawa au kukimbia nchi. Saddam Hussein alilenga kushika utawala juu ya Shat al Arab ambayo ni mdomo wa mito Frati na Hidekeli kwenye ghuba ambako mizigo ya mafuta ya petroli ya Irak inapaswa kupita ikiuzwa nje. Alilenga pia kutwaa sehemu za Uajemi zilizokuwa na wasemaji wa lugha ya Kiarabu na sehemu hizi zinaitwa Khuzistan; Saddam alidai ya kwamba ilikuwa eneo la Kihistoria ya Irak iliyokamatwa na Uajemi.

Mwanzoni Wairaki walifaulu kuteka maeneo karibu na mpakani upande wa Uajemi lakini serikali mpya ya Kiislamu iliweza kutuma wanamigambo hasa vijana wengi ambao walikuwa tayari kufa hata kama hawakufundishwa kazi ya askari. Mtindo huu ulirudisha Wairaki nyuma lakini ulikuwa pia sababu ya kwamba Waajemi wengi walikufa kushinda Wairaki. Ila tu Uajemi ni nchi yenye watu wengi zaidi na Waajemi wengi walikuwa tayari kwa kifo kwa sababu waliona ya kwamba nchi yao ilishambuliwa. Viongozi wa kidini walitangaza ya kwamba ilikuwa wajibu wa kidini kushika silaha.

Nchi za nje kama Marekani zilihofia mapindizi ya Kiislamu zikasaidia Irak kwa silaha na habari kama picha kutoka vyombo vya angani. Vita hii ilikuwa maarufu kwa sababu Irak ilitumia silaha marufuku kama gesi ya sumu.

Vita iliendelea ingawa Umoja wa mataifa ilisihi pande zote mbili kumaliza mauaji. Mwishowe walipatana kusimamisha mapigano na kurudi kwa mipaka ya kimataifa kwa sababu ya uchovu na uharibifu mkubwa kwenye pande zote mbili.


Marejeo ya Nje


Kigezo:Link FA