Saratani : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza pa:ਰਾਜਫੋੜਾ
Mstari 64: Mstari 64:
[[io:Kancero]]
[[io:Kancero]]
[[is:Krabbamein]]
[[is:Krabbamein]]
[[it:Neoplasia#Comportamento biologico: benignità e malignità]]
[[ja:悪性腫瘍]]
[[ja:悪性腫瘍]]
[[jv:Kanker]]
[[jv:Kanker]]

Pitio la 18:22, 9 Februari 2013

Picha ya eksirei inayoonyesha kivuli cha kansa katika mapafu

Saratani (Ar. سرطان sartan) au kansa (Ing. cancer) ni aina za ugonjwa unaoanzishwa na seli za mwili zinazoanza kujigawa yaani kukua bila utaratibu na bila mwisho. Ukuaji huu unaleta uvimbe mwilini unaozidi kuwa kubwa hadi inabana viungo vya mwili kama neva, mishipa ya damu, ubongo, mapafu, maini, utumbo na kadhalika na kuzuia visifanye kazi. Pamoja na hayo kansa / saratani huwa na tabia za kujisambaza mwilini mahali pengi baada ya muda fulani na kusababisha kutokea kwa vimbe nyingi mwilini vinavyoendelea kukua hovyo. Kama uvimbe hauna uwezo wa kusambaa seli zake mwilini na kusababisha vimbe mpya si saratani.

Kansa inaweza kutokea kwa mtu yeyote lakini hutokea zaidi kwa watu wenye umri mkubwa na watu anaoathiriwa na kemikali mbalimbali. Katika nchi zilizoendelea ambako wanachi hufikia umri mkubwa saratani iko kati ya sababu kuu za kifo.

Uchunguzi na matibabu ya kansa ni utaalamu wa onkolojia ndani ya somo la tiba.


Kigezo:Link FA