Pangani (mto) : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.1) (Roboti: Imeongeza es:Río Pangani
d r2.7.2) (Roboti: Imeongeza hr:Pangani
Mstari 21: Mstari 21:
[[en:Pangani River]]
[[en:Pangani River]]
[[es:Río Pangani]]
[[es:Río Pangani]]
[[hr:Pangani]]
[[lt:Panganis]]
[[lt:Panganis]]
[[pl:Pangani]]
[[pl:Pangani]]

Pitio la 00:36, 6 Februari 2013

Beseni ya Mto wa Pangani

Mto wa Pangani ni kati ya mito mikubwa ya Tanzania. Unabeba maji ya Milima ya Meru, Kilimanjaro, Pare na Usambara kwenda Bahari ya Hindi. Mdomo wake uko mjini Pangani.

Beseni ya Pangani ni eneo la 43,650 km2. Karibu yote imo Tanzania isipokuwa kuna pia 3,914 km2 huko Kenya katika mazingira ya Taveta.

Chanzo cha mto Pangani ni ziwa la Nyumba ya Mungu kusini ya Moshi. Mito inayoingia Nyumba ya Mungu ni hasa Kikuletwa na Ruvu (Luvu). Kikuletwa hupokea maji kutoka Mlima wa Meru na mitelemko ya Kilimanjaro upande wa Kusini. Ruvu hupokea maji kutoka mitelemko ya Kilimanjaro upande wa Mashariki pamoja na Ziwa la Jipe.

Mto wa Pangani unaendelea km 432 hadi Pangani mjini unapoingia katika Bahari Hindi. Jumla ya wakazi katika beseni ya Pangani ni milioni 3.7.

Mto wa Pangani unategemea misitu panapokusanywa maji yake. Misitu hii imepungua sana kutokana na uenezaji wa mashamba, kukatwa kwa miti kwa ajili ya makaa na matumizi ya ubao. Vilevile machafuko yamekuwa hatari kwa ajili ya afya ya mto na watu wanaotegemea maji yake. Asili ya machafuko ni hasa kilimo, mvua hupeleka mbolea mtoni na kusababisha kukua kwa wingi majani yasiyotakika. Uvuvi umezidi vilevile hadi kuhatarisha samaki wenyewe.

Viungo vya nje