Aral (ziwa) : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza af:Aralmeer
d Roboti: Imeongeza be:Аральскае мора
Mstari 30: Mstari 30:
[[ar:بحر آرال]]
[[ar:بحر آرال]]
[[bat-smg:Arala jūra]]
[[bat-smg:Arala jūra]]
[[be:Аральскае мора]]
[[be-x-old:Аральскае мора]]
[[be-x-old:Аральскае мора]]
[[bg:Аралско море]]
[[bg:Аралско море]]

Pitio la 01:03, 25 Januari 2013

Meli ya ziwani inayokaa jangwani mahali pa bandari zamani

Ziwa la Aral (Kikazakhi: Арал Теңізі (aral tengizi), Kiuzbeki Orol dengizi, Kirusi Аральскοе мοре aralskoye more) ni ziwa la Asia ya Kati linalopakana na Kazakhstan na Uzbekistan. Hadi mwaka 1960 lilikuwa na eneo la maji la 68,000 km² lakini limepungua hadi kubaki na 17,160 km² pekee mwaka 2004. Tangu 1987 kupungua kwa maji kulisababisha ugawaji wa ziwa katika sehemu mbili upande wa kazkazini na upande wa kusini ambazo haziungana tena.

Mito mikubwa inayoingia na kubeba maji yake ni Amu Darya na Syr Darya na mito hii ilitumiwa katika mipango ya Umoja wa Kisovyeti kwa umwagiliaji wa mashamba makubwa ya pamba na mazao mengine. Miradi hii iliyoanzishwa katika mazingira yabisi iliendelea kwa miaka 30 hivi hadi kushindikana; maji yamepotea kwa wingi mashambani na katika mifereji kutokana na usimbishaji na kusababisha kupunguza kwa mazao. Kiasi cha chumvi ardhini kiliongezeka sana jinsi ilivyo mara nyingi katika miradi ya umwagiliaji ya nchi za joto na kumaliza rutba ya udongo.

Ziwa halikupokea tena kiasi chake cha maji likapungua. Sehemu kubwa za eneo la ziwa la awali zimekuwa jangwa. Maji yaliyobaki yameharibika kutokana na maji sumu ya viwanda na mbolea nyingi iliyosukumwa kutoka mashamba mitoni halafu ziwani.

Kuna mradi wa kuokoa angalau sehemu ndogo ya kaskazini. Ukuta ulijengwa kwa shabaha ya kuzuia upotevu wa maji katika jangwa la msingi wa ziwa la kale. Uwiano wa maji yamepanda tena katika sehemu hii ndogo.

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Aral (ziwa) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA Kigezo:Link FA