Daniel Comboni : Tofauti kati ya masahihisho

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Content deleted Content added
d r2.7.1) (roboti Nyongeza: arz:الآباء الكومبونيان
d r2.7.3) (Roboti: Imeongeza ar:كمبوني
Mstari 45: Mstari 45:
[[Jamii:Waliofariki 1881]]
[[Jamii:Waliofariki 1881]]


[[ar:كمبوني]]
[[arz:الآباء الكومبونيان]]
[[arz:الآباء الكومبونيان]]
[[ca:Daniele Comboni]]
[[ca:Daniele Comboni]]

Pitio la 15:05, 14 Januari 2013

Mtakatifu Daniele Comboni

Daniele Comboni (Limone sul Garda, Italia 15 Machi 1831 - Khartoum, Sudan, 10 Oktoba 1881), alikuwa mmisionari wa Kanisa Katoliki nchini Sudan.

Ndiye aliyeanzisha shirika la Wamisionari wa Moyo Mtakatifu wa Yesu na shirika la Masista wa Afrika, yaani Wamisionari Wakomboni na Masista Wakomboni.

Alitangazwa kuwa mtakatifu na Papa Yohane Paulo II tarehe 5 Oktoba, 2003.

Sikukuu yake ni 10 Oktoba.

Maisha

Daniele Comboni alikuwa moja kati ya ndugu wanane, lakini ndugu zake walifariki wote walipokuwa watoto.

Daniele aliacha wazazi wake alipokuwa na miaka 12 na alienda Verona kusoma kwenye shule ya padri Nicola Mazza ambapo alichagua kuwa padri na kwenda Afrika kama mmisionari.

Alifika Misri na wamisionari wengine watano (1857). Wote waliendelea hadi kufika Sudan kusini.

Baada ya miaka miwili Daniele alirudi Italia kwa sababu wamisionari wenzake walifariki huko Sudan.

Siku moja, alipokuwa akiomba ndani ya basilika la Mt. Petro mjini Roma alitafakari kuhusu njia ya kueneza Injili barani Afrika.

Aliandika “Mpango ya Kuirudishia Afrika Uhai”. Katika mpango huu Comboni alisema ya kwamba ni lazima kusaidia Waafrika kukua katika elimu ili wenyewe waweze kupanga maendeleo yao.

Mwaka 1867 alianza shirika la mapadre na mabruda.

Mwaka 1877 alipewa na Papa daraja ya askofu ili kujenga Kanisa katika Afrika ya Kati (Sudan, Uganda, Kenya ya leo).

Daniele Comboni aliaga dunia tarehe 10 Oktoba 1881.

Viungo vya Nje

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.